Nguvu ya Umma Afrika Mashariki ni funzo tosha

Nguvu ya Umma Afrika Mashariki ni funzo tosha

airmax

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2022
Posts
870
Reaction score
965
Nchi za kiafrika tunajifunza nini kwa mandamano haya? nijambo la kushangaza ya kwamba raisi aliyejinadi kushinda uchaguzi wa uraisi na kuthibitishwa na tume ya uchaguzi, yanayotokea leo yanatia aibu, waandamanji waliojitokeza kwa mujibu wa takwimu ni zaidi ya asilimia 77, hapa swali ni je nani walimchagua raisi huyu?

Wapinzani walipeleka mahakamani hoja 7, majaji wakiongozwa na jaji mkuu walitupa karibu hoja zote sasa swali liko hapa, je walitoa hukumu ya haki?

Je, walio mchagua wanaweza kuandamana kumkataa mtu waliyemchagua miezi michache tu iliyopita?? jibu ni HAPANA ulikuwa uchaguzi wa hila

Nina hakika yajayo yanafurahisha, hawa viongozi dhalimu wote wataanguka tena kwa kishindo kikuu, hawa walioingia madarakani wote walituhumiwa kwa ufisadi wa Arror na Kimwarer Dams, baada ya kuingia madarakani tu, mashataka yote yameondolewa

Makamu wa Rais alishatakiwa kwa wizi wa fedha za county, tayari mashtaka yameondolewa, huku mashahidi wakidai walitishwa na utawala wa Rais aliyemaliza muda wake ili watoe ushahidi wa uongo, sasa Mungu anawaumbua wanaojitokeza kwenye maandamano ni wengi zaidi ya waliowaliopigia kura hii ni ajabu

Nyepesi nyepesi yasemekana Rais yuko nje ya nchi, nadhani kakimbia aibu, waafrika tusimame dhidi ya viongozi wote wanaoingia madarakani kwa wizi wa kura na dawa yao ni mandamano bila ukomo

Wasaalaam.

 
Nchi za kiafrika tunajifunza nini kwa mandamano haya? nijambo la kushangaza ya kwamba raisi aliyejinadi kushinda uchaguzi wa uraisi na kuthibitishwa na tume ya uchaguzi, yanayotokea leo yanatia aibu, waandamanji waliojitokeza kwa mujibu wa takwimu ni zaidi ya asilimia 77...
Kwahiyo waandamanaji wote ni wapiga kura na walipiga kura. Na walimpigia Raila.

Kwani Hali ya Maisha ilikuwaje wakati Ruto anaingia madarakani?
 
Back
Top Bottom