Nimefurahishwa na uchambuzi ulioandikwa kwenye gazeti la KULIKONI hivi karibuni. Nitanukuu sehemu tu ya uchambuzi huu ili tuweze kuujadili.
"Tabaka la mibaka-uchumi (mafisadi) limeteka nyara mchakato na mustakabali mzima wa siasa na uchumi wa nchi. Tabaka hili, pamoja na kuvamia nafasi za kisiasa kama ubunge na ukamanda wa vijana, linafadhili pia nafasi za uongozi, toka urais hadi ubunge, na nafasi kuu ndani ya chama... Tabaka hili limeweza kupenyeza watu wake katika taasisi nyeti kama usalama wa taifa, Ikulu, Takukuru, mahakama na bunge. Tabaka hili limeunda na kuongoza serikali isiyo rasmi ndani ya nchi, lakini yenye nguvu kuliko serikali ya Kikwete; haliwezi kukemewa, bali linaweza kuitisha serikali; hasa pale maslahi ya watu wao yanapoguswa! Tabaka hili hatari linaipenda Tanzania (kwa raslimali zilizomo), lakini haliwapendi Watanzania; lipo tayari kudhuru na hata kuua kisiasa na kimwili, inapofikia kutetea maslahi yake. Hili haliwezi kung'olewa kwa nguvu ya serikali iliyomo madarakani, ila kwa KIPIGO CHA NGUVU YA UMMA.