SoC04 Nguvu ya vijana kwenye urithi wa nchi

SoC04 Nguvu ya vijana kwenye urithi wa nchi

Tanzania Tuitakayo competition threads

KimbakaeKO

Member
Joined
Jun 23, 2024
Posts
39
Reaction score
45
Vijana ni kundi la watu ambalo lipo kati ya umri wa miaka 18 mpaka 40, hii hutofautiana kwa baadhi ya jamii nyingine.

Kundi hili ndio kubwa zaidi kwenye nchi yetu na linaongezeka kwa kasi kila siku(Sensa 2012-2022).
Katika kipindi hichi cha ujana ndicho kinapaswa Vijana wapewe Elimu na Mafunzo, Uzoefu na kuandaliwa kwa majukumu ya baadae.

Vijana ni kundi lenye nguvu katika jamii linaweza kupatw na athari nyingi lisipoangaliwa kwa makini kutokana na sera mbalimbali zilizowekwa kama vile za Kisiasa, Kiuchumi na Kijamii.

Urithi ni hali ya kumilikishwa Mali, Elimu na mambo mbalimbali kutoka kwa ambaye una mahusiano nae Kinasaba, Kijamii na Kitaifa.

Mrithi wa chochote anatarajiwa kuendeleza alivyorithishwa. Hii ni moja ya lengo la kurithishwa, mbali na hili utakuwa umepoteza thamani ya urithi.

Jamii zetu zilizopita zklikuwa zinawarithisha vizazi vyao ili kushika majukumu yao ya baadae mfano Wasukuma,Wanyamwezi, Wamasai,Watu wa pwani na Visiwani.

Vijana hao walikuwa wanafunzwa Kulima, Kuvua, Kuchunga na Kutengeneza samani mbalimbali kama vile Kuchonga, Kufinyanga nakadhalika.

Kwa shughuli hizi waliokuwa wanafundishwa(kurithishwa),vijana walikuwa wanamiliki mashamba, nyumba na kuenrelesha familia zao(mke na watoto).

Tena hakukuwa na ambaye analalamika kazi hakuna au hana shughuli zakufanya aendeleshe maisha yake.

Mashujaa wa Afrika
Mara tu, unapolisikia jina hili(Shujaa) huwa linatoa taswira kwenye Ubongo kwamba ni jambo kubwa ambalo limefanya au linalofanyika na mtu/watu ambalo wengine hatuliwezi kufanya.

Ushujaa huu hawakuupata kutoka kwa Majini, Mizimu au Malaika bali walirithishwa kutoka kwa Baba/Mama zao na Babu/Bibi zao waliwarunza na kuwapa maandalizi ya hali ya juu kabisa.

Mashujaa walioikomboa Afrika na kuipigania katika hali zote Mali na Nafsi zao, wengi wao hawakuzidi miaka 40. Hivyo basi asilimia 90 walikuwa ni vijana.

Mfano wa hao Kwame Nkuruma, Patrice Lumumba, Nelson Mandela na Mwl Nyerere na wengine wengi kutoka hapa Afrika.

Jicho La Huzuni
Wakati wote huwa nahuzunika kutokana na hali zinazowafika vijana wenzangu, mpaka hupelekea moyo kuuma na kupatwa na msongo wa mawazo.

Vijana wengi hutumbukia katika mambo mabaya tofauti tofauti hasa wale wanaoishi katika jamii masikini(Uswahilini) na huko ndipo kwenye kundi kubwa la vijana.

Huko mitaa ya walalahoi(Uswahilini) ambapo ninapotokea Mimi, kama vile maeneo ya Tandale, Tandika, Mbagala na vitongoji vyake, Gongo la mboto, Dodoma majengo na pengine panapofanana na haya.

Vijana wengi wa maeneo haya waliosoma ni wachache sana, kama wale wahitimu shule ya msingi,kidato cha nne na sita, na wale waliobahatika kufika vyuo vya kati na vikuu lakini pia waliopata ujuzi wa ufundi stadi kupitia vyuo vya Maendeleo na Veta. Kundi lote hili baada ya kukosa ajira linaungana pamoja mtaani na wale wasiosoma au kuacha Elimu ya ngazi yoyote, ndipo wanakuja kutumbukia katika mambo maovu.

Vijana wakiume, huingia katika Wizi na Ujambazi, Utumiaji wa dawa za kulevya(Bangi, shisha na kokeni) na kuvuta gundi.

Vijana wakike, hujiingiza katika kuuza miili yao kimtandao au udada poa, mimba zisizotarajiwa na kusababisha watoto wa mtaani kuongezeka lakini pia kushiriki katika wizi na ujambazi.

Hili ni ongezeko kubwa sana la vijana wa aina hii ambao husababisha watoto wao kutochukulia umuhimu suala la elimu na ujuzi katika maisha yao.

Hivyo imekuwa kawada mitaani mwetu, vijana kuingia kwenye makundi maovu lakini pia kujivunia hayo wayatendayo na kujitukuza kwa majina kama vile PanyaRoad, VidegeJohn, Viselengi, UtumboNdizi, Mizinga22, No 45, No 43 na No D na E nk.

Twendeni tukatazame, hali zilivyo mitaani(Uswahilini) ni hatari mno. Tunajitengenezea bomu kubwa sana baadae bila kujua.

Nini Cha kufanya(Tanzania Tuitakayo)

Serikali inapaswa kuitolea macho jamii haswa kwenye kundi la vijana na kurekebisha na kuboresha sera za Kielimu na Ujuzi Kiuchumi na Kisiasa.

(i) Elimu na Ujuzi
Mfumo wa Elimu unapaswa kubadilika kwa kuboresha na kuimarisha Elimu ya Msingi na kubadilisha Elimu ya sekondari kuwa na mfumo wa vyuo vya Maendeleo(FDC) na baadhi ya shule za sekondari kuwa vyuo vya kati.
Lakini pia Vyuo vya Maendeleo(FDC) kuviongezea umahiri na uwezo katika fani mbalimbali zinazofundishwa.
Hapa wanafunzi wataweza kujiendeleza na elimu kwa ngazi inayofuta mpaka kufikia chuo kikuu kwa mpango uliowekwa. Na ikiwa hawatoweza kuendelea basi wataweza kujiajiri na kuajiriwa kwa ngazi waliopo.
Mimi ni shuhuda wa hili, nina marafiki zangu waliojiajiri na wengine kuajiriwa kwenye mashirika ya serikali mfano Tanesco na mashirika binafsi hasa viwandani.

(ii) Kisiasa
Vijana wanapaswa kupata kipaumbele katika nyazifa mbalimbaliza kisiasa, Taasisi na jumuiya ili kuwawezesha kupata ujuzi na uzoefu ambao utawasaidia kuwa viongozi bora baadae.

Vijana waweze kupewa kazi za kimkataba kwa kubadilishana katika mashirika ya kiserikali na binafsi hata kwa miaka 2 tu, baada ya kuhitimu mafunzo yao mpaka pale watakapopata ajira rasmi.
Lakini pia kulipwa angalau robo ya mshahara ili wajikimu sasa na baada mkataba kuuisha.

(iii)Kiuchumi
Serikali inapaswa kuanzisha maeneo ya uzalishaji kwa ajili ya wale waliohitimu mafunzo mbalimbali ya kielimu kama vile wanavyohitimu vijana wa JKT na kwenda kuishi kambini takribani miaka 2.

Serikali inapaswa kutoa mikopo bila riba na kwa uwazi zaidi na iwe yenye kufuatialia kwa karibu.
Serikali ifuatilie vijana kwa ukaribu zaidi ili kubaini wasiojishughulisha. Hii ianze kwenye ngazi za chini za uongozi, kwa mjumbe wa nyumba 10 ili kubaini wimbi la wasiojishughulisha.

Kwa kufanya hili, tutapata takwimu za vijana wasiofanyakazi/shughili wanaosoma na wasiosoma. Hivyo tutaweza kudhibiti wimbi la vijana wazurulaji na kuwainua katika nyanja mbalimbali kimaendeleo.

Vijana ni Taifa la leo, la kesho na ndio warithi wa kubwa wa nchi hii. Tutakapoicha injini hii iendelee kuharibika , gari hili halitasogea hata mita moja.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom