Nguvu ya XI Jinping: Trump mwenyewe aenda uwanjani kumpokea

Xi Jinping

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2023
Posts
9,548
Reaction score
28,817
Miaka zaidi ya 60 imepita tangu mara ya mwisho Raisi wa Marekani aende airport kumpokea mgeni mbaye ni Raisi wa taifa lingine isipokuwa mgeni huyo awe ni Papa wa kanisa Katoliki
​
MAREKANI IMEWEKA ITIFAKI YA KIWANGO CHA JUU SANA KWENYE ZIARA YA XI JINPING​


Katika ziara nyingi za viongozi wa kigeni nchini Marekani, mgeni hupokelewa uwanjani na maafisa wa serikali na itifaki, huku Rais wa Marekani akikutana naye baadaye White House kwa hafla rasmi.​


Lakini kwa Rais Xi Jinping, Donald Trump alivunja utaratibu huo.​


Septemba 23, 2026, Trump mwenyewe alikwenda Joint Base Andrews kumpokea Xi na mke wake, Peng Liyuan, walipowasili Marekani, utaratibu adimu sana kwa Rais wa Marekani​


Na mapokezi hayo ya airport hayakuwa tukio pekee.​


Ratiba ya Xi ilijumuisha State Arrival Ceremony White House, mapitio ya kijeshi katika Rose Garden, mazungumzo ya ngazi ya juu kati ya viongozi hao na State Dinner iliyowakutanisha baadhi ya vigogo wakubwa wa teknolojia na biashara duniani akiwemo Elon Musk, Tim Cook, Sundar Pichai, Jeff Bezos, Sam Altman na Jensen Huang

Ajenda kuu ilihusisha masuala mazito ya biashara, rare earths na Artificial Intelligence (AI), pamoja na masuala mengine ya kimkakati kati ya Marekani na China

Kwa historia ya hivi karibuni, kumpokea kiongozi wa nchi nyingine moja kwa moja airport imekuwa jambo lisilo la kawaida.

Miongoni mwa mifano maarufu ya hivi karibuni ya marais wa Marekani kumpokea mgeni airport:

​
  • Mwaka 2008, Raisi George Bush alimkaribisha Papa Benedict XVI katika kiwanja cha Joint Base Andrews​

  • Mwaka 2015, Barack Obama alimkaribisha Papa Francis Joint Base Andrews​

Kinachoonekana kwenye ziara ya Xi si mapokezi ya kawaida ya kidiplomasia. Marekani imeandaa red carpet ya kiwango cha juu, kuanzia airport hadi White House, huku biashara, teknolojia, AI na rare earths zikiwa sehemu muhimu za ajenda

Baadhi ya wachambuzi husema Xi is the most powerful person in the world
​
 
Trump anapenda sifa, ukimuona kajiweka mbele Kuna uwezekano mkubwa anataka kuonyesha ubabe. Sijafatilia hayo mapokezi lakini Kuna uwezekano kulikuwa na show ya jet zake na bombers kama alivyofanya kwa Putin.
 
Trump anapenda sifa, ukimuona kajiweka mbele Kuna uwezekano mkubwa anataka kuonyesha ubabe. Sijafatilia hayo mapokezi lakini Kuna uwezekano kulikuwa na show ya jet zake na bombers kama alivyofanya kwa Putin.
Trump alimfuata Xi moja kwa moja Joint Base Andrews kumpokea. Kulikuwa na red carpet, bendi ya kijeshi na hakukuwa na maonyesho ya kijeshi yalikuwa mapokezi rasmi ya kiserikali.

Mapokezi ya Putin yalifanyika Alaska, kwenye Joint Base Elmendorf-Richardson,

Kwa hiyo, Xi alipata mapokezi ya juu sana ya kidiplomasia, lakini Putin alipata mapokezi yenye military display iliyo wazi zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…