Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,151
- 4,277
Hakuna kitu chenye nguvu na kinachozalisha kama giza. Nadiriki kusema nguvu ya kiumbaji ipo katika giza kuu. Ninaweza nisieleweke mapema ila nina uhakika kupitia mifano nitakayoitoa angalau tunaweza kupata maana ya maana.
Mfano wa 1. Biblia katika kuelezea usuli na asili ya uumbaji imetamka uwepo wa giza na ukiwa na ni kama vitu vilitokea gizani baadae.
Mfano wa 2. Mimba ya kiumbe inapotungwa, zoezi hili hufanyika katika giza.
Mfano wa 3. Mbegu za mimea zinapopandwa hufukiwa gizani (ardhini) na huko mchakato mzima wa uotaji hufanyika.
Mfano wa 4. Njia ya mojawapo ya kuingia katika ulimwengu wa roho ni ndoto na ndoto huja mtu anapokuwa amelala (sawa na kuwa gizani).
Mifano hiyo michache Inaweza kutusaidia angalau kwa kupapasa kuiona nguvu ya giza na kuona giza kama eneo muhimu la kuvuna nguvu za kiumbaji.
Ipo tafsiri mbaya juu ya nguvu za giza ila lengo la niliyoyaandika siyo tafsri hiyo ila ni kuonesha kuwa giza lina nguvu na Lina umuhimu wake. Hivyo kuwa na maarifa juu ya nguvu za giza ni jambo la muhimu sana kwa mtu anayetamani kuuona uumbaji wake.
Karibu.