BICHWA KOMWE -
JF-Expert Member
- Jul 21, 2022
- 6,373
- 16,073
😂😂😂😂😂Body,Mind, and Soul
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
😂😂😂😂😂Body,Mind, and Soul
Kwako ukiwa ndani ya box 📦 ila njee kwa wote ndivyo mambo ya livyo, ila wewe ni bigwa wa evasion😁😁😁😁Kwangu haiwezi kuwa hivyo
Mkuu evasion ni kitu gani hicho, nijuze tafadhaliKwako ukiwa ndani ya box 📦 ila njee kwa wote ndivyo mambo ya livyo, ila wewe ni bigwa wa evasion😁😁😁😁
Kukwepa au kuepuka kitu au swaliMkuu evasion ni kitu gani hicho, nijuze tafadhali
Ni kweli ni muhimu Kushukuru kwa kukubaliana na hali halisi alafu ku move on, lakini sio kufurahia mabaya na kuchukulia poa.Kushukuru sio kukubaliana na jambo baya, ni kusema kwamba wewe ni mkubwa kuliko jambo baya.
Unaposhukuru unatengeneza mtetemo chanya, na utavutia mambo mengine mengi yaliyo chanya.
we shukuru tu sema asante na itoke moyoni. It creates a unique positive charge which will attract more positivity and good things in your way.
Cc: min -me
unacheka nini? we bichwa😂😂😂😂😂
Hiyo ni judgment yako juu yangu, ni projection of what you think I am. It has nothing to do with me.Kukwepa au kuepuka kitu au swali
😂😂😂😂 sijui ataunacheka nini? we bichwa
Hata kujitoa ufahamu, (kuahirisha kufikiri), a. K. a kujizima dataKwa hapa kwetu Afrika; nilichogundua kupiga domo kunalipa maana watu wanaamini wapiga domo ndo wenye akili, ushirikiano na ushawishi..
Mafanikio ni Nini ?hayo ulioandika yanalipa kwenye Christian western societies au jamii zinazofwata western philosophy i.e meritocracy, tanzagiza haifwati meritocracy hivyo hard work haiwi rewarded na hailipi wanaoafanikiwa (karibia)wote ni wezi, walaghai na wababaishaji btw rostamu is 8 billion dollars worth, how is that possible kwenye nchi masikini kabisa duniani kama tanzagiza?
Mafanikio ni Nini ?
Huenda ungejibu hili.....swali gumu kulijibu …
Usingesema haya..., Sababu technically kufanikiwa ni kufanikisha kile ambacho umekianza kwahio kama motive ni monetary basi kwenye jamii inayocheza rafu wewe kufanya fair ni vigumu kupata hizo material things..., lakini kama wewe ulichokianza ni kusaidia jamii yako basi hautafanikiwa kama ukiwaibia na kupata pesa wakati wao wanadumaa kwa kufanya hivyo utakuwa haijafanikisha ustawi wao bali umezidi kuwadidimiza...hayo ulioandika yanalipa kwenye Christian western societies au jamii zinazofwata western philosophy i.e meritocracy, tanzagiza haifwati meritocracy hivyo hard work haiwi rewarded na hailipi wanaoafanikiwa (karibia)wote ni wezi, walaghai na wababaishaji btw rostamu is 8 billion dollars worth, how is that possible kwenye nchi masikini kabisa duniani kama tanzagiza?
Asante kaka kwa kutupa elimu adimu sanaWanabodi,
Nipashe ya Leo 16/06/2024
View attachment 3018955
NGUZO 7 ZA MANISTATION
Hili ni bandiko mwendelezo wa wiki iliyopita. Kama hukulisoma bandiko la kwanza, anzia hapa Siri ya Mafanikio Kupitia Manifestation -1: Manifestation ni Nini?
Kwa wasomaji wapya, wiki iliyopita niliintruduce topic ya kitu kinachoitwa manifestation, kwa lugha rahisi ni kuweka nia na kudhamiria kwa dhati kufanikiwa, kwa kutumia nguvu za nia, zilizomo ndani yako. Nikataja manifestations ina nguzo kuu 7.
Nguzo kuu ya kwanza ni Foundation: Msingi mkuu wa Manifestation ni nia na imani ya kufanikiwa.
- Foundation: Msingi wa Manifestation
- Laws: Sheria za Manifestation
- Vibrations:Mitetemo ya Manifestation
- Intention: Kuweka Nia
- Visualization: Kuona kwa jicho la ndani
- Affirmations: Kutumia Imani Chanya ya Kufanikiwa
- Process: Utekelezaji wa Manifestation.
Kuna makundi makuu 5 ya watu waliofanikiwa.
1. The Inheritors: hawa ni watu waliozaliwa kwenye familia tajiri, wafalme na matajiri, na viongozi, mtoto wa familia hii anazaliwa na kujikuta amerithi utajiri, hata kama kichwani ni zero, huyu atahesabika amefanikiwa.
2. The Best Brains: Hawa ni watu wenye akili nzuri, wasomi, wataajiriwa kazi nzuri, na kulipwa mishahara, hivyo kupata maisha ya mafanikio, kundi hili ni la waajiriwa.
3. The Best Talent: Hili ni kundi la watu wenye vipaji, wanamuziki, wasanii, waigizaji, wacheza mpira, au watu wenye vipaji vyovyote vinavyowaletea maisha mazuri, wakiwemo waandishi wa habari, watangazaji, etc. Mwanamuziki Michael Jackson, hakusoma hata darasa moja!, huyu Daimond Platnum wetu, Hamonise ni darasa la saba tuu lakini wamefanikiwa kutokana na vipaji.
4. The Hard Workers: Wafanyakazi kwa bidii, hawa ni working class, ukifanyakazi kwa bidii, utafanikiwa, hili ni kundi la wanaofanikiwa kwa kutumia nguvu zao, “mtaji wa masikini ni nguvu zake”.
5. Fixers: Hili ni kundi la mwisho la wapiga domo!, humu ndio kuna wanasiasa, wanaweza wasiwe best brains, hawana talent yoyote, sio hard workers, lakini wanafanikiwa kwa kupiga deals, fix na kupiga domo.
Makundi yote hayo yanafanikiwa kwa kufanya manifestation kwa kujua au bila kujua.
Lugha nyingine ya manifestation is “making your dream come true”, kufanya ndoto yako kuwa kweli.
Msingi mkuu wa manifestation ni nia na imani ya kujiamini kuwa wewe una powers ndani yako na una uwezo wa kufanikiwa, kwa kutumia mawazo yako kutia nia ya kuzifungulia hizo powers zilizomo ndani yako zikuletee mafanikio ya kupata kitu unachokitaka
Manifestation ni kutumia the power of mind, through positive thinking to open the energy stored in your subconscious mind, ikupe chochote unachokitaka. Watu wote wenye mafanikio wanatumia manifestation kwa kujua au kutokujua, ila siri kuu ya kwanza ya mafanikio, ni kuwa na ndoto, wazo, nia, kisha kuifanyia kazi hiyo ndoto.
Kuna wengi wana mawazo mazuri tuu ya maendeleo, na kusema nikiwa mkubwa nataka kuwa pilot, daktari, polisi, tajiri, lakini wazo hilo linaishia hewani, kwasababu haulifanyii kazi. Ili uweze kufanikiwa, ni lazima ufanyie kazi ndoto yako. Kuota tuu ndoto ya unataka kuwa tajiri, halafu hauifanyii kazi hiyo ndoto, inaitwa ni “day dreaming”, yaani yaani kuota ndoto ya mchana, kama ile hadithi ya ndoto ya Alinacha kwenye hadithi za Alfu Lela Ulela.
Kwenye Nguzo 7 za Manifestation, Nguzo ya kwanza ni Asili ya Manifestation
Kuna wengi wanadhani manifestations ni jambo jipya, hapana, manifestation ni jambo la enzi na enzi toka enzi za Masiha, alifundisha “ombeni mtapewa", "tafuteni mtapata", "bisheni hodi, mtafunguliwa”, na akasema “hata ukiwa na imani ndogo kama chembe ya haradali, unaweza kuiambia milima iondoke na milima ikahama”.
Kitu kinachoitwa meditation, tafakuri jadidi au tahajudi, ni manifestation. Wakati wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Waislamu, wanatakiwa kunuizia kufunga kila siku kuwa kesho nitafunga. Kitendo cha kunuizia ni manifestation. Wakatoliki hufanya sala za novena ni manifestation. Sala za kujirudia rudia kama rozari ni manifestation, sala za tasbihi ni manifestations.
Mara nyingi enzi za ujana maji ya moto, mvulana akimuona msichana, akampenda, akadhamiria kumpata, hufanya juhudi mbalimbali, ili kumpata, hivyo kutumia manifestation bila kujijua, ila mwisho wa siku, hufanikiwa.
Ili kupata mafanikio kwenye jambo lolote, lazima kwanza, uwe na ndoto ya kufanikiwa, ndoto hiyo ni kuwa na mawazo chanya, kwa kizungu, “positive thinking”. Mawazo chanya haya yanakuwa yana nguvu ndani yake, inayoitwa “the power of positive thinking”. Kisha uweke nia thabiti na ya dhati ya kufanikiwa, tatu ufanye juhudi na bidii kulifanikisha hilo jambo lako. Ile power au nguvu iliyomo ndani yako, itafungua milango ya mafanikio, na utafanikiwa.
Kuna watu wanadhani kuna watu wana bahati tuu ya kufanikiwa na wengine wana laana ya umasikini, hapana!, Mungu alituumba binadamu wote tufanikiwe, ila kuna kanuni za mafanikio, ukizifuata na kuzipatia, ni lazima utafanikiwa.
Wiki itajayo nitakuletea nguzo ya pili ya manifestation yenye sheria 12 za mafanikio kupitia manifestation ambazo ukizifuata kikamilifu, utafanikiwa.
Paskali
No ile sio manifestation, ile ni uwezo wa kusikia sauti kutoka ndani yako, inakuambia kitu fulani, bila kukupa sababu.Na ile voices from within yako huwa ni manifestation yako? Au huwa unaambiwa na mtu fulani