Nguzo 7 za Mafanikio Kupitia Manifestation, Nguzo Kwanza ni Kuijua Asili ya Manifestation, Kuwa na Ndoto, Kutia Nia, Kuamini, Kuthubutu, na Kutenda

Ni kweli ni muhimu Kushukuru kwa kukubaliana na hali halisi alafu ku move on, lakini sio kufurahia mabaya na kuchukulia poa.
 
Mafanikio ni Nini ?
 
Hizi mada Huwa nazikubali ila shida Bro Mayalla Huwa hammalizi code mnaenda Halaf mnatuacha njia ya panda

Fungua tu code zote tupate kila kitu 🙏🙏

Nipo seat ya mbele kusubiri nondo zijazo Big up Sana Kwa bandiko zuri
 
swali gumu kulijibu …
Huenda ungejibu hili.....

Usingesema haya..., Sababu technically kufanikiwa ni kufanikisha kile ambacho umekianza kwahio kama motive ni monetary basi kwenye jamii inayocheza rafu wewe kufanya fair ni vigumu kupata hizo material things..., lakini kama wewe ulichokianza ni kusaidia jamii yako basi hautafanikiwa kama ukiwaibia na kupata pesa wakati wao wanadumaa kwa kufanya hivyo utakuwa haijafanikisha ustawi wao bali umezidi kuwadidimiza...
 
Kilichoandikwa humu ndo ukweli mtupu. Mungu yuko ndani yetu na kupitia "postive thinking" ambayo mimi huwa naitafsiri kama "kuamini kupitia wewe/kujiamini na kujiamlia ufanye nini ili upate nini" ndo humuwezesha mtu kufanikiwa

Kitu kingine ambacho nakiona niku "focus" na unachoamini wewe wala sio mtu mwingine.

Hizi dini zipo na kwa asilimia kubwa sasa hivi zinatumiwa na wachache kwa maslahi yao binafsi. Jamii iliyojengwa kwa kumfanya mtu ajiamini yeye mwenyewe huwa inafanikiwa sana kuliko jamii iliyojengwa kwa kuamini miujiza na hofu ya kutoweza

Siku moja nilihudhuria ibada mahala fulani kanisani alikuwepo mgeni kutoka ulaya (Mzungu) ambaye naye alikuwa kiongozi wa dini. Katika salamu zake alishindwa kuficha mshangao wake kwa kuona kundi kubwa sana la vijana kanisani. Alishangaa sana na kusema kwao siku hizi wanaojaa kanisani ni watu wazima ambao sio "working age". Alisifia na kuwapongeza viongozi kwa kuwahamasisha vijana kuja kanisani. Waumini walishangilia kwa makofi na vigelegele sana.

Kwa upande wangu nilitikisa kichwa kuwashangaa waumini wenzangu walifurahia kitu gani? Afrika dini imeletwa na wazungu na ukisoma historia vizuri dini iliambatana na ukoloni na hakuna mahali wamisionari walioleta dini Afrika walikemea ukoloni au kujitenga nao. Kauli na mshangao wake nilielewa tofauti kabisa. Nilichokielewa nakijua Mimi mwenyewe acha nibaki nacho tu

Tuwafundishe watoto wetu kujiamini na kufanya vile wanavyoviwaza kwasababu mawazo mazuri yote ndo roho mtakatifu mwenyewe huyo hakuna Mungu mwingine zaidi ya kitu chema unachokiwaza moyoni mwako! Mungu alitupulizia pumzi ya uhai yaani roho na Mungu ni roho kwa hiyo roho hiyo ipo ndani yako.

Wakristu tunaamini tulivuviwa roho mtakatifu anayekaa ndani yetu siku zote, sasa kwanini tunahangaika kumtafuta sehemu nyingine wakati tuko naye ndani yetu??

Unajikuta kabisa unapanga jambo jema la maendeleo kwamba nitafanya hiki na hiki na hiki, halafu from no where unapuuzia kufanyia kazi kisha unakaa unaanza kuilaumu serikali, wazazi wako au kwenda kukesha makanisani ushushiwe miujiza, no way!

Muujiza unao wewe na unaweza kufanikiwa kwa kufanya kilichoko ndani ya mawazo yako

TAHADHARI: Hata sheteni nae ni roho vile vile hivyo zingatia mawazo chanya ambayo ni halali na si haramu
 
Na ile voices from within yako huwa ni manifestation yako? Au huwa unaambiwa na mtu fulani
 
Asante kaka kwa kutupa elimu adimu sana
 
Na ile voices from within yako huwa ni manifestation yako? Au huwa unaambiwa na mtu fulani
No ile sio manifestation, ile ni uwezo wa kusikia sauti kutoka ndani yako, inakuambia kitu fulani, bila kukupa sababu.

Sauti hiyo ni kutoka kwake YEYE aliye ndani yako, most of the times, huwa kweli. Hii ni baadhi ya mifano
- Voices from within: Nimesikia sauti, Dr. Tulia Ackson ndiye Spika ajaye! Sauti hiyo imenieleza Ndugai, japo atatamani aendelee lakini...

- Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani

- "Ombeni Mtapewa", "Tafuteni Mtapata", "Bisheni Hodi Mtafunguliwa" Je, Wajua Kuna "Kauli" na "Kauli Umba" Ambazo Huumba? Shuhudia

P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…