Nguzo 7 za Mafanikio Kupitia Manifestation, Nguzo Kwanza ni Kuijua Asili ya Manifestation, Kuwa na Ndoto, Kutia Nia, Kuamini, Kuthubutu, na Kutenda

Nguzo 7 za Mafanikio Kupitia Manifestation, Nguzo Kwanza ni Kuijua Asili ya Manifestation, Kuwa na Ndoto, Kutia Nia, Kuamini, Kuthubutu, na Kutenda

Wanabodi,
Nipashe ya Leo 16/06/2024

View attachment 3018955
NGUZO 7 ZA MANISTATION
Hili ni bandiko mwendelezo wa wiki iliyopita. Kama hukulisoma bandiko la kwanza, anzia hapa Siri ya Mafanikio Kupitia Manifestation -1: Manifestation ni Nini?

Kwa wasomaji wapya, wiki iliyopita niliintruduce topic ya kitu kinachoitwa manifestation, kwa lugha rahisi ni kuweka nia na kudhamiria kwa dhati kufanikiwa, kwa kutumia nguvu za nia, zilizomo ndani yako. Nikataja manifestations ina nguzo kuu 7.
  1. Foundation: Msingi wa Manifestation
  2. Laws: Sheria za Manifestation
  3. Vibrations:Mitetemo ya Manifestation
  4. Intention: Kuweka Nia
  5. Visualization: Kuona kwa jicho la ndani
  6. Affirmations: Kutumia Imani Chanya ya Kufanikiwa
  7. Process: Utekelezaji wa Manifestation.
Nguzo kuu ya kwanza ni Foundation: Msingi mkuu wa Manifestation ni nia na imani ya kufanikiwa.

Kuna makundi makuu 5 ya watu waliofanikiwa.

1. The Inheritors: hawa ni watu waliozaliwa kwenye familia tajiri, wafalme na matajiri, na viongozi, mtoto wa familia hii anazaliwa na kujikuta amerithi utajiri, hata kama kichwani ni zero, huyu atahesabika amefanikiwa.

2. The Best Brains: Hawa ni watu wenye akili nzuri, wasomi, wataajiriwa kazi nzuri, na kulipwa mishahara, hivyo kupata maisha ya mafanikio, kundi hili ni la waajiriwa.

3. The Best Talent: Hili ni kundi la watu wenye vipaji, wanamuziki, wasanii, waigizaji, wacheza mpira, au watu wenye vipaji vyovyote vinavyowaletea maisha mazuri, wakiwemo waandishi wa habari, watangazaji, etc. Mwanamuziki Michael Jackson, hakusoma hata darasa moja!, huyu Daimond Platnum wetu, Hamonise ni darasa la saba tuu lakini wamefanikiwa kutokana na vipaji.

4. The Hard Workers: Wafanyakazi kwa bidii, hawa ni working class, ukifanyakazi kwa bidii, utafanikiwa, hili ni kundi la wanaofanikiwa kwa kutumia nguvu zao, “mtaji wa masikini ni nguvu zake”.

5. Fixers: Hili ni kundi la mwisho la wapiga domo!, humu ndio kuna wanasiasa, wanaweza wasiwe best brains, hawana talent yoyote, sio hard workers, lakini wanafanikiwa kwa kupiga deals, fix na kupiga domo.

Makundi yote hayo yanafanikiwa kwa kufanya manifestation kwa kujua au bila kujua.

Lugha nyingine ya manifestation is “making your dream come true”, kufanya ndoto yako kuwa kweli.

Msingi mkuu wa manifestation ni nia na imani ya kujiamini kuwa wewe una powers ndani yako na una uwezo wa kufanikiwa, kwa kutumia mawazo yako kutia nia ya kuzifungulia hizo powers zilizomo ndani yako zikuletee mafanikio ya kupata kitu unachokitaka

Manifestation ni kutumia the power of mind, through positive thinking to open the energy stored in your subconscious mind, ikupe chochote unachokitaka. Watu wote wenye mafanikio wanatumia manifestation kwa kujua au kutokujua, ila siri kuu ya kwanza ya mafanikio, ni kuwa na ndoto, wazo, nia, kisha kuifanyia kazi hiyo ndoto.

Kuna wengi wana mawazo mazuri tuu ya maendeleo, na kusema nikiwa mkubwa nataka kuwa pilot, daktari, polisi, tajiri, lakini wazo hilo linaishia hewani, kwasababu haulifanyii kazi. Ili uweze kufanikiwa, ni lazima ufanyie kazi ndoto yako. Kuota tuu ndoto ya unataka kuwa tajiri, halafu hauifanyii kazi hiyo ndoto, inaitwa ni “day dreaming”, yaani yaani kuota ndoto ya mchana, kama ile hadithi ya ndoto ya Alinacha kwenye hadithi za Alfu Lela Ulela.

Kwenye Nguzo 7 za Manifestation, Nguzo ya kwanza ni Asili ya Manifestation
Kuna wengi wanadhani manifestations ni jambo jipya, hapana, manifestation ni jambo la enzi na enzi toka enzi za Masiha, alifundisha “ombeni mtapewa", "tafuteni mtapata", "bisheni hodi, mtafunguliwa”, na akasema “hata ukiwa na imani ndogo kama chembe ya haradali, unaweza kuiambia milima iondoke na milima ikahama”.

Kitu kinachoitwa meditation, tafakuri jadidi au tahajudi, ni manifestation. Wakati wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Waislamu, wanatakiwa kunuizia kufunga kila siku kuwa kesho nitafunga. Kitendo cha kunuizia ni manifestation. Wakatoliki hufanya sala za novena ni manifestation. Sala za kujirudia rudia kama rozari ni manifestation, sala za tasbihi ni manifestations.

Mara nyingi enzi za ujana maji ya moto, mvulana akimuona msichana, akampenda, akadhamiria kumpata, hufanya juhudi mbalimbali, ili kumpata, hivyo kutumia manifestation bila kujijua, ila mwisho wa siku, hufanikiwa.

Ili kupata mafanikio kwenye jambo lolote, lazima kwanza, uwe na ndoto ya kufanikiwa, ndoto hiyo ni kuwa na mawazo chanya, kwa kizungu, “positive thinking”. Mawazo chanya haya yanakuwa yana nguvu ndani yake, inayoitwa “the power of positive thinking”. Kisha uweke nia thabiti na ya dhati ya kufanikiwa, tatu ufanye juhudi na bidii kulifanikisha hilo jambo lako. Ile power au nguvu iliyomo ndani yako, itafungua milango ya mafanikio, na utafanikiwa.

Kuna watu wanadhani kuna watu wana bahati tuu ya kufanikiwa na wengine wana laana ya umasikini, hapana!, Mungu alituumba binadamu wote tufanikiwe, ila kuna kanuni za mafanikio, ukizifuata na kuzipatia, ni lazima utafanikiwa.

Wiki itajayo nitakuletea nguzo ya pili ya manifestation yenye sheria 12 za mafanikio kupitia manifestation ambazo ukizifuata kikamilifu, utafanikiwa.

Paskali
Hili lingekuwa limeandikwa na bhakresa au dangote au Elon au Jeff ningeamini.
 
Ila pia mimi naamini bidii ndio huonyesha ndani yako ni kweli una imani na unachokiamini, nayo pia ni kanuni ya kimaumbile , auwezi kuwa una amini utanunua gari then unajenga nyumba unaweka geti la kupita baiskel apo imani itakua imepishana na matendo na tayari upo negative.


Hakika pia kuhurusu muda au kuupa muda nafasi .

Ukisema unataka great things lazima uupe muda nafasi

Sometimes mediocre life inasababishwa na haraka haraka Mimi nimejufunza Ku-hustle kupata great things na kuupa muda nafasi .
 
Hongera kwa thread nzuri kaka mkubwa.
Mimi binafsi nna swali; kama mtu hujioni kwenye halo makurdi ma5 utakua wait???
- Big brain kama hajasoma ikamfanya aajiriwe atahualpa wait? Ama ndio kufeli kwa manifestation
 
Manifestation ni mchakato wa kutumia mawazo hisia na vitendo kufanya kitu unachokitaka.

Law of attraction, ni sheria ya mvutano .

Japo vinauhusiano ila tafsiri inakua kuwa tofauti ni sawa na useme shule na kusoma.
Sawa kabisa, pia nilifahamu hivyo ni vitu vilivyo sambamba. Hii ni elimu muhimu ambayo kila mtu anapaswa kuifahamu.
 
Hakika pia kuhurusu muda au kuupa muda nafasi .

Ukisema unataka great things lazima uupe muda nafasi

Sometimes mediocre life inasababishwa na haraka haraka Mimi nimejufunza Ku-hustle kupata great things na kuupa muda nafasi .
Jamaa yetu anapinga kufanya manifestation wakati hata yesu aliwafundisha kutumia kanuni za kimaumbile kumanifest vitu , ndio maana yule bwana aliwambia mna masikio ila hamsikii mna macho ila hawaoni.
 
Hongera kwa thread nzuri kaka mkubwa.
Mimi binafsi nna swali; kama mtu hujioni kwenye halo makurdi ma5 utakua wait???
- Big brain kama hajasoma ikamfanya aajiriwe atahualpa wait? Ama ndio kufeli kwa manifestation
Nakujibu apo kufeli kwa manifestation , huwa inategemea mawazo hisia na vitendo vya mhusika.
 
Jamaa yetu anapinga kufanya manifestation wakati hata yesu aliwafundisha kutumia kanuni za kimaumbile kumanifest vitu , ndio maana yule bwana aliwambia mna masikio ila hamsikii mna macho ila hawaoni.
Mkuu sijapinga, ila napinga kufanya kwa njia tofauti na ya Mungu, unapo zungumza kuhusu Yesu, hapo tayari umegusa eneo ambalo Mungu anahusika.
 
Sawa mkuu, Law nyingine ambayo ni muhimu ni Law of Polarity/Opposites.

Hii nayo unaielewa vipi?

Hiyo sijaipitia Sana mkuu

Mimi natumia hii

Law of karma /causes and effect
Law of attraction

Hizi mbili ndo huwa natumia Sana kupush maisha yangu .

Pia kuna law of Gratitude -hii nadhani nikipande kimemegwa kutoka Katika law of attraction na law of karma.
 
Hiyo sijaipitia Sana mkuu

Mimi natumia hii

Law of karma /causes and effect
Law of attraction

Hizi mbili ndo huwa natumia Sana kupush maisha yangu .

Pia kuna law of Gratitude -hii nadhani nikipande kimemegwa kutoka Katika law of attraction na law of karma.
IMG_20221113_221117.jpg
 
Sawa kabisa, pia nilifahamu hivyo ni vitu vilivyo sambamba. Hii ni elimu muhimu ambayo kila mtu anapaswa kuifahamu.
Kufahamu na kuto kufahamu hakufanyi kuwa kanuni hizi zitende kazi au zisitende ,kanuni zipo tu , ila ukizifahamu utakua aware na kila kinachotokea kwenye maisha , hakijasababishwa na mtu bali ni wewe mwenyewe.
 
Nimekupata hii nadhani ndo ile huwa tunafanya gratitude mfano unapopatwa na matatizo ,mikosi , hasira, kuibiwa ,kuachwa unanfanya gratitude ili kuondoa hisia mbaya ili hisia nzuri zije.
Gratitude ni Law inayohusu shukurani, kushukuru na kupendezwa na yale uliyo nayo.

Hiyo Polarity ni kwamba kila kitu kina Opposite side, yani mazuri na mabaya. Mfano upendo na chuki, maumivu na furaha, kukosa na kupata
 
Back
Top Bottom