Ngwair alikuwa na kipi cha pekee kwa watu kumsifia sana, au ni kufunika kifo chake cha aibu?

Huna akili nmesoma Benjamin mkapa chimbo napiga kariakoo na karume utaniambia umjini upi nisio ujua?
Watoto wa Benjamini mkapa hatunaga lugha mbaya kama zako mzee. Mtu akienda opposite na mawazo yako no need ya kutoa shombo mdogo angu
 
Watoto wa Benjamini mkapa hatunaga lugha mbaya kama zako mzee. Mtu akienda opposite na mawazo yako no need ya kutoa shombo mdogo angu
Ni mimi sasa nipo ww labda ulikuwa wale mashoga mabonge la olevel
 
Ipo siku mtu ataleta mada kwamba Marijan Rajab hakua na maajabu, kumbe yeye mleta uzi ndio hakuwepo enzi za Marijani..😜
 
Sasa nakumbuka 2007 Albert Mangwair alikujaga Benjamin mkapa aliletwa na 5 selekt aka perform Nipeni deal masela kipindi hiko ni hit kwelikweli. Alisepa na kijiji mbaya.. FK21
 
Mnaomsifia ngwair mna hoja zipi,?
Ni moja kati ya freestyler bora kuwah kutokea Tanzania.. ni mwanzilishi wa rap yenye ladha tamu sana Tz.. ikawa inaskizwa sana na jinsi zote KE na ME. Ngwair aki flow una feel heaven. Oya weee Albert alikua mtu na nusu
 
NGWAIR HAKUA MSANII WA KAWAIDA LABDA KAMA WEWE SIO MPENZI WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA.

Sijajua Una umri gani huenda umemjua Ngwair baada ya kifo chake au pengine umeanza kushabikia bongo fleva enzi hizi za kina Zuchu na sukari yake.

Lakini Kwa mdau wa muziki wa Bongo fleva Ngwair ni miongoni ya wasanii Bora waliotamba ndani na nje ya mipaka ya Tanzania enzi za uhai wake na alikua anakinukisha kinoma.

Kusema kwamba alivuma baada ya kifo chake huu ni uongo wa Hali ya juu kwani jamaa alitamba Sana na Ngoma zake zilikua zinashika namba moja kwenye top ten ya vituo mbalimbali vya redio na T.v sasa sijui pote huko walikua wanampendelea Kwa kua walijua atakufa [emoji16][emoji1787]

Umeuliza eti Ngwair alikua na uspesho gani Hadi apewe Sana promo hata baada ya kufa..! ok kabla sijaandika uspesho alikua nao, hebu jiulize we wameshakufa wasanii wangapi hapa Bongo, na kwanini Ngwair ndio awe spesho? nazani kuna majibu yameshajijenga kichwani mwako.

Hizi na baadhi ya sifa "Spesho" alizokua nazo Ngwair.

1. KUIMBA NA KURAP
- Ngwair alikua na kipaji cha kipekee Sana kwani alikua na uwezo wa kuimba na kurap Kwa ubora wa hali ya juu Sana. mfano kwenye Ngoma ya She got a gwan na Nipo ndani ya club, Humo jamaa aliimba vibaya mna usingeamini ni msanii anaeweza kufanya rap.

2. TAJIRI WA MISEMO
Ngoma za Ngwair zilikua zinaacha MISEMO mingi Sana tu kitaani mfano kwenye Ngoma yake ya mikasi aliyoimba na mchizi mox ndio iliyopelekea neno "mikasi" kuanza kutumika kitaa kumaanisha sex. na Misemo mingine ni kama "cha Arusha" "kulipuka" na mingine

3. MKALI WA HIT SONGS
Kwa wasio mjua Ngwair ingia Google or boomplay sikiliza hizi Ngoma.
CNN ft Fid q

Mapenzi gani ft lady jaydee

Aminia feat Inspecta Haruni, FA

Birthday N'GE ft Mwasiti, TID & Mez B

Speed 120 ft Chid Beenz

TZ Hustler ft J-Son

She performs ft TID

Mafia ft. JAY MO

Bado nimo

Zawadi

Salamu

Mademu wangu

Mida mibovu

Kimya Kimya

Nipe deal

Singida Dodoma ft Dully Sykes

Napokea simu

Weekend

Sikiliza

Wife

Tupo juu ft Squeezer & Steve RNB

Ghetto langu

Clubbin'

She got a Gwan

4. INSPIRATIONAL RAPPER
Mistari mingi ya Ngwair imerudiwa kuimbwa na wasanii wengine..
mfano Young Lunya kuna mstari aliimba kwenye serikali kuu ya mizuka "niguse nikuchane chane na kiwembe" huu ni mstari wa Ngwair kwenye Ngoma ya Demu Wangu ft Mchizi mox.. lakini pia kwenye Ngoma ya "simu zinaita" Young Lunya kaikopi vilevile kama Ngwair alivoimba kwenye Ngoma ya "napokea simu"
pia msanii p the MC karudia baadhi ya Ngoma za Ngwair kuonesha kua jamaa alikua mwamba baadhi ya hizo Ngoma ni "weekend", "mademu zangu" na "ghetto langu".

5. ALIKUA MBUNIFU SANA
Wakati ugonjwa wa ukimwi umeshika Kasi wasanii wengi walijaribu kutunga nyimbo mbalimbali ili kuionya jamii. Wengi wao walikua wanaenda straight kuuelezea ukimwi but Ngwair alikua tofauti Sana yeye alifanya Kwa staili nyingine.
mfano kwenye Ngoma ya bado nimo, alijivika balaa la Ngoma na kuelezea watu kua bado ukimwi upo na unawatafuna kimyakimya.. pia kwenye Ngoma ya zawadi alielezea ukimwi Kwa mtindo wa Stori, hapa alielezea jinsi alivompa dada mmoja (wanaodanga) zawadi nyingi kama gari,cheni na nyumba ya kifahari lakini kumbe kuna zawadi nyingine spesho alimpa kimyakimya ambayo ni HIV... na hata sasa ni wengi tu wanapewa hiyo Zawadi.

6. MUZIKI WAKE ULIKUA VIWANGO VYA JUU
Ngwair pia aliwahi kushinda tuzo ya Kilimanjaro Music Awards kama mwana Hip Hop Bora wa mwaka 2005.
kipindi hicho tuzo zikiwa za Moto mno na zenye heshima kubwa.

nimechoka kutype Ila jua Tu Ngwair hakua MSANII wakaida kama unavozani ndo maana hata Legend wa Hip-hop Tanzania Farid Kubanda maarufu kama Fid Q kwenye Ngoma ya "Sumu" alionesha ni jinsi gani alikua anamkubali Sana Ngwair kuna mistari anajisifu kua na kipaji kama cha Ngwair, anasema hivi..

"Aliyeniumba alinipa mdomo hivo n′na haki kuongea
Hii bahati meotea, safi kamwe siachi kui-share
Hamtaki niwe fair, trust me man huwa happy nki-care
Naona watachosema mshkaji uko smart upstairs
Usiache kuongea, usiache we ni incharge huna spare
KIPAJI ka' NGWAIR, mapaji ka′ bahati aliowagea
Flag pepea, hitaji zaidi ya maji na mmea
Ilikuwaje wa muache hadi mshkaji ulaji wa drugs ukamzoea"

Hapo anamaanisha tukimzungumzia Ngwair tunazumgumzia kitu kimoja tu KIPAJI...
Hicho Ndo kinafanya atajwe tajwe Sana Hadi we uhisi anapewa promo.
 
Goma jingine alilo freestyle ni lile kaimba na Jay Mo linaitwa KIMYA KIMYA, ile ngoma Majani aliitendea haki.


Kiswahili ni lugha ya ajabuajabu ila kwenye rap Ngwair alikifanya kama kiingereza tu, maneno anayatamaka smoothly bila nguvu.
Braza Ngwair alikua ana ladha. Jamaa anapata wap nguvu ya kudiss uwezo wa mchizi aiseeee
 
Alikuwa mbele ya muda, watu kama wewe hamuwezi kumuelewa maana bado mnaishi zama za ujima.
 
Wakati yupo hai alikuwa boya tu
No alikua mkali mana aliachia hits kali sana. Sema kifo kilimuongezea ukubwa kutokana pia na msiba wake ulivyo hudhuriwa na watu wengi
 
Umeongizwa na chuki, ubinafsi na kutokujua mziki...kifupi unaumizwa na ukubwa na umaarufu wa marehemu!
Nitajie mwanamuziki aliyefanya muziki kipindi kile cha Ngwair (muziki aina ya aliofanya Ngwair) ambaye unaweza kumuweka daraja moja (kiuwezo) na Ngwair.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…