Ngwair alikuwa na kipi cha pekee kwa watu kumsifia sana, au ni kufunika kifo chake cha aibu?

Ngwair alikuwa na kipi cha pekee kwa watu kumsifia sana, au ni kufunika kifo chake cha aibu?

NGWAIR HAKUA MSANII WA KAWAIDA LABDA KAMA WEWE SIO MPENZI WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA.

Sijajua Una umri gani huenda umemjua Ngwair baada ya kifo chake au pengine umeanza kushabikia bongo fleva enzi hizi za kina Zuchu na sukari yake.

Lakini Kwa mdau wa muziki wa Bongo fleva Ngwair ni miongoni ya wasanii Bora waliotamba ndani na nje ya mipaka ya Tanzania enzi za uhai wake na alikua anakinukisha kinoma.

Kusema kwamba alivuma baada ya kifo chake huu ni uongo wa Hali ya juu kwani jamaa alitamba Sana na Ngoma zake zilikua zinashika namba moja kwenye top ten ya vituo mbalimbali vya redio na T.v sasa sijui pote huko walikua wanampendelea Kwa kua walijua atakufa [emoji16][emoji1787]

Umeuliza eti Ngwair alikua na uspesho gani Hadi apewe Sana promo hata baada ya kufa..! ok kabla sijaandika uspesho alikua nao, hebu jiulize we wameshakufa wasanii wangapi hapa Bongo, na kwanini Ngwair ndio awe spesho? nazani kuna majibu yameshajijenga kichwani mwako.

Hizi na baadhi ya sifa "Spesho" alizokua nazo Ngwair.

1. KUIMBA NA KURAP
- Ngwair alikua na kipaji cha kipekee Sana kwani alikua na uwezo wa kuimba na kurap Kwa ubora wa hali ya juu Sana. mfano kwenye Ngoma ya She got a gwan na Nipo ndani ya club, Humo jamaa aliimba vibaya mna usingeamini ni msanii anaeweza kufanya rap.

2. TAJIRI WA MISEMO
Ngoma za Ngwair zilikua zinaacha MISEMO mingi Sana tu kitaani mfano kwenye Ngoma yake ya mikasi aliyoimba na mchizi mox ndio iliyopelekea neno "mikasi" kuanza kutumika kitaa kumaanisha sex. na Misemo mingine ni kama "cha Arusha" "kulipuka" na mingine

3. MKALI WA HIT SONGS
Kwa wasio mjua Ngwair ingia Google or boomplay sikiliza hizi Ngoma.
CNN ft Fid q

Mapenzi gani ft lady jaydee

Aminia feat Inspecta Haruni, FA

Birthday N'GE ft Mwasiti, TID & Mez B

Speed 120 ft Chid Beenz

TZ Hustler ft J-Son

She performs ft TID

Mafia ft. JAY MO

Bado nimo

Zawadi

Salamu

Mademu wangu

Mida mibovu

Kimya Kimya

Nipe deal

Singida Dodoma ft Dully Sykes

Napokea simu

Weekend

Sikiliza

Wife

Tupo juu ft Squeezer & Steve RNB

Ghetto langu

Clubbin'

She got a Gwan

4. INSPIRATIONAL RAPPER
Mistari mingi ya Ngwair imerudiwa kuimbwa na wasanii wengine..
mfano Young Lunya kuna mstari aliimba kwenye serikali kuu ya mizuka "niguse nikuchane chane na kiwembe" huu ni mstari wa Ngwair kwenye Ngoma ya Demu Wangu ft Mchizi mox.. lakini pia kwenye Ngoma ya "simu zinaita" Young Lunya kaikopi vilevile kama Ngwair alivoimba kwenye Ngoma ya "napokea simu"
pia msanii p the MC karudia baadhi ya Ngoma za Ngwair kuonesha kua jamaa alikua mwamba baadhi ya hizo Ngoma ni "weekend", "mademu zangu" na "ghetto langu".

5. ALIKUA MBUNIFU SANA
Wakati ugonjwa wa ukimwi umeshika Kasi wasanii wengi walijaribu kutunga nyimbo mbalimbali ili kuionya jamii. Wengi wao walikua wanaenda straight kuuelezea ukimwi but Ngwair alikua tofauti Sana yeye alifanya Kwa staili nyingine.
mfano kwenye Ngoma ya bado nimo, alijivika balaa la Ngoma na kuelezea watu kua bado ukimwi upo na unawatafuna kimyakimya.. pia kwenye Ngoma ya zawadi alielezea ukimwi Kwa mtindo wa Stori, hapa alielezea jinsi alivompa dada mmoja (wanaodanga) zawadi nyingi kama gari,cheni na nyumba ya kifahari lakini kumbe kuna zawadi nyingine spesho alimpa kimyakimya ambayo ni HIV... na hata sasa ni wengi tu wanapewa hiyo Zawadi.

6. MUZIKI WAKE ULIKUA VIWANGO VYA JUU
Ngwair pia aliwahi kushinda tuzo ya Kilimanjaro Music Awards kama mwana Hip Hop Bora wa mwaka 2005.
kipindi hicho tuzo zikiwa za Moto mno na zenye heshima kubwa.

nimechoka kutype Ila jua Tu Ngwair hakua MSANII wakaida kama unavozani ndo maana hata Legend wa Hip-hop Tanzania Farid Kubanda maarufu kama Fid Q kwenye Ngoma ya "Sumu" alionesha ni jinsi gani alikua anamkubali Sana Ngwair kuna mistari anajisifu kua na kipaji kama cha Ngwair, anasema hivi..

"Aliyeniumba alinipa mdomo hivo n′na haki kuongea
Hii bahati meotea, safi kamwe siachi kui-share
Hamtaki niwe fair, trust me man huwa happy nki-care
Naona watachosema mshkaji uko smart upstairs
Usiache kuongea, usiache we ni incharge huna spare
KIPAJI ka' NGWAIR, mapaji ka′ bahati aliowagea
Flag pepea, hitaji zaidi ya maji na mmea
Ilikuwaje wa muache hadi mshkaji ulaji wa drugs ukamzoea"

Hapo anamaanisha tukimzungumzia Ngwair tunazumgumzia kitu kimoja tu KIPAJI...
Hicho Ndo kinafanya atajwe tajwe Sana Hadi we uhisi anapewa promo.
Chief umemaliza vyote,hapo hujaweka featuring alizofanya cow-bama, huyu kipindi mabibo hostel inavuma alibadili ile nyimbo ya hotel ya cassid ikawa mabibo hostel kuna ile in da club ndio mnamfananisha na kenge gani wa kizazi hiki alivyosema akifa pengo halina spea alimaanisha..
 
Ngwea alikuwa na kipaji sana na ngoma zake kama Masikini wenzangu, Mapenzi gani ft Jide, AKA mimi na No beef ft TID aiseee basi tu jamaa alijua sana hata sasa kwa wasanii wa leo zipigwe ngoma za Ngwea na msanii yoyote wa kizazi hiki zipigiwe kura utapata jibu mkuu,# Pesa haipunguzi matatizo bali inaongeza so usikaribie meza kama huchangii unachomeza, daah. R.I.P Ngwea
 
Kwangu mm cjawahi kukaa nae wala kua rafiki yake. .but his music talk itself ni km Nature or prof. ..I don't know their life behind a scene ila kasikilize mziki wake. ."she got gwan" ni moja ya nyimbo zake kali...nyuma ya beat za Majani. .mnyonge mnyongeni lkn hakiyake mpeni
 
Mnapamba sana mavi maua wazee ngwair alikuwa na styles na swagger ila huo u GOAT hell no
Hizo styles na swaggs.. the guy Albert call him king of freestyle. He was the founder. Wakati tuna mu enjoy Albert we ulikua wap??? Mbona umekosa raha sana?!
 
Geto langu ......linawazingua maduuuu...... Ngwea nomaaaaa wala hapendelewi
 
"Kuna wengine kwa kifupi wameshapotea, umeambiawa usiyaguse maji km hauwezi kuogelea, wamebaki kutapatapa wameshiwa Cha kuongea, wamebaki kum diss ngwea,............."
Nakazia...!
 
"Kuna wengine kwa kifupi wameshapotea, umeambiawa usiyaguse maji km hauwezi kuogelea, wamebaki kutapatapa wameshiwa Cha kuongea, wamebaki kum diss ngwea,............."
Nakazia...!
Sasa ndiyo ujinga gani[emoji16]
 
Hizo styles na swaggs.. the guy Albert call him king of freestyle. He was the founder. Wakati tuna mu enjoy Albert we ulikua wap??? Mbona umekosa raha sana?!
Hakuna enjoyment yeyote labda kama mlikuwq mnavuta nae
 
Habari zenu wadau wa sanaa,

Mimi sipendi kuwa mnafiki, niko hapa, mwenye kutoa clarification aje. Je, msanii Ngwair alikuwa na kipi cha special kinachofanya asifiwe na kupewa promo kubwa na Clouds Media na wasanii baada ya kifo chake?

Maana imekuwa mkumbo sasa, kila mtu Ngwair hana mpinzani! Kwa lipi sasa? Mbona hata kukaza lyrics alikuwa hawezi, kidogo freestyle alijitahidi, ila mbona mnamsifia kuzidi uwezo?

Ttuacheni notion ya marehemu hasemwi vibaya, Magufuli daily anakaangwa tu!

Naombeni kuwasilisha.
personally naona yupo overrated sana.
 
Back
Top Bottom