Ngwair vs Jay Moe (AKA Mimi vs Ulimwengu ndio Mama)

tyc nakupa challenge,kasikilize na album ya Daz Baba-Elimu Dunia.

Kama utabahatika kusikiliza full album basi njoo tena.

Kwangu binafsi Daz naona haitokuja kutokea album kama ile,nyimbo kwa nyimbo,maudhui ya kila wimbo,uadishi,chorus na mpangilio wa ala zilizotumika.

Bahati mbaya sana kipindi kile Ruge alikua na biashara zake na MWANAFA,album bora akawa anachukua FA.

Kwangu naamini album hii ina madini mengi sana na ubora uliotukuka

 
NB-kazi nyingi sana na albums ambazo hadi leo zikitajwa kwa ubora,hutokosa mkono wa P-Funk Majani,kuanzia kwa kina Prof Jay,Fid,TID,JayMo,Nature,Solo Thang,Dull Sykes etc.

Jamaa kiwanda cha muziki anakidai,kakifanyia kazi sana!!
 
Nakubali hii ni Album kali sana, sema kila mtu na bahati yake. Feruzi alitoboa zaidi ya Daz Baba kwasababu ya umaarufu wa nyimbo kama 2 tu
 
Nakubali hii ni Album kali sana, sema kila mtu na bahati yake. Feruzi alitoboa zaidi ya Daz Baba kwasababu ya umaarufu wa nyimbo kama 2 tu
Hapana mkuu screpa si nyimbo mbili tu.
Album ya "Safari" ya Ferouz ilikuwa Ina ngoma Kali Sana,kiufupi
Bongo records kwa watu waliokuwa Label walikuwa wanatumia muda vizuri kwenye content na wakaleta ladha nzuri tu kwa audience.
Elimu Dunia pia ilikuwa nzuri japo haikuweza kupiku mauzo ya Safari
 
Nakubali hii ni Album kali sana, sema kila mtu na bahati yake. Feruzi alitoboa zaidi ya Daz Baba kwasababu ya umaarufu wa nyimbo kama 2 tu
Hakika Mkuu, album yake haikua ya kutisha sana na inasemekana Ferouz ndio alianza kumfanyia fitna Daz kwa P-Funk baada ya kuona jamaa ana mawe makali,jamaa akataka yeye ndio apewe kipaumbele na hadi ikafikia sehemu jamaa akatunga wimbo wa "kijana mteja kumdiss Daz.
 
Hizo ndizo nyimbo sasa achana na ushetwani wa "mwagia ndani, dera lako jipya chupi lako la zamani, nani kamwaga pombe yangu na kibamia"
Mola niokoe mimi ni dent au mjeshi
Shule za boarding bwana mizengwe haishi
Ukiongea kiswahili adhabu swahili speaker
Je huu ni uungwana hii si ni lugha ya taifa


Kweli muda unaruka
 
Proff J muoga sana. Kwenye wimbo wa Una aliogopa kumpa ngwair hata verse moja, alijua ngwair sio mtu mzuri.
 
Kuna jamaa alsema hamjui jay moe ila anashabikia hip pop..huyu tunamuweka kundi gan?
 
Proff J muoga sana. Kwenye wimbo wa Una aliogopa kumpa ngwair hata verse moja, alijua ngwair sio mtu mzuri.
Mpe heshima yake Profesa, huyo yuko sayari ya pekeyake hawezi hofia watoto wadogo
 
Honestly hizi album zina uzani sawa sawa kabisa. Zinalingana kila kitu aisee. Nimeishiwa maneno .
 
Aha! Aha! Jay Moe (Jay Moe)
Bongo Records (Bongo Records)
Maisha Ya Boarding (Aaah)
Ulimwengu ndo mama! (Aaah)! (Aaah)! (Aaah)!
UBETI 1
Maisha ya boarding noma, Jay Moe nimesoma,
Na ndo lipo nlipata neno Ulimwengu ndo mama,
Primary sikupass, sikuwa na nyota njema,
Ikabidi nikasome boarding kuziepuka lawama,
Mi n'navyoona maisha ya boarding yana raha na noma,
Ila wanafunzi wengine kwao hayakuwa salama,
Kama wewe Form One shida kibao utapata,
Kuna kuibiwa, kuna kuna adhabu, maisha kama vita
Siku za mwanzoni ni siku za kufanya tathmini,
Niliogopa sana mambo ya kupiga simu chooni,
Viongozi wenyewe wazamu, hawana akili timamu,
Bakora mtindo mmoja mpaka fulani atoke damu!
Hapo binamu sikugoma, kazi zao nilifanya
Ili nisiwe ukingoni mwa sakafu na mbio za panya,
Morning jioni niko job, me ni denti au mjeshi?
Shule za boarding bwana mizengwe haiishi,
Ukiongea Kiswahili adhabu "Swahili speaker"!
Kweli, huu ungwana? Hii si ni lugha ya taifa?
Mbona inakuwa adhabu? Mi sikusoma English Media,
Shule ya msingi Uswahilini, huko ni Swahili Media
KIITIKIO
Tunanyanyasikaa, faidikaa
Twatesekaa, maisha ya boarding,
Chakula shidaa, twahangaikaa
Taabikaa, maisha ya boarding X2
UBETI 2
Asubuhi nakwenda bwaloni nakuta uji,
Uji bila sukari ni mchemsho wa sembe na maji
Shule ina kantini kuna chai bila kushangaa
Itakubidi uweke iwe freshi ili usife njaa
Kwani mchana ni soo, kote kabichi na ugali
Wali mpaka siku ya sherehe na siku hiyo ni hatari
Waalimu fimbo mkononi kisa wali na nyama!
Hapo ndipo utauona ubora wa baba na mama
Teacher class anateach sum, nje watu wanapuff some,
Mtoto wa mama bora usome day bongo Dar es Salaam
Iramba hakuna tuition, Iramba hakuna fashion,
Kama unakwenda town hadi utegee gari ya Mission
Term inapoanza watu wako safi kama bosi
Sababu hakuna pombe hapo ni pamba misosi
Baada ya miezi miwili watu wamechoka ile mbaya
Wakianza kula ugali hali imezidi kuwa mbaya,
Wengine wana majiko mpaka pilau wanapika,
Ila teacher akishtuka basi na shule itakwisha!
Walioogopa mambo Shauritanga si mnakumbuka?
Walioogopa hata wasifanye jipu likajatubuka
KIITIKIO MARA 2
UBETI 3
Wengine wanafukuzwa shule kwa makosa tofauti,
Huyu hula bangi, huyu usiku alifumwa na binti
Yaani usiku mchana kasheshe, inahitaji uwe fiti
Ili usifukuzwe shule, ukifukuzwa itakuwa vipi?
Kama una dem subiri hadi shule kufungwa,
Sehem ni town tu, Dar es Salaam wanafugwa
Wanaojifanya wagonjwa mida ya break wanapona,
Ilimradi wazunguke wee kusaka waschana,
Baada ya break kwa bwenini story kila kitanda,
Wengine utaskia ooh Carolina ana mimba!
Na shule inakuwa chungu kwenye zamu za kwenda shamba,
Wajanja hawakwenda, wengi waliokwenda ni washamba
Watu hawaogi wiki labda iwe weekendi
Baridi kama Urusi maji bafuni hayapandi,
Watu umande kila siku, maisha ya boarding hayafai
Hata awe dada mkuu wakimwotea hakatai
Wengine wanakwenda wajiseti huku mpira hawachezi
Na vingine vingi mtu yeyote kumaliza hawezi
Ndo maana boarding zenye elimu ni za Seminari
Shule kama Iramba mwanao ni lazima atafeli!
KIITIKIO MARA 2
Maisha ya boarding bwana!
Bora mlosoma day
Maisha ya boarding siyo mchezo
Utafikiri kambi ya mafunzo
KIITIKIO
Tunanyanyasikaa, faidikaa
Twatesekaa, maisha ya boarding,
Chakula shidaa, twahangaikaa
Taabikaa, maisha ya boarding X2
 
KAMA UNATAKA DEM -JAY MOE FT Q CHILLAH
CHORUS
Kama unataka dem, sema wataka aweje aweje,
Kama ukienda bugie, ungependa atokeje tokeje?
Marashi itakuwaje? angenukiajee?
Na akiwa mtaani, ungependa atokejeee?
Kama unataka dem, sema wataka aweje aweje,
Kama ukienda bugie, ungependa atokeje tokeje?
Marashi itakuwaje? angenukiaajee?
Na akiwa mtaani, ungependa atokejeee?
VERSE 1
Ndiyo nataka dem lakini tuanzie Makumbusho,
Awe mfano fifi madada zangu wamuite wifi,
Siyo Mkinde siyo Leyla, mtaa wao miyayusho
Simtaki flani Amri Dave ndiyo leo na kesho,
Siogopei Fat Family full dhahiri watapeta,
Belinda na Mose wakirealize vipi watadata?
Jedida na Lidya wabaki vikono mkipita,
Sina habari na Naomy wala Salama vile walinitesa,
Ndo kisa cha kutompenda Coco wala Zeitun,
Mwambie Samira mtoe kachichi ni washkaji tu,
Rosillah, Mandu mapacha nisije nkachanganya,
Ni sawa na Esther na Suzzy wa Magorofa Bima,
Bora nitoke Makumbusho niende zangu Kinyama,
Kwenye watoto wa geti kali baba mama tajiri
Kama Miriam Masa nusu Bongo nusu Msomali,
Nakwenda kumpa dili Akhenaton nageuza gari,
Nkaendelee na Sinza, Mbezi hata Kunduchi,
Heri ntoe Sinza, Mbezi Shakilla hata Makunduchi,
Nadhani ushanielewa dem wangu atakuwaje takuwaje,
Wee njoo Makumbusho utamuona amevaaje mevaaje
CHORUS
VERSE 2
Sasa nakwenda kwenye majina na heshima mahususi,
Kama Phobia, Judithi Domini au kama uups!
Au sera zikimnasa Kibibi kuna ubaya?
Nadhani mamiss hawataniona tena mi mbaya
Ila awe mkweli, siyo mambo ya Miss California
Awe kama Sister Jay mweupe kama Eugenia,
Na maradhi niliyoyataja naomba msiwe na kinyongo,
Mi nafanya kuwapeni thamani ya juu ndani ya Bongo,
Kusema mtoto wa tajiri mi namchagua Regina,
Tukisema model ni Miriam Odemba au hapana,
Tukisema miss, Aminata Keita haina noma
I FM watakoma kwa muda wote ambao wanasoma,
Ila ataweza vipi kuimba RnB kama Stara?
Au ni sana Miss Color Bar wa leo kuwa msela
Nini gado kama Zeidin mrefu kama Bascilla,
Design Khadija mavazi akatoneshee kajara,
Nitahakikisha hakuna machozi kama Jay Dee
Sitosubira sema anakuja kama Sister P
Nadhani ushanielewa dem wangu atakuwaje takuwaje,
Kama ukija Bills utamuona amevaaje mevaaje
CHORUS
VERSE 3
Yoh nataka dem miguu mizuri kama Ray C
Macho kama Acy, alcoholic ka Sister V
Napenda dem awe sister dread kama Baby
Naogopa sana mpenda chapaa kama Dotty
Awe anapenda rap siyo bolingo kama Essy
Mchizi ka Nazizi ila bright kama Cecil
Mrefu siyo mfupi na nyama asiwe mwembamba
Hewani kama gesi kiuno kama Odemba,
Asiwe lady flani hajui kupiga pamba,
Avae kama Seven japo atoke bomba
Awe anajua kupika, awe anang'aa kama Sanka
Laini kama mafuta kwenye giza awe anawaka
Awe anang'ara, apoze zangu harara
Awe na sauti tamu kuliko ile ya Stara,
Siyo kauzi kama Nina bora mcheshi kama Norah
Ili nimpende sana waganga wasijenipora
Awe na ishi ama questions bila mamake Jipsy
Ili siku ikichacha tukakope hata chipsi
Maridadi, mvuto wa zamaradi
Apitapo maskani washkaji mpandwe midadi
Awe na uvundo ka zinduna, mjanja kama Munah
Awe na tabasam siyo kila siku ananuna,
Kama ntapata demu itakuwaje fikiria,
Lafudhi iwe tamu siyo kithethe ka Radiya
Hapo mimi ntadata kama Nature kwa Sonia
Hapo mimi ntadata kama Nature kwa Sonia
CHORUS
 

Humo nyimbo ni 4 tu:

1. Elimu Dunia
3. Namba 8
4. Nipe 5
10. Wife

Zilizobaki zote utopolo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…