Safi sana Screpa kwa kuanzisha huu mjadala
Kwenye ile thread kuhusu Ngwair ni mimi ndie nilichomekea kwa kumwambia mchangiaji mmoja kwamba kama anasema hajaona álbum bora zaidi ya AKA MIMI basi itakuwa hajaisikiliza álbum ya 'Ulimwengu ndio Mama' ya Juma Mohamed Mchopanga aka J Mo au Mo Teknik
Back in Mada,
Álbum zote nilishawahi kuzinunua na kuzisikiliza sana na sana tu kwasbb walikuwa moja ya artists niliokuwa nawakubali sana
Ubora wa Jmo ktk hii album:
Binafsi ubora wa Jmo nauona ktk uandishi mzuri wa mashairi, flowing styles, beats kali za Pfunk na matumizi mazuri ya lugha kiasi kwamba nyimbo zake zote za hio álbum unaweza kusikiliza hata na mzazi wako au mtu yoyote wa heshima na usifadhaishwe na hata neno moja lenye kukengeuka maadili
Udhaifu wake nauona ktk kutumia mtindo mmoja wa kurap karibu nyimbo zake zote na hana club bangers song hata moja ktk hii album
Albert Mangwea ( RIP) :
Kwenye hii álbum nakubali sana uwezo wa Ngwea ktk flowing styles ( namna anavyonata na beatz), vina mwanzo kati na mwisho hasa ktk ngoma za Mikasi, Gheto langu, Napokea simu nk,
beats zilizoenda Harvard University kutoka kwa Pfunk nafikiri ni moja ya artist aliyependelewa sana na Pfunk ktk beats labda kwasbb ya ule uswahiba wa kushibana na vile alikuwa chini ya management yake,
Ngwea ni bora sana pía ktk kubadilika kwenye nyimbo ana uwezo wa kurap, kuimba, kupiga back vocal nk kwa mfano nyimbo za Dakika moja na Bado Nimo utaona uwezo wa kuimba wa Albert.
Pia ana ngoma kadhaa ambazo ni club bangerz
Udhaifu ktk ngoma zake kwenye hii álbum kulinganisha na JMo ni uandishi wa songs zake nyingi sio za kusikilizwa na rika lote au Ukiwa na watu wa heshima maana Albert anapenda sana kutumia vijimaneno vya hapa na pale vyenye ukakasi ktk maadili kama ngoma ya Mikasi kuna sehemu demu anatoa sauti za miguno ya sex ( bahati nzuri miaka ile basata walikuwa kama joka la kibisa, hawaumi) [emoji3]
All in All hizi álbum mbili sio za kukosa kuacha kusikiliza hata kidogo na kwangu mimi naziona ni moja ya álbum bora kabisa za wasanii wetu kuwahi kuzisikiliza na hata kwenye ngoma zao walizoshirikiana zilikuwa hits haswaaa...!!!