Wachangiaje wengi humo wanafurahia mpango wa NHC kuendeleza hizi majumba. Hilo jambo ni jema sana na hata ni bora kwa wapangaji na wananchi wengine ambao wangepata nao eneo zuri.
Swala kubwa ipo katika utekelezaji. Huwezi kuwahamisha wapangaji wote hao kwa mpigo moja bila kuwa na planned transition.
Athari za hiyo unplanned mass layoff:
Watu kukosa ajira. Ikiwa kila mpangaji ana say watu 4 on average, watu wangapi wameathirika hapo?
Wafanyabiashara wengi hukopa kutegemea biashara yao, hizo mikopo watalipa vipi?
Itasababisha vacuum katika real estate market na kuja kuathiri hata wale waliopanga kwenye majengo yasiyo ya NHC. Wenye nyumba wengine watapandisha kodi maradufu.
Kupanda kwa kodi kutaleta bei za vitu kupanda na kusababisha inflation ambayo itaathiri watanzania wote.
Hao watu ni walipa kodi za serikali, unawafungia wote kwa mpigo watalipa nini?
Kuna wapangaji wana uwezo wa kuingia ubia na NHC, hao walipewa hiyo nafasi au zabuni za kukaribisha ilitangazwa lini?
Hivi sasa kuna presha kubwa katika infrastucture ya maji, umeme, usafi wa mazingira, mfumo wa maji machafu, barabara za kupita watu na magari. Hii itakuja kuharibu zaidi.
Wapangaji wa zamani hawajapewa first right of allocation za nyumba mpya, hivyo allocation mpya itakuwa ni RUSHWA tupu.
Naona serikali hapo imewafungulia NHC jini la kulitumia na wao wanachukua fursa hii kujinemesha bila ya kuwa na social and economic impact assessment na sensitivity analysis ya maamuzi yao.
Maamuzi ya bodi ya NHC kubariki hii program kama ilivyo, ni dhahiri imekuwa influenced na wawekezaji au wenyewe kupata tenda za hizo kazi, bahasha au rushwa za aina zingine.
Naomba serikali iingilie hii swala na kuhakikisha inafanyika kwa hali ambayo haiathiri wananchi wake. Tunataka maendeleo lakini siyo kwa staili hiyo.