NHC yatelekeza miradi ya mabilioni wilayani Chato

NHC yatelekeza miradi ya mabilioni wilayani Chato

Afadhali...

Tumechoka na viwimbo vya Chato...

Acha yawe magofu kama yale ya NHC pale Kawe...

Sijui wale twiga waliopandishwa pickup bado wapo?

Nchi ni yetu sote...
 
Tutakuja ngoja tushughulike na mkataba wa Bagamoyo.

IMG-20210915-WA0057.jpg
 
NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula, amesikitishwa kwa kusuasua kwa utekelezaji wa miradi ya shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wilayani Chato mkoani Geita.
-
Dk Mabula ambaye alitembelea na kukagua miradi hiyo leo Septemba 14, 2021 alionyesha kusikitishwa kutokana na kusuasua kwa utekelezaji wake kunakosababishwa na ucheleweshaji wa fedha.
-
Miradi mitatu inayotekelezwa na NHC ni mradi wa mnada wa mifugo Buzirayombo wenye thamani ya shilingi Bilioni 4.8, mradi wa ujenzi wa shule maalum ya Mbuye Bilioni 5.14 pamoja na mradi wa nyumba 20 za watumishi wa hospitali ya Rufaa ya Kanda- Chato wa thamani ya shilingi Bilioni 1.139
-
Akizungumza mara baada ya kukagua miradi yote mitatu Dk Mabula alisema, miradi hiyo ni muhimu na inapaswa kukamilika kwa wakati ili ianze kutumika.
-
Aidha Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Kagera, Maneno Mahenge, alimwambia Dk Mabula kuwa shirika lake la NHC limekuwa likisuasua kutekeleza kwa kasi miradi katika wilaya hiyo kutokana na kutopatiwa fedha za miradi kwa wakati.
Huyo Waziri hana akili, yaani hajui kwamba hiyo miradi ilisukumwa kwa nguvu na mwendazake ikiwa haina utashi wa NHC ?, ccm kuna ouzo wa viongozi, yeye kama anaweza awaambie ccm watoe hela zikamalizie hiyo miradi ambayo kimsingi haitakuwa na faida yeyote
 
Maamuzi ya mtu mmoja matokeo yake ndo hayo,na vipi hali ya uwanja wa ndege na ujenzi was hospitali ya kikanda na kimataifa hapo Chato? CCM inatakiwa ituombe radhi watanzania kwa mess za mwedazake alizoziacha nyuma.
Kuna watu waliomba wawe Wana Anika mounga na dagaa sijui Kama walikubaliwa au la!
 
Hivi Chato bado ni kitovu cha utalii kanda ya Ziwa ?Kuna chuo cha uongozi kile kama cha Kigamboni ilikuwa kijengwe Chato pia. Hivi lile pori ilipandwa miti inaendeleaje?
 
Kama hiyo miradi ilishaanza ni vyema ikamilishwe tu, serikali ijitahidi kutafuta fedha, kuliko kuacha pesa iliyokwisha tumika ipotee bure, bora miradi ikamilishwe.

Hili linaweza kuwa fundisho huko tuendako, Rais wa nchi asiwe kila kitu, pawepo mamlaka ya kufuatilia na kuagiza nini kifanyike na kipi kisifanyike kwa manufaa ya taifa.
 
Miradi ya Chato inanikumbusha kitabu cha Ngoswe- Penzi kitovu cha uzembe…
Kujipendekeza kwingi kulifanya watu wasahau feasibility study….
 
Huu sasa ni usheitwani kama sio ushirikina.
Naibu waziri ambaye ni serikali anasikitika, meneja wa miradi naye anasikitika.
 
Naomba kujua ufanisi wa Chato airport
 
tatizo ni NHC, TBA na Suma jkt kupewa kandarasi kubwa za ujenzi pasipo kuwa na uwezo wa kufanya miradi hiyo

Tatizo la pili ni ucheleweshaji wa malipo au fedha kutoka serikalini huyo waziri kushangaa ni unafiki!

Tatizo la 3 ni kwamba sio kipaumbele kwa Sasa kwa maendeleo ya Chato
 
Hayo ndiyo matokeo ya Maamuzi ya kibabe na kujipendelea, Mwalimu angekuwa hulka Kama ya Mwendazake kwa miaka 25 aliyokaa madarakani,Butiama ingekuwa Mkoa.
 
Tangu mtu wa kazi rais wa awamu ya tano magufuli afariki miradi ya jimbo /wilaya imesimama jambo lililomkera naibu waziri wa ardhi Ms Mabura

Ukipita chato utashangaa licha ya kuwepo na mipango wa kuifanya kuwa makao makuu ya mkoa mpya wa Geita kila jambo limesimama vyuo,mbuga,uwanja wa ndege, hospital kubwa ya kikanda hadi uwanja wa mpira umekufa

Wananchi wa chato wanaamini tukio la magufuli kusimamisha ujenzi wa bandari ya bagamoyo baada ya kuingia madarakani anajibiwa na yeye akiwa amekufa,




USSRView attachment 1938304
Mwambie kayafa afufuke...Mungu anaipenda sana Tanzania
JamiiForums-1165162837.jpg
 
Ningekuwa mimi Hangaya, ningesema wazi sitoi hata senti tano, mumesha tumia fedha nyingi nje ya bajeti, na tabia ya kujipendelea ife na wanachato muone aibu!
 
Back
Top Bottom