NHC yatelekeza miradi ya mabilioni wilayani Chato

Afadhali...

Tumechoka na viwimbo vya Chato...

Acha yawe magofu kama yale ya NHC pale Kawe...

Sijui wale twiga waliopandishwa pickup bado wapo?

Nchi ni yetu sote...
 
Huyo Waziri hana akili, yaani hajui kwamba hiyo miradi ilisukumwa kwa nguvu na mwendazake ikiwa haina utashi wa NHC ?, ccm kuna ouzo wa viongozi, yeye kama anaweza awaambie ccm watoe hela zikamalizie hiyo miradi ambayo kimsingi haitakuwa na faida yeyote
 
Maamuzi ya mtu mmoja matokeo yake ndo hayo,na vipi hali ya uwanja wa ndege na ujenzi was hospitali ya kikanda na kimataifa hapo Chato? CCM inatakiwa ituombe radhi watanzania kwa mess za mwedazake alizoziacha nyuma.
Kuna watu waliomba wawe Wana Anika mounga na dagaa sijui Kama walikubaliwa au la!
 
Hivi Chato bado ni kitovu cha utalii kanda ya Ziwa ?Kuna chuo cha uongozi kile kama cha Kigamboni ilikuwa kijengwe Chato pia. Hivi lile pori ilipandwa miti inaendeleaje?
 
Kama hiyo miradi ilishaanza ni vyema ikamilishwe tu, serikali ijitahidi kutafuta fedha, kuliko kuacha pesa iliyokwisha tumika ipotee bure, bora miradi ikamilishwe.

Hili linaweza kuwa fundisho huko tuendako, Rais wa nchi asiwe kila kitu, pawepo mamlaka ya kufuatilia na kuagiza nini kifanyike na kipi kisifanyike kwa manufaa ya taifa.
 
Miradi ya Chato inanikumbusha kitabu cha Ngoswe- Penzi kitovu cha uzembe…
Kujipendekeza kwingi kulifanya watu wasahau feasibility study….
 
Huu sasa ni usheitwani kama sio ushirikina.
Naibu waziri ambaye ni serikali anasikitika, meneja wa miradi naye anasikitika.
 
Naomba kujua ufanisi wa Chato airport
 
Ndo mnajilisha matangopori ivo. Mwewe wa atcl anatua km kawaida. Wanaosafiri huku wanajua.
Hahahaha vichekesho vingine sijui tutaendelea kuletewa bure au vitawekewa tozo wallah
 
tatizo ni NHC, TBA na Suma jkt kupewa kandarasi kubwa za ujenzi pasipo kuwa na uwezo wa kufanya miradi hiyo

Tatizo la pili ni ucheleweshaji wa malipo au fedha kutoka serikalini huyo waziri kushangaa ni unafiki!

Tatizo la 3 ni kwamba sio kipaumbele kwa Sasa kwa maendeleo ya Chato
 
Hayo ndiyo matokeo ya Maamuzi ya kibabe na kujipendelea, Mwalimu angekuwa hulka Kama ya Mwendazake kwa miaka 25 aliyokaa madarakani,Butiama ingekuwa Mkoa.
 
Mwambie kayafa afufuke...Mungu anaipenda sana Tanzania
 
Ningekuwa mimi Hangaya, ningesema wazi sitoi hata senti tano, mumesha tumia fedha nyingi nje ya bajeti, na tabia ya kujipendelea ife na wanachato muone aibu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…