SI KWELI NHIF imetoa mkataba kwa shirika binafsi BABULEO LTD kufanya usajili wa Bima kwa watoto walio chini ya miaka kumi na nane

SI KWELI NHIF imetoa mkataba kwa shirika binafsi BABULEO LTD kufanya usajili wa Bima kwa watoto walio chini ya miaka kumi na nane

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
photo_2025-08-15_16-59-01.jpg
 
Tunachokijua
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ni Taasisi ya Bima ya Afya iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Bima ya Afya, Sura namba 395 kwa lengo kuu la kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya kwa watu. Ni taasisi ya Serikali inayofanya kazi chini ya Wizara ya Afya.

Pamoja na utaratibu wa uandikishaji watumishi wa umma, Mfuko umeongeza wigo wake na kujumuisha vikundi vingine kama Madiwani, kampuni binafsi, taasisi za elimu, watu binafsi, watoto chini ya umri wa miaka 21, wakulima katika vyama vya ushirika pamoja na vikundi vilivyosajiliwa kama machinga na vikundi vya bodaboda.

Kuanzia Agosti 13, 2025 kumekuwepo na taarifa inayosambazwa mtandaoni kuwa NHIF imetoa mkataba kwa shirika binafsi BABULEO LTD kufanya usajili wa Bima kwa watoto walio chini ya miaka kumi na nane.

Je, ni upi uhalisia wa Taarifa hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck, Kupitia utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) imebainika kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani haikutolewa wala kuchapishwa na NHIF bali imetengenezwa na wapotoshaji wenye nia ovu.

Vilevile taarifa hiyo hiyo ina mapungufu kadhaa ikiwemo ya kiundishi, na kisarufi, matumizi ya njia za mawasiliano binafsi ikiwemo namba ya simu na barua pepe, jambo linaloitofautisha taarifa hiyo na taarfa halisi zilizowahi kutolewa na TAMISEMI.​
Hii si kweli. Barua yenyewe ina makosa kibao ya kiuandishi. Pia usajili wa sasa wa NHIF unafanyika online.
 
Back
Top Bottom