NHIF inachangia kuua Huduma za Afya kwa kutolipa madeni ya Hospitali

Na huu ndio ukweli. Kama aliyoiua NFRA ndivyo hivyo alivyotaka kuua NHIF.

Ruzuku waliyokuwa wanapewa NHIF ilikatishwa, mfuko ukayumba.

Yaani matumizi ya wachangiaji yalikuwa makubwa kuliko pesa zinazokusanywa na NHIF kutoka kwa wachangiaji.

Kilichofuata ndio hicho. Na ili kuunusuru mfuko kina Anna Makinda wakaamua kuunda vifurushi vipya ambavyo mpaka leo kila mchangiaji analalamika!

Magonjwa mengi wameyaondoa, kima cha chini cha uchangiaji wamepandisha yaani ni zig zag.

Magu alikuwa shetani kabisa.
Duu,balaa kweli kulikuwa na mengi nyuma ya panzia tusiyoyajua.
 
Tatizo pale utawala wa magu ulivyolazimisha mashirika yote ya umma kutumia Nhif kama compulsory scheme, hili limepelekea shirika hili kuzubaa sabab halina upinzani kabisa wa kibiashara.

Yani hapa tumejikuta tunatengeneza tanesco nyingine, Mama samia kama anasoma hapa ajue kabisa ni lazima mfumo wa uendeshaji haya mashirika ubadilike kuwa na free market economy, watu wachague bima inayokidhi mahitaji yao.
 
Watalipa na nini wakati pesa yote mmepeleka kujengea miradi mnayoita ya kimkakati?
Shirika limefirisika limefikia hatua mpaka linakopa afya za watu, watumishi wanakatwa kila mwezi wao wanalipia huduma baada ya miezi mitano ovyo kabisa
 
Tatizo pale utawala wa magu ulivyolazimisha mashirika yote ya umma kutumia Nhif kama compulsory scheme, hili limepelekea shirika hili kuzubaa sabab halina upinzani kabisa wa kibiashara.

Yani hapa tumejikuta tunatengeneza tanesco nyingine, Mama samia kama anasoma hapa ajue kabisa ni lazima mfumo wa uendeshaji haya mashirika ubadilike kuwa na free market economy, watu wachague bima inayokidhi mahitaji yao.
Na huu ndio ukweli
 
Shirika letu la Bima (NHIF) limechangia kuua Huduma za Afya katika kulipa Madai ya Hospitali zetu kwa kuchelewesha kulipa kwa wakati, ambapo hospitali zote nchini zimekuwa zikilamika kuchelewesha malipo hayo ili ziweze kununua dawa,vifaa tiba na kulipa uendeshaji wa hospitali

NHIF imekuwa na tabia ya kukopesha hospitali kwa mda wa miezi mitano(5) kitu kinachopelekea hizi hospitali kuwambia wagonjwa kujinunulia vifaa na dawa ili waweze kutibiwa hali hii imekuwa kero kubwa sana kwa wananchi, na kwa kiwango cha wananch wanaotumia Bima ni zaidi ya 70 %. Na Taifa linakoelekea watu wengi watajiunga na Bima, Hili shirika lispokuwa na Mipango mikakati linaenda kuua Sekta ya afya

Ushauri
- Kuwepo na sheria ya kulipa claim za tasisi na Hospitali kulipwa mapema not more than 2 month
-Uongozi uliopo ufumuliwe ni kero
  • Makato ya ovyo yaangawe upya
  • kuwepo na specialist Mabingwa wenye kukagua ujazaji wa formu za NHIF siyo MD
- Kuwepo na Mfumo wa moja kutoka hospitali mpaka kwenya kitengo
Umeangalia madhaifu ya upande mmoja vipi na zile private hospitals zinazofanya janja janja ili bill iwe iwe kubwa
 
Shirika letu la Bima (NHIF) limechangia kuua Huduma za Afya katika kulipa Madai ya Hospitali zetu kwa kuchelewesha kulipa kwa wakati, ambapo hospitali zote nchini zimekuwa zikilamika kuchelewesha malipo hayo ili ziweze kununua dawa,vifaa tiba na kulipa uendeshaji wa hospitali

NHIF imekuwa na tabia ya kukopesha hospitali kwa mda wa miezi mitano(5) kitu kinachopelekea hizi hospitali kuwambia wagonjwa kujinunulia vifaa na dawa ili waweze kutibiwa hali hii imekuwa kero kubwa sana kwa wananchi, na kwa kiwango cha wananch wanaotumia Bima ni zaidi ya 70 %. Na Taifa linakoelekea watu wengi watajiunga na Bima, Hili shirika lispokuwa na Mipango mikakati linaenda kuua Sekta ya afya

Ushauri
- Kuwepo na sheria ya kulipa claim za tasisi na Hospitali kulipwa mapema not more than 2 month
-Uongozi uliopo ufumuliwe ni kero
  • Makato ya ovyo yaangawe upya
  • kuwepo na specialist Mabingwa wenye kukagua ujazaji wa formu za NHIF siyo MD
- Kuwepo na Mfumo wa moja kutoka hospitali mpaka kwenya kitengo
Kwani NHIF siku hizi inakopesha vituo? Mnatuchanganya wengine wanasema bila NHIF tungekosa mapato wengine mnasema hamlipwi.
 
Uzoefu unaonesha Mfuko umekuwa ukilipa watoa huduma kati ya siku 30 hadi 45 na hii inategemea na mtoa huduma amewasilisha madai yake lini na vipo vituo ambavyo vimekuwa vikilipwa haraka zaidi kwa lengo la kutokwamisha huduma. Sheria inautaka Mfuko kulipa madai ndani ya siku 60.
 
Shirika letu la Bima (NHIF) limechangia kuua Huduma za Afya katika kulipa Madai ya Hospitali zetu kwa kuchelewesha kulipa kwa wakati, ambapo hospitali zote nchini zimekuwa zikilamika kuchelewesha malipo hayo ili ziweze kununua dawa,vifaa tiba na kulipa uendeshaji wa hospitali

NHIF imekuwa na tabia ya kukopesha hospitali kwa mda wa miezi mitano(5) kitu kinachopelekea hizi hospitali kuwambia wagonjwa kujinunulia vifaa na dawa ili waweze kutibiwa hali hii imekuwa kero kubwa sana kwa wananchi, na kwa kiwango cha wananch wanaotumia Bima ni zaidi ya 70 %. Na Taifa linakoelekea watu wengi watajiunga na Bima, Hili shirika lispokuwa na Mipango mikakati linaenda kuua Sekta ya afya

Ushauri
- Kuwepo na sheria ya kulipa claim za tasisi na Hospitali kulipwa mapema not more than 2 month
-Uongozi uliopo ufumuliwe ni kero
  • Makato ya ovyo yaangawe upya
  • kuwepo na specialist Mabingwa wenye kukagua ujazaji wa formu za NHIF siyo MD
- Kuwepo na Mfumo wa moja kutoka hospitali mpaka kwenya kitengo
Ndokeji vepeee......kituo chako kinaitwaje?
Maana utetezi wako hapa unaonyesha umebanwa......NHIF nawapenda Coz claims za kufoji hawalipi.
 
Shirika letu la Bima (NHIF) limechangia kuua Huduma za Afya katika kulipa Madai ya Hospitali zetu kwa kuchelewesha kulipa kwa wakati, ambapo hospitali zote nchini zimekuwa zikilamika kuchelewesha malipo hayo ili ziweze kununua dawa,vifaa tiba na kulipa uendeshaji wa hospitali

NHIF imekuwa na tabia ya kukopesha hospitali kwa mda wa miezi mitano(5) kitu kinachopelekea hizi hospitali kuwambia wagonjwa kujinunulia vifaa na dawa ili waweze kutibiwa hali hii imekuwa kero kubwa sana kwa wananchi, na kwa kiwango cha wananch wanaotumia Bima ni zaidi ya 70 %. Na Taifa linakoelekea watu wengi watajiunga na Bima, Hili shirika lispokuwa na Mipango mikakati linaenda kuua Sekta ya afya

Ushauri
- Kuwepo na sheria ya kulipa claim za tasisi na Hospitali kulipwa mapema not more than 2 month
-Uongozi uliopo ufumuliwe ni kero
  • Makato ya ovyo yaangawe upya
  • kuwepo na specialist Mabingwa wenye kukagua ujazaji wa formu za NHIF siyo MD
- Kuwepo na Mfumo wa moja kutoka hospitali mpaka kwenya kitengo
Hivi kwa nini malalamiko yako usipeleke mamlaka husika na vithibitisho kama unavyo. Huku tutakuonea huruma tu hatuna msaada. Kama una vithibitisho peleka mamlaka husika waitwe wajieleze.
 
Nashangaa kuona wanataka Eti bima iwe kwa waTZ wote ili hali Hawa wachache wa sasa ni mashaka matupu!
Imarisheni kwanza huduma ya uhakika kwa Hawa waliopo kisha ndipo muongeze wigo wa kuwafikia wengi .
 
Shirika letu la Bima (NHIF) limechangia kuua Huduma za Afya katika kulipa Madai ya Hospitali zetu kwa kuchelewesha kulipa kwa wakati, ambapo hospitali zote nchini zimekuwa zikilamika kuchelewesha malipo hayo ili ziweze kununua dawa,vifaa tiba na kulipa uendeshaji wa hospitali

NHIF imekuwa na tabia ya kukopesha hospitali kwa mda wa miezi mitano(5) kitu kinachopelekea hizi hospitali kuwambia wagonjwa kujinunulia vifaa na dawa ili waweze kutibiwa hali hii imekuwa kero kubwa sana kwa wananchi, na kwa kiwango cha wananch wanaotumia Bima ni zaidi ya 70 %. Na Taifa linakoelekea watu wengi watajiunga na Bima, Hili shirika lispokuwa na Mipango mikakati linaenda kuua Sekta ya afya

Ushauri
- Kuwepo na sheria ya kulipa claim za tasisi na Hospitali kulipwa mapema not more than 2 month
-Uongozi uliopo ufumuliwe ni kero
  • Makato ya ovyo yaangawe upya
  • kuwepo na specialist Mabingwa wenye kukagua ujazaji wa formu za NHIF siyo MD
- Kuwepo na Mfumo wa moja kutoka hospitali mpaka kwenya kitengo
1.0 Maelezo ya awali
Kwa mujibu wa Mikataba kati ya NHIF na watoa huduma malipo yanapaswa kufanyika ndani ya siku 60 (miezi 2), ili kuongeza ufanisi Mfuko umejiwekea malengo ya kulipa ndani ya siku 30 pale tu madai (claims) yanapokuwa hayana shida. Changamoto zinazosababisha madai kuchelewa kulipwa ni pale dai likiwa na shida ikiwemo kuwa na viashiriana vya udanganyifu wenye lengo la kuuhujumu Mfuko na kutofuata miongizo ya tiba pamoja na masharti ya mkataba. Dai likikatwa ni pale Mfuko umejiridhisha bila shaka, ila kuna utaratibu wa makubaliano/mapatano (reconciliation) ambapo mtoa huduma na Mfuko hujadili maeneo mbalimbali na kufikia makubaliano rasmi.

Mlango wa reconciliation upo wazi – ila vituo vya afya haswa vile vya binafsi hukwepa kwa wingi wao (siyo wote) kukaa na Mfuko, yote ikiwa ni viashiria vya kutokubali makosa kwa makusudi au tabia endelevu ya kupika madai. Mfuko hupata ushirikiano sana kutoka vituo vya afya vya Serikali – na ni mfano wa kuigwa.

Kama sehemu ya kutolea hasira kwa vituo vingi vya binafsi ni kupitia mitandao ya jamii – taarifa za lawana ambazo ni za upande mmoja; na ambazo zimechujwa kujilinda wao. Hii siyo haki, kama unakuja mtandaoni elezea pande zote mbili, na weka wazi wajibu wa kituo, na kile kisichofanyika kuelekea kukatwa madai.

Kuhusu mikopo ya vituo vya afya; Mfuko unatoa mikopo ya ukarabati wa vituo (facility improvement loan); mikopo ya Tehama (ICT facility loan); mikopo ya vifaa tiba (medical equipment loan); na mikopo ya dawa (medicine and medical consumable loan); marejesho ya mikipo hii inafika hadi miaka 5 kwa kukatwa kidogo kidogo kutoka katika madai yao. Vituo vinakatwa asilimia ndogo, isiyozidi 40% ya madai husika. Mikopo imekuwa mkombozi kwa vituo vya afya katika kuboresha huduma. Hoja ya kuzorota huduma kwa sababu ya mikopo, ni hoja ambayo inahitaji maelezo zaidi, shida ni nini. Ni sawa na kuilaumu benki marejesho ya mkopo wa biashara, wakati uliomba mwenyewe kupanua biashara/mtaji; sasa uovu upo wapi?

2.0 Ukataji madai na Wajibu wa Watoa Huduma

2.1 CAG Report

Turejee muhtasari wa ripoti za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/20 ulioishia tarehe 30/06 iliyowasilishwa tarehe 8/04/2021; *pitia kurasa 56; Hasara itokatokanayo na kukataliwa kwa madai ya fedha za Bima ya Afya Kiasi cha Sh. bilioni 4.46 “Tathmini niliyofanya katika zahanati, vituo vya afya, na hospitali katika Mamlaka 60 za Serikali za Mitaa nilibaini uwepo wa madai yaliyokataliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ikiwa ni gharama za matibabu kwa wagonjwa wanaotumia huduma za bima ya kiasi cha Sh. bilioni 2.28 na sh.bilioni 2.18 kwa Hospitali za Rufaa 26 kutokana na makosa katika ujazaji wa taarifa za wagonjwa pamoja na kutozingatia taratibu kama vile idhini batili, kutozingatia miongozo ya matibabu, kutoonesha vipimo vya utambuzi, na kuingizwa kwa huduma ambazo hazikuwa katika Mfuko. Madai yaliyokataliwa yanaathiri uwezo wa zahanati, vituo vya afya na hospitali katika kutoa huduma za afya kwa jamii kwani hii ni sawa na kutoa huduma za matibabu bure.”

Kadiri unavyosoma ripoti zaidi utagundua Halmashauri ambazo zinasimamia vituo mbalimbali vya afya kwa kutokuwa makini kutunza pesa, au ufujaji zimeshindwa kuhudumia huduma za msingi za jamii kiufanisi ikiwemo manunuzi ya dawa, vifaa tiba n.k; ukweli huu upo pia katika kurasa:

*pitia kurasa 42, matokeo ya ukaguzi wa mamlaka za serikali za mitaa, mapato ya shs. Bilioni 18.769 yalikusanywa lakini hayakupelekwa benki.

*pitia kurasa 44, matokeo ya ukaguzi wa mamlaka za serikali za mitaa, mapato ambayo hayajakusanywa kutoka kwenye vyanzo mbalimbali shs. Bilioni 30.86.

*pitia kurasa 47, matokeo ya ukaguzi wa mamlaka za serikali za mitaa, fedha za mapato ya ndani bilioni 33.96 hazikupelekwa kwenye miradi ya maendeleo

*pitia kurasa 60, Halmashauri ya Manispaa ya Buboka: kutopokelewa kwa vifaatiba kutoka Bohari ya Dawa (MSD) vyenye thamani ya shs. Bilioni 1.08

*pitia kurasa 64, Halmashauri ya jiji la DSM: kutokamilika ujenzi wa zahanati katika kata ya kipunguni kutokana na upotevu wa fedha Sh. 74,093,000

*pitia kurasa 70, Halmashauri ya jiji la Tanga: Vifaatiba Vilivyolipiwa Lakini Havijafikishwa Kituo cha Afya Duga Sh. 175,679,500

Hivyo basi hoja ya Mfuko kutolipa vituo na kusababisha kudhorota kwa huduma haina mashiko. Vituo binafsi ukweli unaweza usiwe mbali pia, tabia za mwanadamu zinafanana, yaweza kuna changamoto za ukaribu kama vituo vya serikali – ukweli ni ngumu kuupata maana CAG hapiti huko!

2.2 Makato ya Vituo
Makato mengi ni kwa sababu ya kutofuata miongozo ya matibabu iliyotolewa na Wizara ya Afya; mf. Muongozo wa STG, muongozo wa magonjwa ya uzazi, muongo wa malaria, etc..

Sababu kubwa nyingine ni kutofuata mkataba wa utoaji huduma (service provision agreement), ambapo ndani yake kuna price list. Yote haya ni kutokujua, kutokuwepo na wafanyakazi walio serious/competent, pia udanganyifu katika madai – uchomekaji wa madai hewa, kupika madai, n.k. Saa nyingine kituo kinaajiri wafanyakazi wapya, orientation hawapati ya kutosha, elimu duni juu ya kushughulikia madai na miongozo ya Wizara, hivyo hujaza sivyo ndivyo madai!

Watoa huduma wana wajibu wa kumuhakiki mwanachama (member verification) kupitia portal ya Mfuko na kutoa authorization number – kinyume na hapo wanaweza kutibu mwanachama asiye hai, hivyo dai hukataliwa iwapo halijafuata utaratibu huu. Watoa huduma wana wajibu wa kuingiza taarifa vizuri katika fomu za madai na katika eClaims system; na hapo inategemewa physical folio na electronic folio zisipishane. Kuna masuala mengine kama signature, attendance date, stamp ya kituo, disease code na namba ya kadi ni muhimu zionekane katika fomu ya madai. Baadhi ya hoja kusema hivi ni vitu vidogo ila kama vinavyoonekana kutofuatwa ni mwanzo wa mwanya wa madai ya kupikwa au udanganyifu; sawa sawa na bank-teller au supervisor aandike cheque alafu afute kwa mkato asahau kusaini (ni jambo dogo ndio ila haitakiwi); au ushawahi ona mhasibu anatumia correction fluid ktk risiti zake? (ni jambo dogo ila hairuhusiwi) – hivyo Mfuko huchukulia kila eneo serious kwa lengo la kulinda uhai na uendelevu wake. La sivyo Mfuko ukifirisika hapa hapa mtaanza kuandika na kuwalaumu Mfuko kuwa walikuwa wapi mpk Mfuko unafirisika!! Ila kama awali nilivyoelezea Mfuko una nafasi ya kukaa na vituo kwa ajili ya mapatano/reconciliation – itumiwe hiyo na huo ndio uungwana, kukaa na kutafuta suluhu ya pamoja.
 
Mbali na kuchelewesha malipo, pia wamekuwa na tabia ya kutolipa kabisa hayo madeni iwapo Form haikujazwa vizuri.

Mgonjwa kashapata matibabu halafu Bima wanagoma kulipa kwa sababu nyepesi tu hiyo hali inafanya wale wanaolipia Cash wathaminiwe kuliko wateja wao wa Bima.
Makato mengi ni kwa sababu ya kutofuata miongozo ya matibabu iliyotolewa na Wizara ya Afya; mf. Muongozo wa STG, muongozo wa magonjwa ya uzazi, muongo wa malaria, etc..

Sababu kubwa nyingine ni kutofuata mkataba wa utoaji huduma (service provision agreement), ambapo ndani yake kuna price list. Yote haya ni kutokujua, kutokuwepo na wafanyakazi walio serious/competent, pia udanganyifu katika madai – uchomekaji wa madai hewa, kupika madai, n.k. Saa nyingine kituo kinaajiri wafanyakazi wapya, orientation hawapati ya kutosha, elimu duni juu ya kushughulikia madai na miongozo ya Wizara, hivyo hujaza sivyo ndivyo madai!

Watoa huduma wana wajibu wa kumuhakiki mwanachama (member verification) kupitia portal ya Mfuko na kutoa authorization number – kinyume na hapo wanaweza kutibu mwanachama asiye hai, hivyo dai hukataliwa iwapo halijafuata utaratibu huu. Watoa huduma wana wajibu wa kuingiza taarifa vizuri katika fomu za madai na katika eClaims system; na hapo inategemewa physical folio na electronic folio zisipishane. Kuna masuala mengine kama signature, attendance date, stamp ya kituo, disease code na namba ya kadi ni muhimu zionekane katika fomu ya madai. Baadhi ya hoja kusema hivi ni vitu vidogo ila kama vinavyoonekana kutofuatwa ni mwanzo wa mwanya wa madai ya kupikwa au udanganyifu; sawa sawa na bank-teller au supervisor aandike cheque alafu afute kwa mkato asahau kusaini (ni jambo dogo ndio ila haitakiwi); au ushawahi ona mhasibu anatumia correction fluid ktk risiti zake? (ni jambo dogo ila hairuhusiwi) – hivyo Mfuko huchukulia kila eneo serious kwa lengo la kulinda uhai na uendelevu wake. La sivyo Mfuko ukifirisika hapa hapa mtaanza kuandika na kuwalaumu Mfuko kuwa walikuwa wapi mpk Mfuko unafirisika!! Ila kama awali nilivyoelezea Mfuko una nafasi ya kukaa na vituo kwa ajili ya mapatano/reconciliation – itumiwe hiyo na huo ndio uungwana, kukaa na kutafuta suluhu ya pamoja.
 
Nashangaa kuona wanataka Eti bima iwe kwa waTZ wote ili hali Hawa wachache wa sasa ni mashaka matupu!
Imarisheni kwanza huduma ya uhakika kwa Hawa waliopo kisha ndipo muongeze wigo wa kuwafikia wengi .
Kuimarishwa kupo, na marekebisho yapo ya mara kwa mara, na itafikiwa tu Universal Health Coverage (Bima ya Afya kwa Wote)

NHIF kama taasisi ya Serikali, chini ya Wizara ya Afya inatekeleza sera ya Taifa ya uchangiaji gharama za utoaji huduma ya matibabu, ya mwaka 1993. Tangu kuanzishwa kwake NHIF (kwa sheria namba 8 ya 1999) imekuwa ikifanya marekebisho mbali mbali yakiwemo ya kitita cha mafao na ya kisheria. Hivyo Mfuko huu umekuwa ukibadilika kadiri na nyakati ziendavyo. Maboresho yataendelea kulingana na changamoto zinazojitokeza. Sheria za marekebisho zilizopita ni za mwaka 2002, 2005, 2009, 2010, 2015. Bila kubagua uchangiaji na ugonjwa mwanachama anapata mafao/huduma mbalimbali: ada ya uandikishaji, gharama ya vipimo, gharama ya dawa, kulazwa, upasuaji, matibabu ya kinywa na meno, n.k

April 2001 wakuu wa nchi wa “African Union” walikutana Abuja, wakaweka maazimio (Abuja Declaration) kwamba angalau waweke asilimia 15% ya bajeti ya nchi kulengea kudumisha sekta ya afya. Ilipofika tarehe 2/05/2011 iligundulika Tanzania tu pekee ndio ilifikia azimio hili; hii inaonyesha jitihada za Serikali ya Tanzania. Na hii pia inaonekana serikali kupitia Wizara ya Afya na taasisi zake ikiwemo NHIF (Bima ya Afya), CHF (Community Health Fund), Tiba kwa Kadi (TIKA), NSSF-SHIB. Na pia serikali imekuwa ikisisitiza wadau binafsi kuwekeza ktk bima ya afya [Private Health Insurance]. Maeneo na taasisi hizi zote zinajenga kitu kimoja - kulinda afya za wananchi. Serikali inadhamiria kuja na mpango wa Bima ya Afya kwa wote; na hotuba ya Mh. Raisi mei mosi 2021 imeelezea bayana.

Mfuko huu siyo kisiwa kinachojitegemea ni mwanachama wa Taasisi za kimataifa katika mlengo wa kupata maoni, industry discipline, n.k. NHIF ni mwanachama ya Shirika la Usanifishaji wa Kimataifa [International Standardization Organization] = ISO 9001:2015; NHIF pia ni mwanachama ya taasisi mbalimbali za kimataifa ikiwemo ISSA, ECASSA hivyo uendeshaji wake una macho mengi.

Mfuko umewekeza katika Tehama; na unazidi boresha mazingira ya uchakataji madai ikiwemo eClaim system na online Claim processing system – ikiwa imeanza kwa baadhi ya vituo vya afya.
 
Hawa waliopo kwa sasa kuwa meneji inaonekana kuwa tatizo sembuse ikiwa bima kwa wote?!

Boresheni kwanza huduma kwa Hawa waliopo sasa na kutafuta mrejesho toka kwa wateja Je hali ya huduma mnaionaje?

Tena mrejesho utakaotolewa na wengi na siyo mapandikizi ya wachache!

Na siyo vinginevyo!
 
Wanachama wanachangia kwa kukatwa mke na mume wakati inatakiwa achangie mmoja tu.

Kila mkiambiwa mkurugenzi Konga hili swala hulioni ni tatizo?

Hii ni dhuluma kubwa sana.

Kama mume na mke wako taasisi moja ambako unaweza kujiridhisha vyeti vya ndoa kwanini mnalazimisha wote wachangie?

Imarisheni namna yenu ya kusimamamia taarifa sahihi na kushindwa kufanya hivyo isiwe kisingizio cha kusema wengine hutoa taarifa za udanganyifu.

Watakaodanganya watambueni sheria ichukue mkondo wake na siyo kishindwa kwenu kusimamamia na kuweka mifumo ya utambuzi wa mapema muwakate mke na mume kwa wakati mmoja..

Bernard Konga na wenzio tafakarini hayo na kuyatolea ufumbuzi wa haraka.

Au mpaka tumwambie Madam President ndipo mtalifanyia kazi hili?
 
Bodi hii ni ovyo kabisa sijapata kuona, imekuwa haina msaada zaidi ya kujilipa wenyewe
Nenda katembelee hospitali mpaka unatamani hivi huu mfuko unasaidiaje hizi hospitali, Mteja anapata huduma wao wanakuja kukagua form na kutofauta makosa madogo madogo na kukata yaani ni bora waunde bodi mpya yenye mkakati wa kusaidia hii tasisi wateja wao na hosipitali zinazotoa huduama
Wewe mpaka inafika NHIF inadaiwa bil 10 haijalipa na taasisi moja sijui wanawaza nini juu uendeshaji wa taasissi hiyo
No research, No right to speak!
Kasome muhtasari wa ripoti za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/20 ulioishia tarehe 30/06 iliyowasilishwa tarehe 8/04/2021; *pitia kurasa 56; Hasara itokatokanayo na kukataliwa kwa madai ya fedha za Bima ya Afya Kiasi cha Sh. bilioni 4.46 “Tathmini niliyofanya katika zahanati, vituo vya afya, na hospitali katika Mamlaka 60 za Serikali za Mitaa nilibaini uwepo wa madai yaliyokataliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ikiwa ni gharama za matibabu kwa wagonjwa wanaotumia huduma za bima ya kiasi cha Sh. bilioni 2.28 na sh.bilioni 2.18 kwa Hospitali za Rufaa 26 kutokana na makosa katika ujazaji wa taarifa za wagonjwa pamoja na kutozingatia taratibu kama vile idhini batili, kutozingatia miongozo ya matibabu, kutoonesha vipimo vya utambuzi, na kuingizwa kwa huduma ambazo hazikuwa katika Mfuko. Madai yaliyokataliwa yanaathiri uwezo wa zahanati, vituo vya afya na hospitali katika kutoa huduma za afya kwa jamii kwani hii ni sawa na kutoa huduma za matibabu bure.”

Halmashauri ambazo zinasimamia vituo mbalimbali vya afya kwa kutokuwa makini kutunza pesa, au ufujaji zimeshindwa kuhudumia huduma za msingi za jamii kiufanisi ikiwemo manunuzi ya dawa, vifaa tiba n.k; ukweli huu upo pia katika kurasa:
*kurasa 42, matokeo ya ukaguzi wa mamlaka za serikali za mitaa, mapato ya shs. Bilioni 18.769 yalikusanywa lakini hayakupelekwa benki.
*kurasa 44, matokeo ya ukaguzi wa mamlaka za serikali za mitaa, mapato ambayo hayajakusanywa kutoka kwenye vyanzo mbalimbali shs. Bilioni 30.86.
*kurasa 47, matokeo ya ukaguzi wa mamlaka za serikali za mitaa, fedha za mapato ya ndani bilioni 33.96 hazikupelekwa kwenye miradi ya maendeleo
*kurasa 60, Halmashauri ya Manispaa ya Buboka: kutopokelewa kwa vifaatiba kutoka Bohari ya Dawa (MSD) vyenye thamani ya shs. Bilioni 1.08
*kurasa 64, Halmashauri ya jiji la DSM: kutokamilika ujenzi wa zahanati katika kata ya kipunguni kutokana na upotevu wa fedha Sh. 74,093,000
*kurasa 70, Halmashauri ya jiji la Tanga: Vifaatiba Vilivyolipiwa Lakini Havijafikishwa Kituo cha Afya Duga Sh. 175,679,500

Hoja ya Mfuko kutolipa vituo na kusababisha kudhorota kwa huduma haina mashiko. Vituo binafsi navyo vina shida ya kiutendaji sehemu moja au nyingine, ni basi tu utendaji wake hauanikwi kama ilivyo upande wa vituo vya serikalini - ama sivyo tungesikia changamoto zake kama CAG angekuwa anapita!

Makato ya Vituo
Makato mengi ni kwa sababu ya kutofuata miongozo ya matibabu iliyotolewa na Wizara ya Afya; mf. Muongozo wa STG, muongozo wa magonjwa ya uzazi, muongo wa malaria, etc..

Sababu kubwa nyingine ni kutofuata mkataba wa utoaji huduma (service provision agreement), ambapo ndani yake kuna price list. Yote haya ni kutokujua, kutokuwepo na wafanyakazi walio serious/competent, pia udanganyifu katika madai – uchomekaji wa madai hewa, kupika madai, n.k. Saa nyingine kituo kinaajiri wafanyakazi wapya, orientation hawapati ya kutosha, elimu duni juu ya kushughulikia madai na miongozo ya Wizara, hivyo hujaza sivyo ndivyo madai!

Watoa huduma wana wajibu wa kumuhakiki mwanachama (member verification) kupitia portal ya Mfuko na kutoa authorization number – kinyume na hapo wanaweza kutibu mwanachama asiye hai, hivyo dai hukataliwa iwapo halijafuata utaratibu huu. Watoa huduma wana wajibu wa kuingiza taarifa vizuri katika fomu za madai na katika eClaims system; na hapo inategemewa physical folio na electronic folio zisipishane. Kuna masuala mengine kama signature, attendance date, stamp ya kituo, disease code na namba ya kadi ni muhimu zionekane katika fomu ya madai. Baadhi ya hoja kusema hivi ni vitu vidogo ila kama vinavyoonekana kutofuatwa ni mwanzo wa mwanya wa madai ya kupikwa au udanganyifu; sawa sawa na bank-teller au supervisor aandike cheque alafu afute kwa mkato asahau kusaini (ni jambo dogo ndio ila haitakiwi); au ushawahi ona mhasibu anatumia correction fluid ktk risiti zake? (ni jambo dogo ila hairuhusiwi) – hivyo Mfuko huchukulia kila eneo serious kwa lengo la kulinda uhai na uendelevu wake. La sivyo Mfuko ukifirisika hapa hapa mtaanza kuandika na kuwalaumu Mfuko kuwa walikuwa wapi mpk Mfuko unafirisika!! Ila kama awali nilivyoelezea Mfuko una nafasi ya kukaa na vituo kwa ajili ya mapatano/reconciliation – itumiwe hiyo na huo ndio uungwana, kukaa na kutafuta suluhu ya pamoja.
 
Wanachama wanachangia kwa kukatwa mke na mume wakati inatakiwa achangie mmoja tu.

Kila mkiambiwa mkurugenzi Konga hili swala hulioni ni tatizo?

Hii ni dhuluma kubwa sana.

Kama mume na mke wako taasisi moja ambako unaweza kujiridhisha vyetu vya ndoa kwanini mnalazimisha wote wachangie?

Imarisheni namna yetu ya kusimamamia taarifa sahihi na isiwe kisingizio cha kusema wengine hutoa taarifa za udanganyifu.

Watakaodanganya watambueni sheria ichukue mkondo wake na siyo kishindwa kwenu kusimamamia na kuweka mifumo ya utambuzi wa mapema muwakate mke na mume kwa wakati mmoja..

Bernard Konga na wenzio tafakarini hayo na kuyatolea ufumbuzi wa haraka.
Hivi wewe hujui kupiga hesabu, kuna familia zetu wengine kubwa, wazazi wa pande zote mbili, watoto bado na mke wa pili, we peke yako utaweza kubeba. Mbona huoni fursa khaaa heheee.

ila kwann watanzania wanajichimbiaga mashimo wenyewe nimeamini.
 
Back
Top Bottom