Shirika letu la Bima (NHIF) limechangia kuua Huduma za Afya katika kulipa Madai ya Hospitali zetu kwa kuchelewesha kulipa kwa wakati, ambapo hospitali zote nchini zimekuwa zikilamika kuchelewesha malipo hayo ili ziweze kununua dawa,vifaa tiba na kulipa uendeshaji wa hospitali
NHIF imekuwa na tabia ya kukopesha hospitali kwa mda wa miezi mitano(5) kitu kinachopelekea hizi hospitali kuwambia wagonjwa kujinunulia vifaa na dawa ili waweze kutibiwa hali hii imekuwa kero kubwa sana kwa wananchi, na kwa kiwango cha wananch wanaotumia Bima ni zaidi ya 70 %. Na Taifa linakoelekea watu wengi watajiunga na Bima, Hili shirika lispokuwa na Mipango mikakati linaenda kuua Sekta ya afya
Ushauri
- Kuwepo na sheria ya kulipa claim za tasisi na Hospitali kulipwa mapema not more than 2 month
-Uongozi uliopo ufumuliwe ni kero
- Makato ya ovyo yaangawe upya
- kuwepo na specialist Mabingwa wenye kukagua ujazaji wa formu za NHIF siyo MD
- Kuwepo na Mfumo wa moja kutoka hospitali mpaka kwenya kitengo
1.0 Maelezo ya awali
Kwa mujibu wa Mikataba kati ya NHIF na watoa huduma malipo yanapaswa kufanyika ndani ya siku 60 (miezi 2), ili kuongeza ufanisi Mfuko umejiwekea malengo ya kulipa ndani ya siku 30 pale tu madai (claims) yanapokuwa hayana shida. Changamoto zinazosababisha madai kuchelewa kulipwa ni pale dai likiwa na shida ikiwemo kuwa na viashiriana vya udanganyifu wenye lengo la kuuhujumu Mfuko na kutofuata miongizo ya tiba pamoja na masharti ya mkataba. Dai likikatwa ni pale Mfuko umejiridhisha bila shaka, ila kuna utaratibu wa makubaliano/mapatano (reconciliation) ambapo mtoa huduma na Mfuko hujadili maeneo mbalimbali na kufikia makubaliano rasmi.
Mlango wa reconciliation upo wazi – ila vituo vya afya haswa vile vya binafsi hukwepa kwa wingi wao (siyo wote) kukaa na Mfuko, yote ikiwa ni viashiria vya kutokubali makosa kwa makusudi au tabia endelevu ya kupika madai. Mfuko hupata ushirikiano sana kutoka vituo vya afya vya Serikali – na ni mfano wa kuigwa.
Kama sehemu ya kutolea hasira kwa vituo vingi vya binafsi ni kupitia mitandao ya jamii – taarifa za lawana ambazo ni za upande mmoja; na ambazo zimechujwa kujilinda wao. Hii siyo haki, kama unakuja mtandaoni elezea pande zote mbili, na weka wazi wajibu wa kituo, na kile kisichofanyika kuelekea kukatwa madai.
Kuhusu mikopo ya vituo vya afya; Mfuko unatoa mikopo ya ukarabati wa vituo (facility improvement loan); mikopo ya Tehama (ICT facility loan); mikopo ya vifaa tiba (medical equipment loan); na mikopo ya dawa (medicine and medical consumable loan); marejesho ya mikipo hii inafika hadi miaka 5 kwa kukatwa kidogo kidogo kutoka katika madai yao. Vituo vinakatwa asilimia ndogo, isiyozidi 40% ya madai husika. Mikopo imekuwa mkombozi kwa vituo vya afya katika kuboresha huduma. Hoja ya kuzorota huduma kwa sababu ya mikopo, ni hoja ambayo inahitaji maelezo zaidi, shida ni nini. Ni sawa na kuilaumu benki marejesho ya mkopo wa biashara, wakati uliomba mwenyewe kupanua biashara/mtaji; sasa uovu upo wapi?
2.0 Ukataji madai na Wajibu wa Watoa Huduma
2.1 CAG Report
Turejee muhtasari wa ripoti za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/20 ulioishia tarehe 30/06 iliyowasilishwa tarehe 8/04/2021; *pitia kurasa 56;
Hasara itokatokanayo na kukataliwa kwa madai ya fedha za Bima ya Afya Kiasi cha Sh. bilioni 4.46 “Tathmini niliyofanya katika zahanati, vituo vya afya, na hospitali katika Mamlaka 60 za Serikali za Mitaa nilibaini uwepo wa madai yaliyokataliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ikiwa ni gharama za matibabu kwa wagonjwa wanaotumia huduma za bima ya kiasi cha Sh. bilioni 2.28 na sh.bilioni 2.18 kwa Hospitali za Rufaa 26 kutokana na makosa katika ujazaji wa taarifa za wagonjwa pamoja na kutozingatia taratibu kama vile idhini batili, kutozingatia miongozo ya matibabu, kutoonesha vipimo vya utambuzi, na kuingizwa kwa huduma ambazo hazikuwa katika Mfuko. Madai yaliyokataliwa yanaathiri uwezo wa zahanati, vituo vya afya na hospitali katika kutoa huduma za afya kwa jamii kwani hii ni sawa na kutoa huduma za matibabu bure.”
Kadiri unavyosoma ripoti zaidi utagundua Halmashauri ambazo zinasimamia vituo mbalimbali vya afya kwa kutokuwa makini kutunza pesa, au ufujaji zimeshindwa kuhudumia huduma za msingi za jamii kiufanisi ikiwemo manunuzi ya dawa, vifaa tiba n.k; ukweli huu upo pia katika kurasa:
*pitia kurasa 42, matokeo ya ukaguzi wa mamlaka za serikali za mitaa, mapato ya shs. Bilioni 18.769 yalikusanywa lakini hayakupelekwa benki.
*pitia kurasa 44, matokeo ya ukaguzi wa mamlaka za serikali za mitaa, mapato ambayo hayajakusanywa kutoka kwenye vyanzo mbalimbali shs. Bilioni 30.86.
*pitia kurasa 47, matokeo ya ukaguzi wa mamlaka za serikali za mitaa, fedha za mapato ya ndani bilioni 33.96 hazikupelekwa kwenye miradi ya maendeleo
*pitia kurasa 60, Halmashauri ya Manispaa ya Buboka: kutopokelewa kwa vifaatiba kutoka Bohari ya Dawa (MSD) vyenye thamani ya shs. Bilioni 1.08
*pitia kurasa 64, Halmashauri ya jiji la DSM: kutokamilika ujenzi wa zahanati katika kata ya kipunguni kutokana na upotevu wa fedha Sh. 74,093,000
*pitia kurasa 70, Halmashauri ya jiji la Tanga: Vifaatiba Vilivyolipiwa Lakini Havijafikishwa Kituo cha Afya Duga Sh. 175,679,500
Hivyo basi hoja ya Mfuko kutolipa vituo na kusababisha kudhorota kwa huduma haina mashiko. Vituo binafsi ukweli unaweza usiwe mbali pia, tabia za mwanadamu zinafanana, yaweza kuna changamoto za ukaribu kama vituo vya serikali – ukweli ni ngumu kuupata maana CAG hapiti huko!
2.2 Makato ya Vituo
Makato mengi ni kwa sababu ya kutofuata miongozo ya matibabu iliyotolewa na Wizara ya Afya; mf. Muongozo wa STG, muongozo wa magonjwa ya uzazi, muongo wa malaria, etc..
Sababu kubwa nyingine ni kutofuata mkataba wa utoaji huduma (service provision agreement), ambapo ndani yake kuna price list. Yote haya ni kutokujua, kutokuwepo na wafanyakazi walio serious/competent, pia udanganyifu katika madai – uchomekaji wa madai hewa, kupika madai, n.k. Saa nyingine kituo kinaajiri wafanyakazi wapya, orientation hawapati ya kutosha, elimu duni juu ya kushughulikia madai na miongozo ya Wizara, hivyo hujaza sivyo ndivyo madai!
Watoa huduma wana wajibu wa kumuhakiki mwanachama (member verification) kupitia portal ya Mfuko na kutoa authorization number – kinyume na hapo wanaweza kutibu mwanachama asiye hai, hivyo dai hukataliwa iwapo halijafuata utaratibu huu. Watoa huduma wana wajibu wa kuingiza taarifa vizuri katika fomu za madai na katika eClaims system; na hapo inategemewa physical folio na electronic folio zisipishane. Kuna masuala mengine kama signature, attendance date, stamp ya kituo, disease code na namba ya kadi ni muhimu zionekane katika fomu ya madai.
Baadhi ya hoja kusema hivi ni vitu vidogo ila kama vinavyoonekana kutofuatwa ni mwanzo wa mwanya wa madai ya kupikwa au udanganyifu; sawa sawa na bank-teller au supervisor aandike cheque alafu afute kwa mkato asahau kusaini (ni jambo dogo ndio ila haitakiwi); au ushawahi ona mhasibu anatumia correction fluid ktk risiti zake? (ni jambo dogo ila hairuhusiwi) – hivyo Mfuko huchukulia kila eneo serious kwa lengo la kulinda uhai na uendelevu wake. La sivyo Mfuko ukifirisika hapa hapa mtaanza kuandika na kuwalaumu Mfuko kuwa walikuwa wapi mpk Mfuko unafirisika!! Ila kama awali nilivyoelezea Mfuko una nafasi ya kukaa na vituo kwa ajili ya mapatano/reconciliation – itumiwe hiyo na huo ndio uungwana, kukaa na kutafuta suluhu ya pamoja.