NHIF inachangia kuua Huduma za Afya kwa kutolipa madeni ya Hospitali

Hivi wewe hujui kupiga hesabu, kuna familia zetu wengine kubwa, wazazi wa pande zote mbili, watoto bado na mke wa pili, we peke yako utaweza kubeba. Mbona huoni fursa khaaa heheee.

ila kwann watanzania wanajichimbiaga mashimo wenyewe nimeamini.


Nisome vizuri sana huenda hujanielewa vizuri.

Mume na mke wote wanakatwa michango ya bima kuchangia watu wale wale .

Wakati inatakiwa mmojawapo tu ndiye achangie.

Hivi unaelewa lakini ?
 
Nisome vizuri sana huenda hujanielewa vizuri.

Mume na mke wote wanakatwa michango ya bima kuchangia watu wale wale .

Wakati inatakiwa mmojawapo tu ndiye achangie.

Hivi unaelewa lakini ?

We una familia umeoa na mke na ana kadi na ana nafasi nne za wategemezi na we nne.... wote mnafanya kazi. Niambie, wewe unaweza kuwabeba wazazi wote na watoto wote ........... peke yako?
 
We una familia umeoa na mke na ana kadi na ana nafasi nne za wategemezi na we nne.... wote mnafanya kazi. Niambie, wewe unaweza kuwabeba wazazi wote na watoto wote ........... peke yako?


Kwani hizo nafasi 4 ni pamoja na watoto?

Wazazi wana nafasi zao mbali na nafasi za watoto 4.

Isitoshe kwa wale ambao wana extend families mfano mitala n.k

Uwepo utaratibu wa wale ambao wanahitaji kukatwa wote mke na mume kwa sababu zao wakatwe na wale ambao kutokana na facts zao hawastahili kukatwa wasikatwe wote , achangie mmoja tu.

Yule ambaye hana mzigo wa wategemezi wengi asilazimishwe kuchangia mke na mume .

Kusiwepo na mazoea au kukariri kwenye hili.

Kuna wengi wamejikuta mke na mume wanakatwa kwa dependants wale wale , walioko kwa mume Ndiyo walioko kwa mke , sasa huoni kuna dhuluma?

Kama anaochangia mke na anaochangia mume ni dependants tofauti hapo inakuwa sawa na haki na siyo kuwa walewale.

Umenisoma vema sasa?
 
Jaribu kutaka uelewa kwanza Mtanzania. Nafasi nne unaweza kuweka wazazi au watoto. Upo apo?
 
Actually hii imeshajidiriwa sana tena mara nyingi kwenye vikao rasmi vye kiofisi na hao jamaa wa NHIF na wanachama.

Jibu ambalo walitoa wakati fulani ni swala la udanganyifu toka kwa baadhi ya wanachama .

Lakini swala la udanganyifu wa wengine Ndiyo iwe fimbo ya kuwaadhibu wengine ambao siyo wadanganyifu?

Wanatakiwa waweke mifumo yao vizuri ili iwapo mwanachama atawadanganya wamtambue mapema na kumchukulia hatua kali za kisheria na siyo kuwakata mume na mke michango ambayo dependants ni wale wale.
 
Kwanza tuwe waungwana kama misingi ya JamiiForums, moja ni kuheshimu nafasi za kazi/uteuzi au heshima tu kwa mtu - kutajana majina siyo jambo jema, tumia tu cheo - Mkurugenzi Mkuu, au "cheo-flani" inatosha kufikisha ujumbe..

Mbili, naona kama vile ume-divert ktk hoja ya vituo thread iliyoanzishwa na kuingia ktk specific issues - unrelated..

Okay, kujibu hoja yako ni hivi: ukipitia sheria ya NHIF ya 1999 na marekebisho yake 2002, 2005, 2009, 2010, 2015, inaongelea makato kwa mtumishi mwajiriwa. Yatosha ieleweke makato haya kisheria ndiyo msingi wa undugu wa kuchangiana matibabu. Ni kama ilivyo PAYE unakatwa lakini yawezekana nje ya nyumbani kwako barabara ni ya vumbi, yawezekana unataka lami; kupitia PAYE ya mwajiri na kodi nyinginezo mpaka za vinywaji/madukani ungetemea maji yakufikie ila labda bado - ila haimaanishi hiyo kodi haifanyi kazi, au haifikii wengine, au haitakufikia na wewe.

Vivyo hivyo, mchangiaji na mwenza wanakatwa kama sehemu ya kutimiza sheria, ila pia wanakatwa kama sehemu ya kutunisha Mfuko. Watanzania tunatakiwa tujifunze kuwa wazalendo, kuupenda Mfuko na kuona faida yake kwa jicho pana zaidi, na siyo kujiangalia kipekee (individualistic). Leo unaweza kuona unanyanyasika kukatwa wewe na mwenza; kesho akija ndugu yako kuomba laki 6 mfano kwa ajili ya matibabu ya mtoto wake, unampa Tsh. 50,400 na kumwambia akakate Toto Afya NHIF atapata matibabu yote - ila ngumu kumeza ni kusukumiza fikra nyuma ya ubongo hiyo difference inatoka kwa nani (600,000 - 50,400); kama siyo uzalendo wa uchangiaji? I can justify this point all over and over with different scenario ila kama jicho la kiuzalendo na undugu limefungwa ila lililo wazi ni individualistic we shall always be parting ways..

Yatosha ieleweke makato haya nayo ni akiba kwa lile usilolijua mbele:
i] Moja ya ukomo wa uchangiaji ni kifo, na hivyo huduma hukwama; sasa let us assume for a moment mwenza ulikuwa huchangii, unatengemea Bima ya mwenzako, alafu ikatokea akafariki - na wewe na watoto mkawa ktk immediate need ya medical service hapo hiyo taharuki unaiwekaje? Upande mmoja umetoka kuzika - na upande mmoja magonjwa/shida hazitatuliki bila pesa, kwa sababu huna Bima.

ii] Uchangiaji huu ni akiba ya credits kukusaidia upate fao la ustaafu; kwa macho ya kutoona mbele waweza sema hakuna msingi wa kuchangia uengemee kwa mume/mke; ila itakapotokea mwenza wako akapata ajali kazini/ulemavu akashindwa kufanya kazi; au akaachishwa au worse akafariki..piga picha miaka imeenda na credits umekosa za ustaafu, unajitengenezea ugumu wa maisha kwa sababu ambazo zingeepukika.

iii] Uchangiaji huu unakusaidia kuwaweka wategemezi: mwenza, watoto wako wa kuzaa, watoto wako wa kufikia, watoto wa kuasili (adopted children), wazazi, wakwe. Ni fursa pana ya kuwaweka hawa wategemezi. Wengi huingia ktk mkumbo wa kulalamika "mimi na mke tunakatwa" kwa kutokujua extent ya coverage aliyonayo. Mwingine anajua ila baada ya kuonja tunda la neema na akaitumia kuweka hawa wategemezi, anaona hakuna haja tena (unthankfulness & ignorance); na mwingine inatokea hana hawa wategemezi (unfortunate circumstance)..ila ktk jicho pana ni msaada wa kuweka wategemezi na kuondoa gharama za maisha.
 
Jaribu kutaka uelewa kwanza Mtanzania. Nafasi nne unaweza kuweka wazazi au watoto. Upo apo?


Wewe ni msemaji wa NHIF humu?

Kama siyo msemaji changia yako lakini usichangie kama msemaji ukapotosha watu.

Nikikwambia uweke ile copy yao ya wategemezi tuone Muundo wao utakuwanayo na kuweza kuiweka hapa?

Nazani kama wewe siyo msemaji wao usiwe jaji wa kuwahukunu wachangiaji wengine.
 


Weeee nawe buana!

Wanatajwa majina ya wahemishimiwa Marais kwa majina yao, wakuu wa majeshi na vyombo vya usalama kwa vyoo na majina yao, IGPs n.k itakuwa huyo CEO wa NHIF?

Halafu wewe utakuwa ni ndiye Konga mwenyewe!

Asitajwe kwanini sasa wakati ni Mtumishi wa Umma ?

Yani ukubali kuteuliwa na kuwa Mtumishi wa Umma Tena sehema nyeti ya matibabu halafu hutaki ujulikane wala kutajwa jina ?

Chukua kile tunachikisema kifanyie kazi achana na hofu wala mashaka.

Wewe naanza kutilia shaka kiwango chako cha ufahamu?!

Tafakari.
 
Na wewe usiwe Jaji msaidizi
 
Na wewe usiwe Jaji msaidizi


Kwani una mitala ?

Kama imani yako inakuruhusu sawa lakini wale ambao hawana mitala basi wasikatwe wote maana wanajikuta wanachangia dependants wale wale.
 

Usiweke fact za uongo hapa hospitali zote kuanzia vituo vya afya mpaka National hospital wanadai malipo yao zaidi ya miez 5 ,Mwisho mlilipa Mwaka jana November Mpaka leo hospitali zinajiendesha kihasara, Wagonjwa wanapata shida vifaa tiba vinapohitajika inafika sehemu Mgonjwa anaambia akanunue gloves, crep bandage, p.o.p hospitali hazina kitu harafu mnatwambia mkataba miez miwili wapi hiyo
Hii Bodi ni bora ifumuliwe tu....
Ovyo kabisa Dawa zingine Mara zinatolewa
 
S
Shida zenu Mnajibu kwa kutumia Makaratasi mkiwa ofisini mnakunywa kahawa ndio maana hii nchi inawatu wa ovyo sijawahi pata kuona, Sisi tunaowaeleza ukweli tunaojionea tunapokwenda kutibiwa mahospitalini na kuona hali halisi
Nyinyi mnajiona mnaelewa sana kumbe ni uelewa fake
Nendeni field mkajionee hali halisi
Vile vile tuambie mwisho kulipa madai ya hospitali ni lini
 
Uongo wako Konki aisee ... safi kabisa ...
 
Hapa anahitajika adjudicator. Huyu awe independent. Ni go between ya huduma hasa hawa NHIF na hizi private. Aweze hata kutoza penalty kwa NHIF au facilities danganyifu. Ikiwepo penalty ya kuchelewa kulipa vituo au hospital.
 
Huu uzi umeleta wageni wengi watetezi.
Kawatuma Boss wao lakini ukweli ni kwamba tunakoelekea hili shirika bila mipango mikakati madhubuti litaua huduma za afya kwa kasi ya hatari
Ikumbukwe kwa sasa wananchi wengi wanajiunga na Bima
Itafika Mahala wagonjwa wa cash watapungua
Bima wanachelewesha malipo, Je Hospitali zitajiendeshaje?
 
Serikali itoe tamka kwenye hili swala ni aibu kuwa na mfuko wenye matatizo makubwa namna hii wao viongozi wako kimya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…