NHIF kupunguza muda wa mahudhurio ya hospitali kutoka 360 kwa mwaka hadi 36, pia itatumia bei ya soko kwa dawa za kansa na kusafisha figo

NHIF imefilisiwa na serikali halafu wanapa watu mzigo, serikali iache kutumia hela za mifuko kwa mambo tofauti
 
Hapa kwetu mfuko ndo unaipa serikali hela
 
Wangeweka vigezo vya siku ya mahudhurio kati ya watumishi wa serikali na walio nje, maana watumishi wa serikali wanaojiunga asilimia kubwa hawajiunga sababu wanaumwa ila walio nje hujiunga kutokana na magonjwa na ndio wanabebesha mfuko huu mzigo ikishindikana waruhusu mashirika mengine ya afya yawekeze ili kuwe na ushindani.
 
NHIF inaelemewa sababu ya

Inakopesha hospital
Inakopesha serikali pesa

Watumishi wa umma wengi mishahara midogo ila wana wategemezi wengi
Katika yote hayo hakuna kinachoifanya NHIF kuwa hivyo.
 
Kuna shida ya uelewa kwa wengi. Mashirika ya bima ya afya yapo mengi, tatizo ni gharama kubwa na ndio kinachowashinda wengi. Mwalimu anayelipwa mshahara wa laki 5 kwa mwezi ataweza kuwa na bima Kama ya jubilee au strategies ambao makato yao kwa mwezi ni karibu laki 1??
 
Ningekuwa raisi juma tatu ungekuwa unakula kiapo chako chakuwa waziri wa afya uanze utekelezaji mara moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawaunga mkono hapo kwenye magonjwa yasiyoamBUkiza.kansa ndio sielewi vyavzo vyake but presha,kisukali na figo vinajulikana.labda wafanye kwa wale wanaozidi miaka 60 wao watibiwe tu lkn hawa vijana wanywa pombe chini ya miaka 50 wanasafisha figo ukimuuliza anakujibu ni POMBE.
 
Rudisha kishikwambi cha watu karani.
 
Mashirika binafsi ya Bima yapo. Tuseme wafanyakazi waachwe wachague wapi wanataka kujiunga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…