Mnaosema hivyo vifurushi ni bei rahisi labda kwa kulinganisha na bima zingine, watoto walikua ni elfu 50, hapo kwenye vifurushi ni karibu laki 2, tunaambiwa wazee wa zaidi ya miaka 60 ni bure lakini hapo wana vifurushi vyao, ni watu wachache sana wenye watoto wanne na umri wao ni chini ya 35, wengi wenye watoto wa4 wanaangukia kwenye fungu la pili 36-59 ambapo gharama zipo juu.
Cha muhimu serikali ingepunguza zaidi hizo gharama angalau kiwango cha juu kabisa kiwe milioni moja, na iongeze fungu kufidia gharama za kutibu wananchi wake, watu wakiwa wazima watafanya kazi na serikali itapata kodi zaidi.