NHIF matatani, kilio cha wamiliki wa hospitali binafsi kukatwa mabilioni ya fedha chaibuka

NHIF hawako consistent kwenye makato wanayoyafanya, which inashusha credibility yao na kuonekana wahuni.

Kuna kipindi flani tuliambiwa tusifanye USS unless mteja ni mjamzito. Mwezi uliofuata tukafanya kama walivyotuambia, lakini cha ajabu walikata USS karibu nusu. Tulipolalamika, wakasema hamuwezi kuwa na wagonjwa wengi kiasi hiki. Tukawaambia basi angalieni mafaili ya wagonjwa, wakatishia kutufungia. Ikabidi tuwe wapole.
 
Kweli, umemaliza mkuu. Daktari kaona mgonjwa na kumpima ,NHIF wanasema Daktari hakupaswa kufanya hivyo vipimo, sasa kama hawataki watu watibiwe si waache kuchukua fedha za watu.

Sema hospitali private nao wanapiga hela kupitia NHIF. Mi niliwahi andikiwa risiti ya magongo ya miguu ila sikutapata na pesa najua hospitali walichukua
 
Hapa ni kuwashikisha adabu wote; NHIF na wamiliki wa Hospitali na hata maduka ya madawa. NHIF ni wapenda rushwa! Miaka yote kuiba kupitia hospitali, Hospitali nao wakawa ni sehemu ya wizi huo, mbali na kushirikiana na maafisa wa NHIF wakaanza kuongeza gharama za kipuuzi kabisa na kuandika hata vipimo ambavyo havikufanyika kwa mgonjwa.

Pharmacy nao wako hivyo wakishirikiana na madaktari wanapojaza fomu za NHIF, inaachwa mwanya wa kuongeza hata madawa ambayo mgonjwa hakuyatumia. Unapewa dawa unazostahili, halafu zinaongezwa zingine za gharama kubwa ambazo hata hukuzitumia na hata pharmacy haina.

Ni nchi inayohitaji mkono wa chuma bado! Tusilalamike kwa niaba ya wengine. Kila mtu anafahamu uaminifu mbovu alionao ingawa kamanda wa yote hayo ni NHIF!
 
Kweli, umemaliza mkuu. Daktari kaona mgonjwa na kumpima ,NHIF wanasema Daktari hakupaswa kufanya hivyo vipimo, sasa kama hawataki watu watibiwe si waache kuchukua fedha za watu.
Kwahiyo hawataki watu wapimwe tena mbona makubwa haya.
 
Sema hospitali private nao wanapiga hela kupitia NHIF. Mi niliwahi andikiwa risiti ya magongo ya miguu ila sikutapata na pesa najua hospitali walichukua
Eti kuna hospitali zinatoza laki 6 kama gharama ya kitanda kwa usiku mmoja! Utadhani uko 5-star hotel yenye heated swiming pool!
 
Yote hii ni kwa sababu ya matumizi ya paper work mpaka leo miaka zaidi ya 50 ya uhuru. NHIF anatakiwa awe na mfumo aachane na kutegemea karatasi ambazo hospitali wanaweza kuziedit
 
Wakati mwingine kadi ya NHIF haina tofauti sana na kitambulisho cha machinga.... takataka tu.
 
Nhif konyo sana!
 
Kubinywa kwa uhuru wa huduma na kutegemea kitu kimoja ndo madhara yake

Bima nyingine mbona zinalipa bila kukata

Ni muda sasa wananchi hasa watumishi waachwe wachague mfuko wakuchangia inaweza boresha hata huduma vituoni


Sio NHIF na apo unakuta baba mfanyakazi
Wanufaika
Mama mzazi na baba
Mke wake
Watoto wakuwazaa

Ni population kubwa Sana ambayo mwisho wa siku wanaopata shida ni wananchi kwa kukosa baadhi ya huduma
Na kifo cha hospital binafsi
 
nafikiri makato siyo vituo binafsi tu hata serkalini wanawapiga panga.tofauti ni kuwa hospitali za serikalini wao wafanyakazi wanalipwa na serkali kuu. kusema kweli kuna kipindi unatamani kulia maana unakuta wamekata 3 million ambayo ungeweza kuwalipa wafanyakazi.

Naikiri tukubariane kwamba daktari ndiye akatwe kwenye mshahara wake .kwa sababu dakatri ndiye centa wa kila kitu.so kama amesababisha makato kufanyika basi yeye ndiye akatwe kwenye mshahara ndipo yeye aende ofisi za NHIF kudai kurejeshewa hela hizo.

Mmiliki wa vituo tunaonewa sana yani inabidi ubebe makosa ya daktari wakati hukushiriki makosa

Too bad and too sad.
 
Kubinywa kwa uhuru wa huduma na kutegemea kitu kimoja ndo madhara yake

Bima nyingine mbona zinalipa bila kukata....
siyo kweli .kwa sasa wote wameiga ushetani wa NHIF sema tu gharama za matibabu kwenye hizo bima nyengine ni kubwa so unaweza ku compensate
 
siyo kweli .kwa sasa wote wameiga ushetani wa NHIF sema tu gharama za matibabu kwenye hizo bima nyengine ni kubwa so unaweza ku compensate
NHIF wanaa makato feki ambayo hata maelezo hayana nna mfano wa vituo

Wanakata Hadi nusu

Mtu kaomba. Mil 30 kapewa 16mil

Huu ni upuuzi na ni kwasababu ya monopoly ya huduma iyo
 
Na bado mtafyekwa Sana reli zijengwe na ndege zinunuliwe
 
NHIF hiyo tabia hawajaanza leo. Uliza wenye pharmacy Moshi au Morogoro watakupa habari yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…