NHIF matatani, kilio cha wamiliki wa hospitali binafsi kukatwa mabilioni ya fedha chaibuka

Tusikimbilie kuwahukumu Nhif sababu wamiliki wa hospital wameulizia mikoa mingine wameambiwa hakuna kitu kama hicho hivyo inawezekana ni tatizo binafsi la wafanyakazi wa nhif Mwanza.
Nadhani ni mikoa mingi sana wanakumbana na kadhia hiyo, mfano mikoa ambayo nilisikia wakilalamika ni Kilimanjaro(Moshi) na Morogoro,ilikuwa mwanzoni mwa mwaka huu, kwasasa sijui hali iko vip huko kwa sasa. Wanadai kwenye malipo ya 250M unaweza katwa 50-80M kwa sababu za kijinga au wakati mwingine bila sababu yoyote.
 
Uhai wa bodi ya wakurugenzi NHIF upo mashakani
 

Wagonjwa wengi sasa NHIF kweli.

NHIF ni mfuko bora kuliko mifuko mingine. Ukiugua muda mrefu au ugonjwa mkubwa ndio unaweza kulitambua hili pale ambapo utaambiwa account yako haina salio la kuendelea na huduma kitu ambacho ni tofauti kabisa kwa NHIF

Mwanzoni malalamiko juu NHIF ilikua ni wagonjwa kupata huduma mbovu, ikaja kuondolewa kwa baadhi ya vipimo na dawa kwenye list yao na sasa hayo yamepita imekuja ya watoa huduma kunyengwa malipo na kutopewa report za wanacholipwa

Serikali ilitupie macho hili na kuhakikisha watendaji wa NHIF wanatoa huduma kwa jamii na sio huduma ya kujinufaisha wao binafsi.
 
Baba yako katumia pesa zao kupindisha matokeo ya uchaguzi. Vumilia tu kwani hiyo ndiyo sadaka kwa mapenzi yako kwa CCM. Kilangila.
 
Habari hizi zina ukakasi kwasababu ni Hispitali zote zinalipwa kwa muda na kwa sasa kuna mfumo ambao NHIF wanawezesha vituo kuchakata madai ndani ya siku 14 unalipwa. Maneno ya kuchafua taasisi inayohudumia wanachama zaidi ya millioni nne ya Watanzania ni kutafuta kiki.
 

Lazima HIHF wajihami sana kwa ujanja wa wenye hospitali binafsi. Mwenyewe nilienda hospitali moja dar nadhani siku hizi NIHF wameintroduce software consultation na documentation zote ni kwa mtandao. Baada ya matibabu nikaonyeshwa sehemu kwenye chombo cha electronic niweke sahihi. Ndipo nikamwbia yule mtumishi hua sitii sahihi bila kujua najicommit kwa kitu gani. Nikamwambie anioneshe gharama kabla ya kutia sahihi.
 
We hata huelewi kinachoongelewa.
 
Kwa sasa kufanya biashara na serikali ni hatari sana,jamaa kukudhulumu/kukunyang'anya haki zako ni kawaida tu na ukileta mdomo unaweza pigwa uhujumu uchumi au jamaa wa TRA ukaletewa chap chap.

Hakika MITANO TENA,Nasema uongo ndg zanguuuuuuuuuuuuuuuuuuu.
 
Hili tatizo limekuwa sugu wamiliki wa vituo binafsi tumenyanyasika sana.
NHIF wanakata madai wanavyotaka na wakikata ni mwanzo mwisho Hutuna mahala kulalamika au kukata rufaa.
Sisi kituo chetu tumepata shida sana mkataba ulipokwisha hatukutamani kuomba tena, bora twende na hao Wateja wachache kuliko kufanya hasara.NHIF Mungu anawaona.
 
Au Nasema uongo ndugu zanguu
 
Mitano tena ili wanyonge wawe mabilionea.
Nina wasiwasi yawezekana jamaa ameshakwanyua hela, hivyo hawawezi kulipa kama inavyotakiwa. Yahani inaenda kuwa kama mifuko ya hifadhi za jamii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…