Mkuu. Sifanyi kazi NHIF ila najua jinsi utaratibu wa kadi za NHIF unavofanyika mavyuoni.
Mwanafunzi akishalipa ile hela (50,400/=) anapewa formu ya kujaza na anabandika picha (passport size).
Zinakusanywa kwa Dean of Students (au muhusika yoyote kutegemeana na Chuo) halafu uyo muhusika ana hakiki majina ya hao waliolipa na form maana mwingine anaweza kusanya tu form bila kulipa.
Akiridhia anapeleka excel yenye taarifa za hao wanafunzi (jina, jinsia, picha, reg no, tarehe ya kuzaliwa etc) NHIF ofisi zao huku akiwa na risiti ya malipo kutokana na idadi ya wanafunzi waliolipiwa.
NHIF watatoa muda kadhaa labda mwezi mmoja au miwili ndio wataanza kutoa izo ID kwa batch.
Sijaona tatizo zaidi kusema labda zinacheleweshwa wangetafuta njia mbadala. Ila kuanzia mwaka wa pili ni easy wana renew tu ile ile kadi hadi atakapo maliza Chuo.
Hii huduma imewasaidia sana wanafunzi ambao walikua hawana kadi kwahiyo tuwapongeze NHIF pamoja na changamoto ndogondogo.