NHIF yafuta Bima ya Afya kwa watoto "TOTO Afya Kadi". NHIF yadai hawajafuta ila wameboresha

NHIF yafuta Bima ya Afya kwa watoto "TOTO Afya Kadi". NHIF yadai hawajafuta ila wameboresha

Habari za awali zinadai kwamba Mfuko wa Taifa wa BIma ya Afya umefuta rasmi bidhaa ya "Toto Afya Kadi" iliyokuwa inatolewa na mfuko huo kwa watoto wa chini ya miaka 18 wanaosajiliwa ili kuwawezesha kupata huduma za matibabu katika vituo vilivyosajiliwa na NHIF nchi nzima.

Ikumbukwe kuwa Toto Afya Kadi ilikuwa inatoa nafasi kwa watoto chini ya miaka 18 kutibiwa kwa gharama ya Tsh. 50,400/= kwa mwaka mzima.

Lakini miongozo iliyotoka hivi karibuni inaonesha kuwa mwanachama aliyekuwa akitibiwa kwa bima hii hawezi kufanya malipo mapya pale bima yale inapokwisha muda wa matumizi (hawezi kurenew).

Hivyo ni kama imeondolewa kimyakimya na hata ukitaka kulipia Bima hiyo hivi sasa wanakwambia kuwa huduma haipo.

======

NHIF yatoa ufafanuzi kuwa hawajafuta kifurushi cha Toto Afya ila wameboresha ili na wazazi wao waingie.

?round hii round hii....
Naenda kuaibika na hawa watoto wa nje ya ndoa
 
Kuna "New members" wamejiunga humu .. na wanachangia kwa kasi kweli kweli
 
Lengo wanataka waondoe mchangiaji mmoja mmoja, wanataka waweke nguvu kwenye shule kila mwanafunzi lazima awe na lazi, wakifanya hivyo watapata wachangiaji milioni 10 kwa mwaka ambao watagenerate zaidi ya Bilioni 50

Lengo lao ni wachangiaji wawe wengi.

Wanaondoa ile ya mtu 1 kukatiwa
Unawatetea Nini hao au we ndo chawa wao 50400 ilikuwa nafuu sana naona mafisadi papa awamu hii mmeamua kutunyonga kabisa fuckin
 
Back
Top Bottom