Ni aibu gani umeshawahi kupata kwenye maisha yako??

Ni aibu gani umeshawahi kupata kwenye maisha yako??

Baada ya kupata ajira nikianza kuwa mlevi wa kutupwa halafu nilikuwa najitamba kuwa nina pesa chafu, sikukumbuka habari ya kujenga nyumba yangu ili nikistaafu nisitaabike.

Mwaka mmoja kabla ya kustaafu nikianza kujenga nyumba ambayo ingekuwa ya kupangisha mungu si Monetary doctor nyumba ikafika katika kiwango lenta lakini isivyo bahati muda wa kustaafu uliwadia.

Nilijisemea kuwa kiinua mgongo changu kitanisaidia kumalizia lakini mambo yalikwenda kinyume na matarajio kwani nilizidisha pombe maradugmfu, nilikuwa nawanywesha marafiki na nilikuwa najitamba hata nikajibatiza kwa jina la Dewji lakini pension nayo iliisha mazima.

Siku moja nilibanwa na njaa kali isiyo na mfano na mfukoni nilikuwa na TSH 1000 niliingia kwenye mgahawa ambao chakula cha bei ya chini kilikuwa TSH 1500 nacho ni ugali. Mazungunzo baina yangu na maman'tilie yalikuwa hivi.

MMI: ugali shilingi ngapi.

MAMAN'TILIE: 1500.

MIMI: (huku nilimpa 1000) hebu naomba unipatie ugali bila mboga.

MAMAN'TILIE: Khah kwa hiyo hutaki mboga au huna hela.

MIMI: Nina hela sema Leo nimeamua Kula ugali peke yake maana katika dunia hii hakuna chakula ambacho sijawahi kula ila ugali bila mboga.

Kumbe watu walikuwa pale mgahawani walikuwa wananisikia, walinicheka na kuanza kunikebehi, yaani siku hiyo niliona aibu ambayo sijawahi kuona mpaka miguu ilikosa nguvu.
Kuanguka na wali assembly nikiwa olevel nimetoka staff kuchukua wali nilipewa na madam wangu,

Eh bhana sikuinuka nililala pale pale mpk nikaja nyanyuliwa 😂 nikijidai nimezima
 
Niliambiwa nimemchafua baada ya tendo 😭😭 sitasahau
 
Mimi O level nilikuaga kwenye Debating club sasa tukawa tumeenda kushindana na shule ya mademu. Sisi tulikua tuna propose afu wao wanaoppose motion. Usiku wakati naandaa points nikajichanganya nikaandaa points za ku-oppose motion ,afu kesho yake mi ndio nilikua first speaker na bahati mbaya nilichelewa ile warm up na wenzangu so hakuna alojua naenda kinyume. Tumefika ukumbini watu wamejaa hadi nje wengine wanachungulia madirishani nikashangaa baada ya introduction nainuliwa kama first speaker to propose the motion. Yale mawenge sijawahi yapata aisee hata sikuelewa nimefikaje kwenye kipaza sauti. Kilichofuata hapo ni kituko cha karne maana sio kwa aibu ile mbele ya mademu mpaka wenzangu wakahisi nimerogwa. Ile aibu sikuwahi tia mguu kwenye mashindano tena maana nilisababisha team yetu kuzomewa vibaya sana
Kwakuwa tu ilikuwa o level. Ila kwingineko kila jibu ni jibu inategemea unaliteteaje. Hapakuwa na aibu yyte
Pole
 
Daaaah juzi nlikua kwenye Harusi nkakanyaga Waya kwa Bahati mbaya Mziki ukazima

X wangu Aka ropoka
Huyo ndio Alivyo Akiona Chakula hatulii sehemu moja 😄 🤣 😂
 
Back
Top Bottom