Tangu awamu ya tano tumekuwa na kasumba ya kuandaa sherehe kupokea ndege au kupokea miradi lakini kwa mtizamo wangu mimi mtu wa chini ninaona kama fedheha fulani.
Nilitegemea serikali kuona kitu kama ununuzi wa ndege ni kitu kidogo ambacho hakihitaji kuandaliwa sherehe ya kuhudhuriwa na mkuu wa nchi.
Tunayo safari ndefu na hapa tulipo tutatakiwa kujivunia mambo gani? Miaka ya 60 labda ndiyo miaka ya mkuu wa nchi kupokea ndege kwa sherehe.
Nikitazama nchi yetu naona tunayo miaka mamia kabla ya kupiga hatua za uhakika kwa sababu tunaweka magoli yetu kwenye mambo mambo madogo na kuyashangilia hayo.
Mfano Leo hii nikipita nchi nzima kumejaa wakandarasi wa kichina wakijenga miradi mbalimbali na ukingiia kwenye miradi hii unakuta kazi zote wanafanya wachina wenyewe. wameajiriwa vijawa wachache kutoka vyuo vyetu vya ufundi na hawa hawafanyi kazi za ujenzi wa miradi bali ni kutafuta vibali, kwenda tanroad kufanya tests za materials, kuandaaa orodha za wafanya kazi n.k
Ujenzi huu wa kichina umekuwepo nchini kwa miaka na bado hatujafanikiwa kujifunza chochote lakini kila mwaka viongozi huandaa sherehe za kupokea miradi. utaendelea kuwepo kwa miaka kadhaa ijayo maana hatuna plan ya watu wetu kujifunza na kuanza kufanya.
Binafsi ningependa kuona zama hizi tunatoka kwenye kasumba au fikra za viongozi wetu wa miaka ya 60 na tunajikita katika kutafuta watanzania leo hii wafanye nini ili kuwa washindani katika dunia na haya ndiyo tuandae sherehe kubwa kusherehekea.