Ndiyo ununuzi wa ndege kinaonekana ni kitu kidogo kwa nchi lakini kina maana kubwa sana miaka ya hivi karibuni hasa baada ya miaka takribani 20 ya kufa kwa kila kitu kilichotambulisha nchi yetu kitaifa na kimataifa.
Viwanda vyote vilivyotengeneza Made in Tanzania waliviua.
Usafiri wa treni uliosafirisha bidhaa za kilimo kwa gharama nafuu toka pande zote za Tanzania mliziua.
Usafiri wa ndege kupitia ATCL nazo mkaziua.
Hadi shule zetu kongwe kidogo mziue.
Ni baada ya JPM kuingia na kuanza takribani kuamsha roho ya utaifa na kuanza kufufua karibu kila kitu.
Kwa muktadha huu kusheherekea hakuepukiki.