Ni aibu kuandaa sherehe za kupokea ndege

Tangu awamu ya tano tumekuwa na kasumba ya kuandaa sherehe kupokea ndege au kupokea miradi lakini kwa mtizamo wangu mimi mtu wa chini ninaona kama fedheha fulani.

Nilitegemea serikali kuona kitu kama ununuzi wa ndege ni kitu kidogo ambacho hakihitaji kuandaliwa sherehe ya kuhudhuriwa na mkuu wa nchi.

Tunayo safari ndefu na hapa tulipo tutatakiwa kujivunia mambo gani? Miaka ya 60 labda ndiyo miaka ya mkuu wa nchi kupokea ndege kwa sherehe.

Nikitazama nchi yetu naona tunayo miaka mamia kabla ya kupiga hatua za uhakika kwa sababu tunaweka magoli yetu kwenye mambo mambo madogo na kuyashangilia hayo.

Mfano Leo hii nikipita nchi nzima kumejaa wakandarasi wa kichina wakijenga miradi mbalimbali na ukingiia kwenye miradi hii unakuta kazi zote wanafanya wachina wenyewe. wameajiriwa vijawa wachache kutoka vyuo vyetu vya ufundi na hawa hawafanyi kazi za ujenzi wa miradi bali ni kutafuta vibali, kwenda tanroad kufanya tests za materials, kuandaaa orodha za wafanya kazi n.k

Ujenzi huu wa kichina umekuwepo nchini kwa miaka na bado hatujafanikiwa kujifunza chochote lakini kila mwaka viongozi huandaa sherehe za kupokea miradi. utaendelea kuwepo kwa miaka kadhaa ijayo maana hatuna plan ya watu wetu kujifunza na kuanza kufanya.

Binafsi ningependa kuona zama hizi tunatoka kwenye kasumba au fikra za viongozi wetu wa miaka ya 60 na tunajikita katika kutafuta watanzania leo hii wafanye nini ili kuwa washindani katika dunia na haya ndiyo tuandae sherehe kubwa kusherehekea.
Acheni unafiki na chuki. Mbona mkinunua magari mapya mnayafanyiea sherehe? Mwenye mali ana haki ya kupokea kitu chake atakavyo. Acheni wivu wa kike.
 
Kumbe kuna sherehe inaendelea huko!mambo mengi muda mchache kwa kweli[emoji1][emoji1][emoji1]
 
Tangu awamu ya tano tumekuwa na kasumba ya kuandaa sherehe kupokea ndege au kupokea miradi lakini kwa mtizamo wangu mimi mtu wa chini ninaona kama fedheha fulani.

Nilitegemea serikali kuona kitu kama ununuzi wa ndege ni kitu kidogo ambacho hakihitaji kuandaliwa sherehe ya kuhudhuriwa na mkuu wa nchi.

Tunayo safari ndefu na hapa tulipo tutatakiwa kujivunia mambo gani? Miaka ya 60 labda ndiyo miaka ya mkuu wa nchi kupokea ndege kwa sherehe.

Nikitazama nchi yetu naona tunayo miaka mamia kabla ya kupiga hatua za uhakika kwa sababu tunaweka magoli yetu kwenye mambo mambo madogo na kuyashangilia hayo.

Mfano Leo hii nikipita nchi nzima kumejaa wakandarasi wa kichina wakijenga miradi mbalimbali na ukingiia kwenye miradi hii unakuta kazi zote wanafanya wachina wenyewe. wameajiriwa vijawa wachache kutoka vyuo vyetu vya ufundi na hawa hawafanyi kazi za ujenzi wa miradi bali ni kutafuta vibali, kwenda tanroad kufanya tests za materials, kuandaaa orodha za wafanya kazi n.k

Ujenzi huu wa kichina umekuwepo nchini kwa miaka na bado hatujafanikiwa kujifunza chochote lakini kila mwaka viongozi huandaa sherehe za kupokea miradi. utaendelea kuwepo kwa miaka kadhaa ijayo maana hatuna plan ya watu wetu kujifunza na kuanza kufanya.

Binafsi ningependa kuona zama hizi tunatoka kwenye kasumba au fikra za viongozi wetu wa miaka ya 60 na tunajikita katika kutafuta watanzania leo hii wafanye nini ili kuwa washindani katika dunia na haya ndiyo tuandae sherehe kubwa kusherehekea.
Watz hawawezi kufanya kitu kikafanikiwa hilo alishajaribu magu akiwa na wazo kama lako na akachemka.
Keshawahi wapa Kazi za ujenzi wa majengo shirika la ujenzi wakashindwa
 
Ndege 11 unaajiri watu 580 siriasi kweli? Fedha za kununulia ndege tu zinanunua treka laki 3 ambazo zinatoa ajira kwa vijana milioni 12 nchi nzima na kuondoa au kumaliza kabisa tatizo la machinga mijini.
Wakishatumia vibaya kodi zetu wanaenda kuwadanganya watu eti wazungu ndio wametuletea umasikini hizi ni chuki kabisa.
Sidhani kama kuna ccm ataingia peponi aisee.
 
Ndiyo ununuzi wa ndege kinaonekana ni kitu kidogo kwa nchi lakini kina maana kubwa sana miaka ya hivi karibuni hasa baada ya miaka takribani 20 ya kufa kwa kila kitu kilichotambulisha nchi yetu kitaifa na kimataifa.

Viwanda vyote vilivyotengeneza Made in Tanzania waliviua.
Usafiri wa treni uliosafirisha bidhaa za kilimo kwa gharama nafuu toka pande zote za Tanzania mliziua.
Usafiri wa ndege kupitia ATCL nazo mkaziua.
Hadi shule zetu kongwe kidogo mziue.

Ni baada ya JPM kuingia na kuanza takribani kuamsha roho ya utaifa na kuanza kufufua karibu kila kitu.

Kwa muktadha huu kusheherekea hakuepukiki.
Nikurekebishe kidogo. Hii nchi toka inapata Uhuru Hadi Sasa imetawaliwa na chama kimoja TANU/CCM. so, aliyeua viwanda na shirika la ndege ndo huyo huyo aliyekuja kufufua.
 
Chama gani kiliua we nguruwe pori
 
Tusiandae sherehe kuipokea ndege tuliyonunua KATIKATI YA JANGA LA CORONA?!!

Dunia nzima hakuna nchi iliyotoa FEDHA ZAKE kununua NDEGE...ni uthubutu pekee wa Tanzania ...kutokuweka LOCKDOWNS kunatupa nguvu ya KUIPOKEA NDEGE HII/HIZI kwa sherehe ndogo.

#SiempreTanzania
#SiempreCCM
#NchiKwanzaKablaYaNafsiZetu
#KaziIendelee
Hela ya kuweka mitungi ya gas kila hospital hakuna alafu umeaharisha upuuzi
 
Nikurekebishe kidogo. Hii nchi toka inapata Uhuru Hadi Sasa imetawaliwa na chama kimoja TANU/CCM. so, aliyeua viwanda na shirika la ndege ndo huyo huyo aliyekuja kufufua.
Umeongea vyema. Kumbe suala hapa si aina ya chama. Suala ni aina ya watu.

Mi si muumini wa CCM au Chadema au TLP au nani sijui. Mi ni muumini wa mtu mwenye moyo sahihi kwa ajili ya nchi na watu wake. Mtu huyo akipatikana TANU sawa, akipatikana CCM sawa, akipatikana Chadema sawa.
 
Kama ATCL yenyewe haijawahi kupata faida toka ndege zianze kununuliwa, je hii sherehe ya kupokea ndege si uthibitisho wa kusherehekea hasara? Ni kama vile wapo watu wanafurahia nchi kufilisika!
 
Hela ya kuweka mitungi ya gas kila hospital hakuna alafu umeaharisha upuuzi
Basi tufanye hivi....

Tununue mitungi tuijaze mpaka zahanati....halafu uone sehemu nyingine zitakavyoathirika....sina maana kuwa tusizijali hospitali zetu....

Kwa taarifa yako ni kuwa si kila kitu cha afya kunalazwa wagonjwa wa UVIKO....wagonjwa wengine mahututi.....

Amka Meku🤣🤣
 
Tungekuwa nazo zaidi ya 150 kama Ethiopian Airlines sijui nchi ingehama na huko Ethiopia hata zinapoletwa hakuna anayefahamu huenda hata watumishi wengi wa shirika hawajui.

Sasa nini faida ya kuleta ndege wakati hazitumiki zinabaki kupaki kisa zinaweza kukamatwa kwa sababu nchi inadaiwa madeni ya dhuluma.
 
Kupanga ni kuchagua, hakuna anayelazimishwa, BTW mazingara vile vile ni tofauti wacha ushamba.

Ni kweli hapa kwetu bado ulimbukeni ni mkubwa, tofauti na huko south Africa. Ila majizi ya kura ya hayaishi vituko.
 
Tangu awamu ya tano tumekuwa na kasumba ya kuandaa sherehe kupokea ndege au kupokea miradi lakini kwa mtizamo wangu mimi mtu wa chini ninaona kama fedheha fulani.

Nilitegemea serikali kuona kitu kama ununuzi wa ndege ni kitu kidogo ambacho hakihitaji kuandaliwa sherehe ya kuhudhuriwa na mkuu wa nchi.

Tunayo safari ndefu na hapa tulipo tutatakiwa kujivunia mambo gani? Miaka ya 60 labda ndiyo miaka ya mkuu wa nchi kupokea ndege kwa sherehe.

Nikitazama nchi yetu naona tunayo miaka mamia kabla ya kupiga hatua za uhakika kwa sababu tunaweka magoli yetu kwenye mambo mambo madogo na kuyashangilia hayo.

Mfano Leo hii nikipita nchi nzima kumejaa wakandarasi wa kichina wakijenga miradi mbalimbali na ukingiia kwenye miradi hii unakuta kazi zote wanafanya wachina wenyewe. wameajiriwa vijawa wachache kutoka vyuo vyetu vya ufundi na hawa hawafanyi kazi za ujenzi wa miradi bali ni kutafuta vibali, kwenda tanroad kufanya tests za materials, kuandaaa orodha za wafanya kazi n.k

Ujenzi huu wa kichina umekuwepo nchini kwa miaka na bado hatujafanikiwa kujifunza chochote lakini kila mwaka viongozi huandaa sherehe za kupokea miradi. utaendelea kuwepo kwa miaka kadhaa ijayo maana hatuna plan ya watu wetu kujifunza na kuanza kufanya.

Binafsi ningependa kuona zama hizi tunatoka kwenye kasumba au fikra za viongozi wetu wa miaka ya 60 na tunajikita katika kutafuta watanzania leo hii wafanye nini ili kuwa washindani katika dunia na haya ndiyo tuandae sherehe kubwa kusherehekea.
Ni jambo la kujivunia unapoona kuja kwa Mali ya nchi ambayo imegharimu pesa nyingi
 
Back
Top Bottom