Huyu dikteta mpya anacopy na ku paste mambo ya dikteta wa aliyeenda zakeTangu awamu ya Tano tumekuwa na kasumba ya kuandaa sherehe kupokea ndege au kupokea miradi lakini kwa mtizamo wangu mimi mtu wa chini ninaona kama fedheha fulani...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyu dikteta mpya anacopy na ku paste mambo ya dikteta wa aliyeenda zakeTangu awamu ya Tano tumekuwa na kasumba ya kuandaa sherehe kupokea ndege au kupokea miradi lakini kwa mtizamo wangu mimi mtu wa chini ninaona kama fedheha fulani...
Je ulimsahau aliezindua mkokoteni kulee 77?kuna yule alifanya sherehe ya zindua daraja la mbao juzi.
n
ni aibu kwako, ila kwetu, kuna advertisement kibiashara imeshafanyika hapo. tuache tusherehekee.
Yaani wakati mwingine huwa najiuliza,kwa mtindo wetu huu maridadi,wa kwenda kupokea ndege kila zinaponunuliwa, kwa nchi kama SA, Kenya, Ethiopia,Eghypt nk.Ndiyo ununuzi wa ndege kinaonekana ni kitu kidogo kwa nchi lakini kina maana kubwa sana miaka ya hivi karibuni hasa baada ya miaka takribani 20 ya kufa kwa kila kitu kilichotambulisha nchi yetu kitaifa na kimataifa...
Usitegemee mabadiliko ukiwa na ceremonial leaders, wao sikukuu ndiyo fahari, jifunze kwenye vigodoro, mtu anaishi kwenye nyumba mbavu za mbwa lakin siku ya kumtoa mwali au kigodoro, anauza shamba,Tangu awamu ya Tano tumekuwa na kasumba ya kuandaa sherehe kupokea ndege au kupokea miradi lakini kwa mtizamo wangu mimi mtu wa chini ninaona kama fedheha fulani...
Kupanga ni kuchagua, hakuna anayelazimishwa, BTW mazingara vile vile ni tofauti wacha ushamba.Yaani wakati mwingine huwa najiuliza,kwa mtindo wetu huu maridadi,wa kwenda kupokea ndege kila zinaponunuliwa, kwa nchi kama SA, Kenya, Ethiopia,Eghypt nk.nafikiri marais wao na wananchi wao kila leo wangekuwa busy kwenda kwenye airport zao kupokea ndege mpya....btw kupanga ni kuchagua na kazi iendelee.
Na kwenda kuzindua madaraja/flyoverskwenda kupokea ndege kila zinaponunuliwa, kwa nchi kama SA, Kenya, Ethiopia,Eghypt
Kumbe CHANGAMOTO iko kwenye hulka za watanzania....sasa tutegemee SERIKALI itoke mbinguni?Usitegemee mabadiliko ukiwa na ceremonial leaders, wao sikukuu ndiyo fahari, jifunze kwenye vigodoro, mtu anaishi kwenye nyumba mbavu za mbwa lakin siku ya kumtoa mwali au kigodoro, anauza shamba...
😁Hata mimi niliwashangaa Chadema kuandaa sherehe ya kumpokea Lisu uwanja wa ndege siku ile. Matokeo yake sherehe ilibuma.
Michango ya kuwachangia kina Lisu imeshaleta jita gani kwa wachangaji na chama kwa ujumla?Zimeanza kuleta faida ? au hii ikishafika ndio faida itapatikana ?
LIsu anachangiwa na Kodi? Kama ni wanachama na watu wake mimi inanihusu nini kuhoji ?, Ila kwenye hili ni Kodi zangu pia kwahio lazima niojiMichango ya kuwachangia kina Lisu imeshaleta jita gani kwa wachangaji na chama kwa ujumla?
Mapokezi ujue pia ni promotion na shirika kutangaza limeongeza ndege. Pia kisiasa hakuna ubaya serikali na chama tawala kuonesha mafanikio yake.Tangu awamu ya tano tumekuwa na kasumba ya kuandaa sherehe kupokea ndege au kupokea miradi lakini kwa mtizamo wangu mimi mtu wa chini ninaona kama fedheha fulani.
Nilitegemea serikali kuona kitu kama ununuzi wa ndege ni kitu kidogo ambacho hakihitaji kuandaliwa sherehe ya kuhudhuriwa na mkuu wa nchi.
Tunayo safari ndefu na hapa tulipo tutatakiwa kujivunia mambo gani? Miaka ya 60 labda ndiyo miaka ya mkuu wa nchi kupokea ndege kwa sherehe.
Nikitazama nchi yetu naona tunayo miaka mamia kabla ya kupiga hatua za uhakika kwa sababu tunaweka magoli yetu kwenye mambo mambo madogo na kuyashangilia hayo.
Mfano Leo hii nikipita nchi nzima kumejaa wakandarasi wa kichina wakijenga miradi mbalimbali na ukingiia kwenye miradi hii unakuta kazi zote wanafanya wachina wenyewe. wameajiriwa vijawa wachache kutoka vyuo vyetu vya ufundi na hawa hawafanyi kazi za ujenzi wa miradi bali ni kutafuta vibali, kwenda tanroad kufanya tests za materials, kuandaaa orodha za wafanya kazi n.k
Ujenzi huu wa kichina umekuwepo nchini kwa miaka na bado hatujafanikiwa kujifunza chochote lakini kila mwaka viongozi huandaa sherehe za kupokea miradi. utaendelea kuwepo kwa miaka kadhaa ijayo maana hatuna plan ya watu wetu kujifunza na kuanza kufanya.
Binafsi ningependa kuona zama hizi tunatoka kwenye kasumba au fikra za viongozi wetu wa miaka ya 60 na tunajikita katika kutafuta watanzania leo hii wafanye nini ili kuwa washindani katika dunia na haya ndiyo tuandae sherehe kubwa kusherehekea.