Yanga bado mnaumia kutopewa nafasi. Hawawezi kutoa nafasi kwa timu ambayo ni kama imefluck to kuruka nafasi hadi kufikia hapo. Hao Enyimba na Mazembe wakati wako kwenye peak walikuwa na muendelezo mzuri na walifika mbali kwenye MASHINDANO YA KLABU BINGWA kwa hiyo rekodi hizo zipo na zinaheshimiwa.
Yanga ili muheshimiwe na kuaminiwa inabidi muwe na muendelezo. Sasa wakiwaangalia klabu bingwa hamjaingia hatua ya makundi kwa miaka 25, si afadhali wawafikirie hata Vipers. Tunawasemaga hapa mnaona sisi wajinga au tuna wivu na chuki hamtaki kukubali ukweli.
Pia kumbukeni kwenye hii AFL ya kwanza, wamechukua timu moja kutoka kila ukanda. Sasa hivi wanaumiza kichwa hao Atletico wa Angola wakitolewa itakuwaje ila usishangae Yanga ikaachwa na kupewa nafasi Vipers, AS Vita au hata Power Dynamos. Hapo hapo kuna Algeria bado hawana muwakilishi, Raja, Pyramids.