Ni aibu kwa Media, Waziri na Wachambuzi wa Michezo kutoa maamuzi Goli la Yanga bila kujiridhisha

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2022
Posts
1,414
Reaction score
3,118
Mpira ni kitu cha Duara hivyo unapotua chini ni sehemu ndogo tu ya mpira inagusa ardhi sehemu kubwa inakuwa hewani .

Kwa maana nyingine ukiwa upande mmoja unaweza ona mpira umevuka lakini ukiangalia kutoka juu ukawa bado haujavuka wote .

Na kwa maana rahisi ni kwamba VAR pia haiwezi kuwa sahihi sana pia ila ni GOAL LINE TECHNOLOGY tu ndio yenye uhakika kwa hapa .

Waziri, Wachambuzi wameconclude moja moja kuwa ni Goli

Yanga nao kwa haraka haraka wamejirizisha ni goal kwa kutumia video na image chache tu

Kulingana na Experts wa VAR Jerome Damon ..“Without GLT (Goal line technology) it’s impossible for VAR to say goal or no goal – one can speculate either way but cannot be 100% sure,” .

Hapa tumekosa
1.Goal line technology kitu ambacho ni muhimu
2.hatuna hata videos ambazo zinaonesha mpira katika pembe tofauti tofauti
Your browser is not able to display this video.

Hapa video ya juu ina angle tofauti inaonesha mpira vizuri goli letu halina

Your browser is not able to display this video.

Hapa technology imetumika
Na ni bora siasa isiingilie Mpira​
 
Nimemsikia Mlevi mmoja wa Clouds Media wa Kuitwa DAKOTA akiutangazia Umma kwamba siku MOTSEPE akija Tanzania tummalize! Nikajisemea this is too much now, ambao hawakuskia hii watafute kipindi cha saa 6 usiku cha Clouds mambo ya Rhumbba.

Yule Naibu Wazir naye kiaziiii hajui hata Diplomacy anaropoka kama anaimba taarabu tuu. Kuna namna ya kuongea kama Kiongozi siyo anatanguliza mihemko na ushabiki mwishowe wanaharibu.
 
Mashabiki wafia timu zao huwa wanaendeshwa na hisia na mahaba zaidi kuliko uhalisia.
 
😆😆😆😆tuna safari ndefu
 
Sasa kama hakuna goal line technology, refa aliamuaje kuwa lile sio goli wakati sote tunaona mpira ulivuka mstari kwa 100%?
Kwanini hakuamua ni goli ili tusimchallenge?
 
kama kuna mtu aliangalia game ya totteham na luton anaweza akasema sisi wa Tanzania bado sana kwenye sheria mpya zinazotoka kila kukicha za mpira
 
Shida unafanya uchambuzi ukiwa umevaa koti la Simba. Vua koti la Simba au Yanga, halafu ndio utachambua vizuri.
 
Njoo na hoja ya msingi ya kutushawishi kuwa lile sio goli, maana hata sisi wana Simba tulioangalia ile mechi tuliona lile ni goli kwa 100%, sasa kama kuna hoja ya msingi ya kusema tofauti, tunaingoja kwa hamu ili tuwanange vilivyo utopolo, otherwise wanaSimba wote tutaonekana ni mbumbumbu kukataa sio goli.
 
Camera zipo nyingi sana pia VAR haikutumika hata hiyo video iliyopo inaonyesha mpira ulivuka zaidi ya cm 30 kutoka kwenye goal line pengine labda wewe unavideo yako peke yako
Kolo lina video yake aliyerekodi ni Ahmed Ally.

Kwenye hiyo video yake mpira hupo nje ya mstari.
 
Huu sasa ndio uchambuzi. Tuwasubiri utopolo waje kumwaga upupu wao hapa
 
Mnavyolia lia kana kwamba ni nyie peke yenu mmeonewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…