Ni aibu kwa mtumishi wa umma kung'ang'ania ofisi huku umestaafu

Ni aibu kwa mtumishi wa umma kung'ang'ania ofisi huku umestaafu

Arudi kijijini akale pension yake!! Kijijini nyumba ya Tembe bei rahisi tu.
 
Kuna mbaba kazini kwetu dereva kastaafu mwezi June. Cha ajabu bado anaendelea kuja kazini. Kwakuwa kuna uhitaji wa dereva basi ofisi haiwezi kumfukuza. Nimemchana leo kuwa akubali matokeo atulie home asubiri stahiki zake.

Watumishi wa umma tujipange, huyu mzee amestaafu hajajenga nyumba, kumbe hata documents zake muhimu alikuwa anazitunza hapa kazini kimyakimya. Juzi ndipo tuligundua, ningeziona mapema ningezificha ahangaike kwanza mpaka alie ndipo ningempa.

Mtumishi wa serikali unaishi nyumba ya kusitiriwa. Mtu kajenga nyumba anakuambia nilindie nyumba yangu!!

Huyu mzee ukimwambia Jpili nakutembelea lazima akupe udhuru.
Yote Maisha na kujaliwa. Hujui dhiki na taabu wanayopitia Watumishi wa Umma..
 
Watu wengi wanaotoa ushauri kuhusu maisha ya watu,ukifuatilia maisha yao hamna lolote la maana.Waswahili wanasema debe tupu ndio linalopiga kelele.
 
Duh, hiyo roho nyeusi km wale watasha waliompiga roba mweusi mwenzetu mpaka akadanchi!
 
Utakuwa dereva ofisini kwenu, madereva hampendani hadi mnarogana ,so sikushangai kwa roho mbaya juu ya huyo mwenzako
 
Ukimuona mchane tena

Kuna watu watakupinga ila hawafikirii kuwa kuna watu wanakosa ajira kwa uwepo wake,ameshatumikia wakati wake,aachie ofisi ili ofisi iajiri mwingine sasa akiendelea kukaa hakuna atakaeajiriwa..

Oya ukimuona tena mchane

Uzi wake ni mzuri,

Ila angeuwakilisha kwa namna nyingine tofauti kidogo,

Let's say, angeweza kuigeuza hii mada, ikawa kama tahadhari kwa watumishi wote ambao hawako makini katika kuyaandaa maisha yao ya ustaafu baada ya kazi, na hii story ya huyu Mzee angeiweka kama Mfano hai kama ushahidi wa kile alichokizungumza.

Kwa njii hii aliyotumia, ni wachache watakao weza kumwelewa mleta mada huku wengi wakimhisi kama vile ana wivu na Mzee wa watu.

Hivyo tu.

Jamani, kuna maisha baada ya kustaafu.
Tujipange, hicho hicho kidogo, tukigawe.
Ili tuweze kusomesha, kununua kiwanja, kujenga na hata kujipatia mlo wa kila siku nyumbani.

Wakati mwingine tunashindwa kuelewa kuwa mlo uliokamilika ni sehemu muhimu kwa watoto wetu katika kujenga afya bora ya Akili. Hivyo tusiishie tu kuwalaumu watoto wetu kushika mikia mashuleni, tujiulize pia, je tunawapa lishee bora kwa ajili ya kufua/chaji kumbukumbu zao?

Mwisho kabisa, nimalizie kwa kusema hivii, kama wewe ni mtumishi na kipato chako hakieleweki, kwa maana kuwa, hata familia yako unashindwa kuitimizia mahitaji yote muhimu kwa mshahara wako, tuache kabisa mambo ya mitaala.

Walionielewa, wameelewa. Mitaala ndio chanzo cha umaskini katika familia zetu. Sasa ukiniuliza mitaala inasababisha vipi umaskini katika familia, jibu sitoweza kukupa moja kwa moja, ila naweza nikakuagiza, ili uende uka practice, kisha uje na jibu hapa.

Kwa mshahara wako wa graduate wa Tshs laki 7 na nusu kabla ya kodi, nenda kaoe wake wawili halafu kila mmoja umtimizie mahitaji yake vile inavyopaswa.

Kiwanja cha million 5, sijui utakuja kununua mwaka gani baada ya ndoa.
 
Ukimuona mchane tena

Kuna watu watakupinga ila hawafikirii kuwa kuna watu wanakosa ajira kwa uwepo wake,ameshatumikia wakati wake,aachie ofisi ili ofisi iajiri mwingine sasa akiendelea kukaa hakuna atakaeajiriwa..

Oya ukimuona tena mchane
Nonsense!
 
Kuna mbaba kazini kwetu dereva kastaafu mwezi June. Cha ajabu bado anaendelea kuja kazini. Kwakuwa kuna uhitaji wa dereva basi ofisi haiwezi kumfukuza. Nimemchana leo kuwa akubali matokeo atulie home asubiri stahiki zake.

Watumishi wa umma tujipange, huyu mzee amestaafu hajajenga nyumba, kumbe hata documents zake muhimu alikuwa anazitunza hapa kazini kimyakimya. Juzi ndipo tuligundua, ningeziona mapema ningezificha ahangaike kwanza mpaka alie ndipo ningempa.

Mtumishi wa serikali unaishi nyumba ya kusitiriwa. Mtu kajenga nyumba anakuambia nilindie nyumba yangu!!

Huyu mzee ukimwambia Jpili nakutembelea lazima akupe udhuru.
Kumbuka na wewe unazeeka
 
halafu anakukukera wewe kitu gani?? kwa uandish wako unaonesha wewe ni junior officer au dada wa usafi hapo ofisin . hakuendesh wewe na wewe doc zako kisa umeajiriwa masijala ya wazi ndio ufiche. wewe ndio umeonyesha tabia mbaya mlizonazo watu wa masijala ya mawizara mna roh mbaya ya kuficha barua za watu.mtu unakuta anapandishwa cheo au uhamisho muda au mafao mmekalia matako yenu barua zao mnataka vihela vidogo vidogo.
anayeendeshwa mbona hajasema na madereva wengine wanastaafu na cheo cha dereva mwandamizi so anajua kazi yake kiuweled.nyie madereva wapya kaz kusinzia barabaran na bis akiwa kweny vikao wewe unashinda baa

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Poa tu ila nishamchana, miaka 60 bado huchoki kazi. Huku wengine tunatamani kuacha kazi tukafanye mambo mengine ya kibinafsi sema tu sheria ya PSSSF majanga

Wawalipe wastaafu pesa zao on time,wanatesa sana wastaafu.
 
Back
Top Bottom