Ni aibu msomi kufanya biashara ambayo hata asiyesoma anaweza kufanya

Ni aibu msomi kufanya biashara ambayo hata asiyesoma anaweza kufanya

Alafu watu mnakosea kusema mfumo wetu wa elimu haumfundishi mtu kujiajiri....vyuo vingi vina course za ujasiriamali siku hizi katika fani karibia zote.
Angalia hao walimu wanaofundisha ujasiriamali wao wana bizness ganì?
 
Only joking,'inatakiwa wasomi wawatumie wajinga katika kujizalishia kipato,lakini kinachoonekana ni wajinga kuwatumia wasomi katika kujizalishia kipato'kwa hiyo mjinga zaidi ni msomi.
 
Kweli kabisa mkuu, hii imenigusa sana na cha ajabu zaidi unakuta media zinaandaa vipindi vya vijana wasomi walioamua kujiajili kupika keki na kutengeneza sabuni za maji.
Hayo maneno mmeyapata wapi ya kuwapangia maprofesa kazi za kufanya,.Wengine kufuga ni hobi sio kwamba wanategenea kamradi hako kawaboreshee maisha kama nyie.Hivi mmesoma kitabu gani kinachobexa wasomi kufanya shughuli za kawaida.Robert kiwasoki(Rich daf poor dad) anapingana kabisa na mawazo yenu.Waso.u huyhibitisha kwa maandiko.Sasa naombeni maandiko yanayothibitisha msomi asiuze mchicha sokoni, asitembeze maji, asilime nk.
 
Kweli kabisa mkuu, hii imenigusa sana na cha ajabu zaidi unakuta media zinaandaa vipindi vya vijana wasomi walioamua kujiajili kupika keki na kutengeneza sabuni za maji.
Hayo maneno mmeyapata wapi ya kuwapangia maprofesa kazi za kufanya,.Wengine kufuga ni hobi sio kwamba wanategenea kamradi hako kawaboreshee maisha kama nyie.Hivi mmesoma kitabu gani kinachobeza wasomi kufanya shughuli za kawaida.Robert kiwasoki(Rich dad poor dad) anapingana kabisa na mawazo yenu.Wasomi huthibitisha kwa maandiko.Sasa naombeni maandiko yanayothibitisha msomi asiuze mchicha sokoni, asitembeze maji, asilime nk.
 
Huyu naona anaandika ushuzi tu.. post yake haijakaa kiuhalisia kabisaaa maana kwa msomi mtanzania aliesomeshwa kwa mkopo wa serikali na alietokea familia duni huo mtaji wa kufungua banda Kama la KFC atautoa wapi.. ustake watu wakumalizie hasira za ugumu wa Maisha inye wew..
Aiseee
 
Nina wasiwasi na mtoa mada kuwa si mfuatiliaji sana wa mambo. Sijui amechunguza kiasi gani nchi nyingine zenye wasomi wengi wanafanya nn. Si kila msomi lazima afanye biashara. Na kufanya biashara kama ya mangi si kosa. Kila kitu huanzia chini, na anaweza kukua taratibu taratibu mpaka akafika juu. Hata akina bahresa walianza chini tena kwa kupika chapati tu. Kuwa na aidea ni jambo jingine na kuifanikisha ni jingine.
Sijui mtoa mada na usomi wake amebuni mbinu gani mpya hata kama ameajiliwa ili atoe fundisho kwa wasomi wengine.
Nadhan angejaribu kuheshimu mtu kwa kile anachokifanya na kumshauri ili kuboresha kuliko kuleta lawama ambazo ni dharau kwa wengine.
 
Tumekupata, yaani ukisoma watakiwa kufanya biashara unique, ila hapo ni uwezo tofauti wa akili zetu, kuna kitu kimoja nakiona duniani, wale wasiosoma sana au kabisa, nimewaona wakianzisha biashara zenye ubunifu kuliko waliosoma, nadhani kusoma ni hakuhusiani na ubunifu wa baishara...yawezekana sijuwi pia...
 
Kikubwa watu wanaangalia kuingiza kipato...watu hawawekezi au hawafanyi biashara kwa sifa tu....Bakhresa si unamuona anauza juice, chapati, unga etc....kuna wasomi wangapi wanamfikia kifedha hata kwa miradi ya kisomi...

Mie nafikiri umekua na upendeleo.....kikubwa si aina ya biashara mtu anayofanya bali namna ya uendeshaji na maboresho ndo yataweza kutofautisha msomi na asie msomi
 
Hayo maneno mmeyapata wapi ya kuwapangia maprofesa kazi za kufanya,.Wengine kufuga ni hobi sio kwamba wanategenea kamradi hako kawaboreshee maisha kama nyie.Hivi mmesoma kitabu gani kinachobeza wasomi kufanya shughuli za kawaida.Robert kiwasoki(Rich dad poor dad) anapingana kabisa na mawazo yenu.Wasomi huthibitisha kwa maandiko.Sasa naombeni maandiko yanayothibitisha msomi asiuze mchicha sokoni, asitembeze maji, asilime nk.
Upo sawa Mkuu Tangantika, lakini kwa nchi zetu hizi za kiafrika tena zenye wasomi wachache na wenye elimu za kuungaunga alafu wasomi hao hao wasizitumie taaluma zao vyema walizozipata kwa misaada ya serikali, Kodi za wananchi na pesa za wazazi maskini waliouza kila kitu ili wasome, Kisha wanashindwa kukiishi walichokipotezea fedha na muda na kufanya biashara ndogo ndogo zisizolingana hata na elimu yao!! Hii haipo sawa kabisa,maana wakiendelea hivyo nchi yetu itajengwa na wageni kwa kila kitu. Issue ni kwamba waamke waziishi ndoto zao ipasavyo na sio Engineer kujiajiri kufuga samaki Kisha media zinasifia kuwa hachagui kazi, na kumwita mbunifu.
 
Sio kwamba watu wasiuze nguo, ila wauze nguo kwa staili ya kisomi. Idea hizi hizi ila utaratibu uwe wa kisomi. Unaogopa competition mangi?
 
Wasomi wa Tz magumashi sana ....kwanza hawawezi kujifunza maarifa mpya ,kimfano umaweza kum introduce kwenye kitu kipya akaishia kukuita tapeli bila ya kufanya research!
 
Wasomi Vijana, mliosoma elimu kubwa za madigrii na Masta tumekosa ubunifu hakika.
Yashangaza sana, Kijana umesoma IT, Umesoma Engeneering, Uhasibu eti unakuja Mtaani unawaza Kufunga Banda la Chips, sijui Kulima matikiti mara duka la vipodozi ni aibu kubwa.

Haiwezekani, Msomi elie elimika unashindwa kuja na mawazo mbadala ya kusaidia Jamii, kuja na mawazo mapya, kuja na Idea za kisomi, mwishoe umepata ajira unachukua mkopo alafu unawaza kufungua duka la Nguo???

Kibaya sio kufanya biashara hizo hapo nilizosema, kinachosikitisha ni kwamba unazifanya biashara hizo kama mtu ambae hajasoma, hakuna kipya wala ubunifu yani ni vuluvulu tu.

Mimi nashangaa sana, Msomi mzima unawekeza milioni 20 kwenye duka la nguo kama la Mangi ambae kaishia la saba na unaifanya biashara hiyo kama yeye?


Nimeikubali Idea ya Benjamin Fernandez, yule jamaa aliyemaliza Stanford university, kaja na Idea ambayo zilikuwepo lakini kaboresha kidogo na sasa ni mwendo wa kupiga pesa tu.

Embu tuacheni Idea za Ajabu, sijui kulima tikiti, sijui juisi ya Muwa, tuje na Idea solid ambayo asilimia kubwa inakuwa ni service business na sio manufacturing ambazo asilimia kubwa ni hasara tu.

Nakaribisha majadiliano,
Beza ni beza tu mura hata kwa kuuza madikiti mura....acha hizo Meku, kwanza unaitwa Moshi ukatambike aka kuhesabiwa.
 
Back
Top Bottom