Ni aibu msomi kufanya biashara ambayo hata asiyesoma anaweza kufanya

We endelea kukaa nyumbani kusubir ajira, acha sisi watu wa darasa la saba tuendelee kupiga pesa
We angaika na vitabu na makaratasi
Sisi tupo bize na miamala ya pesa.
 
Ndo maana wasomi wanakua masikini wa kutupa
 
Naona wengi mmemjibu jamaa kwa hasira. Nadhani ni kutokana na kuwa amewagusa na binadamu muda wote hatutaki kujilaumu, tunatupia lawama kwa wengine.

Mtoa mada kaandika kabisa kuwa tatizo siyo kufanya hizo biashara ndogo alizozitaja, tatizo ni kushindwa kutumia elimu yako kuongeza thamani.

Fanya biashara anayofanya mtu aliyeishia la saba, lakini ongeza thamani. Keep records za mauzo yako, weka sehemu yako safi, target wateja wako vizuri.

Faida kubwa ya elimu ni kufungua mawazo, kuipa ubongo wako uwezo wa kufikiri na kuchambua mambo. Bila hivyo unakuwa umesoma ila hujaelimika.

Itumie elimu yako kufanya biashara ile ile kama wengine, ila kwa utofauti. Hicho ndo naona wengi mnajifanya hamja kiona kwenye mada ya jamaa.

Yaani genge la mchoma chipsi asiyesoma na wewe uliyesoma hakuna tofauti. Haweki records za mauzo na wewe uweki. Hawezi kuwashikilia wateja na wewe mule mule.

Lugha chafu kwa wateja na wewe yale yale. Anatumia zana za zamani kuendesha biashara na wewe mule mule. Yaani huongezi chochote. Hilo ndo tatizo.

Mtu akikutazama wewe msomi na yule asiyesoma haoni tofauti.
 
Wee endelea na innovation sisi tunaangalia wapi pesa inapatikana full stop. Ya nini niumize kichwa akati kuna biashara rahisi ya kupiga mpunga.heshima pesa zingine mbwembwe tu.nbona hujahoji maprof kugombea ubunge na Kusifia ovyoovyo.
Innovation waachie wachina na wahindi ambako fursa hata za kulima tikiti ni za kulenga na manati.
 
Mfano!?
 
Uzuri ni kwamba ukiwa la saba ukajifanya unaenda kufanya kazi za wasomi unakamatwa ndani (mfano madaktari feki muhimvili)! Lakini ukiwa msomi ukaenda kujiunga na kazi za la saba ni murua tu!
 
Kambi popote njomba; unachagua kazi utakula degree?
 
"Service business na sio manufacture".
Point kubwa kuliko hata na ulichokiandika, asante mkuu.
 
Uwezo wako wa kufikiri ni mdogo sana
 
Kwan ukiwa unafanya kaz bank au tra na CPA yako af unakua unajaza ma file tuu au kufungulia watu accounts au bank teller au kujazia watu fomu za makadirio ya kodi,hyo si kaz hata mtoto wa darasa la saba anafanya kiongoz?

Kiongoz nahis hujayajua maisha na nahis bado ni mchanga sana kwenye utaftaj

Hujui vtu rahis ndivyo vinaingiza pesa,bakhresa anauza unga,pip, juic, nazi

Bas angefanya biashara ya kurusha roket au sio..

Nahis bado mchanga sana,ukikua utaelewa..
 
Mtoa mada wewe unafanya biashara gani kisomi?
 
Mkuu katika maisha yako usidharau kaz za watu mm mwenyew sijasoma na mimeajiri hao hao wasomi wako na wanapanga foleni kila mwez
 
Kila mtu apambane na hali yake.

Kwani mtu akiwa msomi halafu akaamua kuuza chipsi wewe unaumia nini??

Kipindi anasoma ulimsaidia japo pesa ya kununua daftari na kalamu????


Mr Bean ni injinia lakini aliamua kuweka pembeni uinjinia wake na kuamua kuwa mchekeshaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…