Ni aibu msomi kufanya biashara ambayo hata asiyesoma anaweza kufanya

Ni aibu msomi kufanya biashara ambayo hata asiyesoma anaweza kufanya

Wasomi Vijana, mliosoma elimu kubwa za madigrii na Masta tumekosa ubunifu hakika.
Yashangaza sana, Kijana umesoma IT, Umesoma Engeneering, Uhasibu eti unakuja Mtaani unawaza Kufunga Banda la Chips, sijui Kulima matikiti mara duka la vipodozi ni aibu kubwa.

Haiwezekani, Msomi elie elimika unashindwa kuja na mawazo mbadala ya kusaidia Jamii, kuja na mawazo mapya, kuja na Idea za kisomi, mwishoe umepata ajira unachukua mkopo alafu unawaza kufungua duka la Nguo???

Kibaya sio kufanya biashara hizo hapo nilizosema, kinachosikitisha ni kwamba unazifanya biashara hizo kama mtu ambae hajasoma, hakuna kipya wala ubunifu yani ni vuluvulu tu.

Mimi nashangaa sana, Msomi mzima unawekeza milioni 20 kwenye duka la nguo kama la Mangi ambae kaishia la saba na unaifanya biashara hiyo kama yeye?

Nimeikubali Idea ya Benjamin Fernandez, yule jamaa aliyemaliza Stanford university, kaja na Idea ambayo zilikuwepo lakini kaboresha kidogo na sasa ni mwendo wa kupiga pesa tu.

Embu tuacheni Idea za Ajabu, sijui kulima tikiti, sijui juisi ya Muwa, tuje na Idea solid ambayo asilimia kubwa inakuwa ni service business na sio manufacturing ambazo asilimia kubwa ni hasara tu.

Nakaribisha majadiliano,
Yani unalosema ni jambo la kweli lakini lin sababu nyingi zinasababisha vijana wa kitanzania waliosoma bongo washindwe.
1. Elimu wanayofundishwa bongo hawafundishwi mbinu za kujiajili
2. Exposure inawafanya wawe behind.
3. Capital ya kuwa na start up business.
4. Commitment, hili linawahusu binafsi
5. Long term plan hakuna short cut, hili linatokana na ugumu wa maisha.
Niishie hapa kwa leo
N.B huyo kijana amefanikiwa sababu katoka familia yenye uwezo na amesoma nje Ana exposure.
 
Mf. Tumemaliza degree ya ualimu , mwenzangu karipoti kazini kaajiriwa , mimi nikaripoti kashamba kadogo ka vitunguu saumu tena umwagiliaji . Mwaka ukiisha nani atakuwa na pesa nyingi benki ? Chukua mapato ya mwalimu kwa mwaka gawa uone kwa siku anaingiza ngapi ? Elimu ni ufunguo na baadae nitapanga namna ya kuchukua mkopo nipanue kilimo changu , nipo free sibanwi na mtu .
 
Nimesoma Mala 4 still sijaelewa ulivyoelewa ulivyoeleza
 
Hata kwenye kuajiriwa tunaajiriwa kwa nafasi na vyeo vile vile kwa mshahara ule ule hatuundi vyeo vipya kisa tu sisi ni wasomi. Mfano umeajiriwa TPA ujiundie kicheo chako "malaika wa zamu" Haiwezekani. This is how things work mambo ni yale yale. Sasa iweje tumshangae msomi aliyeopt kufanya biashara ile ile kwa kiwango chake cha mtaji? Labda tuanze kwa kujiuliza lengo la elimu at first place ni lipi?
 
issue mi naona hapo ni mtaj tu
mtu umehitim chuo lakin pesa ya kufanya biashara zinazoendena na elim yako haipo ukaibe sasa ilipigwe kipirit Jib Hapana
 
Mtoa maada kasome historia ya Nakumatt na Tuskys au Heinz ketchup utagundua umeandika utoto
 
Maisha ni kama maji yanavyofuata mkondo, hata ufanye nini lazima yatafika kwenye lowest ground level na kuwa stable. Mfano msomi anapowekeza kisomi kabisa kwenye kiwanda cha nguo, halafu serikali ikaruhusu mitumba inayouzwa kwa tani kama korosho basi hicho kiwanda tunazika, hata uwe mbunifu vipi, economics hazina uchawi! Sasa sijui unaongea haya ili umsifie tu huyo jamaa au ni vipi
 
Hivi Masters holder akija na wazo wa kufanya biashara kama za Bakhressa kwa lengo la kumfikia bakhlesaa atakuwa mjinga??? Akienda shamba akalima ekali za vitunguuu na kuanza kuzisafirisha nje??? Ulitaka aanze kuzalisha masters zake na kuziuza?
Ndio hapo sasa, linataka degree ya masters iwe ni kilema cha kushindwa kujishughulisha?
 
cha kwanza hela mkuu,
naskia biashara ya kwanza kwanza kufanywa na Mengi alikuwa anaimport kalamu za Bic kutoka Kenya (biashara ambayo ingefanywa na mtu yoyote mwenye mtaji ) na jamaa alikuwa msomi, angeamua kufanya kazi za wasomi labda leo angekuwa nyumbani baaada ya kutumbuliwa na rais anasubii kupangiwa kazi nyingine
Hili jamaa linataka lenyewe ndio lipige mpunga kwenye biashara halafu wengine mkajazane uwanja wa taifa kuomba ajira mlizosomea uhamiaji, no way, kila mtu afe kivyake!
 
Umenigusa. Nafanya biashara ambayo hata asiesoma anaweza kufanya. Ila jinsi ninavyoifanya mimi na hao wengine ni tofauti kabisa jambo linalofanya nipate wateja wa kudumu kirahisi sana, kwa sababu wateja wengi wa biashara yangu ni wasomi hivyo wanakuwa na amani ku-deal na mtu wanaeongea nae lugha moja.

Ni vigumu sana kufanya jambo jipya ila unaweza kufanya kitu kile kile wanachofanya wengine kwa namna tofauti na bora zaidi,utafanikiwa. Bottom line kinachotakiwa ni kipato kizuri kama biashara ni halali hamna ubaya. Mentality kama hii unayoizungumzia ndio inawagharimu wasomi wengi na kubaki walipo kwasababu wanaona watu kama wewe mtawaonaje.
Yaani umepakua kilichokua kichwani mwangu na kumlisha hujo bwege, safi sana!
 
Mkuu trust the process.

Biashara ndio hizi hizi hakuna bizness mpya saaana ila ni vile una exposure gani na market na unafanya bizness yako kwa lengo gani haswa
 
mwee, mmeamua kunisema miye na masters yangu naendesha boda boda naumia sana naposikia boda boda wenzangu wakisema yani wangejua kingereza wasingekuwa pale wangekuwa wamejiongeza zaidi yani nikisikia hivyo narudi kwa mama cha usiku najifungia ndani naanza kitafakari nimekosea wapi miye
 
Wasomi Vijana, mliosoma elimu kubwa za madigrii na Masta tumekosa ubunifu hakika.
Yashangaza sana, Kijana umesoma IT, Umesoma Engeneering, Uhasibu eti unakuja Mtaani unawaza Kufunga Banda la Chips, sijui Kulima matikiti mara duka la vipodozi ni aibu kubwa.

Haiwezekani, Msomi elie elimika unashindwa kuja na mawazo mbadala ya kusaidia Jamii, kuja na mawazo mapya, kuja na Idea za kisomi, mwishoe umepata ajira unachukua mkopo alafu unawaza kufungua duka la Nguo???

Kibaya sio kufanya biashara hizo hapo nilizosema, kinachosikitisha ni kwamba unazifanya biashara hizo kama mtu ambae hajasoma, hakuna kipya wala ubunifu yani ni vuluvulu tu.

Mimi nashangaa sana, Msomi mzima unawekeza milioni 20 kwenye duka la nguo kama la Mangi ambae kaishia la saba na unaifanya biashara hiyo kama yeye?

Nimeikubali Idea ya Benjamin Fernandez, yule jamaa aliyemaliza Stanford university, kaja na Idea ambayo zilikuwepo lakini kaboresha kidogo na sasa ni mwendo wa kupiga pesa tu.

Embu tuacheni Idea za Ajabu, sijui kulima tikiti, sijui juisi ya Muwa, tuje na Idea solid ambayo asilimia kubwa inakuwa ni service business na sio manufacturing ambazo asilimia kubwa ni hasara tu.

Nakaribisha majadiliano,
Guys subiri kwanza....!
Mimi nafuga kuku wa mayai....wewe unafanya biashara gani? Hebu tuanzie hapo
 
Unapokuja na mada kama hii ni vyema ukaja na suluhisho pengine hawajui.
Tuna kizazi cha wasomi wajinga ambao hawajaelimika. Tena mleta maada hii kitu ipo sana kwa PhDs holders vyuoni hao ma professors etc. Unakuta li lecturer linafunga ng'ombe, linalima matikiti, linalima nyanya, linafuga kuku, linafungua duka la nguo ka za mangi etc, mengi hayafanyi utafiti yanafuga samaki, halafu kesho yake linalalamika eti serikali hailisaidii etc, yaani mifumo yetu ya elimu ina problem
 
Kweli kabisa mkuu, hii imenigusa sana na cha ajabu zaidi unakuta media zinaandaa vipindi vya vijana wasomi walioamua kujiajili kupika keki na kutengeneza sabuni za maji.
 
Back
Top Bottom