Ni aibu msomi kufanya biashara ambayo hata asiyesoma anaweza kufanya

Huu uzi kiukweli ni mzuri sana nilicho JIFUNZA KUPITIA UZI HUU NI KUWA BADO NAHITAJI KUJIFUNZA ZAIDI.

Naona watu wengi wanazungumzia mtaji wa KIFEDHA NDIO CHANGAMOTO KUBWA mimi kwa uzoefu wangu mdogo wa kibiashara naoana changamoto sio MTAJI WA KIFEDHA changamoto kubwa iliopo ni KUKUBALI KUJARIBU KUFANYA BIASHARA FLANI kwanini nasema hivyo kwasababu kuna njia nyingi za kuweza kupata MITAJI YA KIFEDHA.

Wasomi wetu wengi sana hawajakosa mtaji wa KIFEDHA ila wamekosa MITAJI ifwatayo

  1. MTAJI WA KUKUBALI KUWA WANAHITAJI KUJIFUNZA ZAIDI KUTOKA KWA WATU TOFAUTI
  2. MTAJI WA KUKUBALI KUJARIBU KUFANYA BIASHARA FLANI
  3. MTAJI WA UBUNIFU WA MWENDELEZO WA BIASHARA FLANI
  4. MTAJI WA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA KIBIASHARA
  5. MTAJI WA PLAN B
  6. MTAJI WA KUKUBALI KUKOSOLEWA
Hizo ndio changamoto kubwa zinazo wafanya WASOMI wetu kukosa kufanya vitu tofauti na watu ambao wamewazidi KIELIMU.

NB:KAMA KUNA MSOMI YOYOTE YUPO HUMU NA ANASEMA CHANGAMOTO KUBWA NI MTAJI WA KIFEDHA BASI ANITAFUTE NIMUONYESHE PESA ZA MITAJI ZILIPO .
wamezoea komba na kupokea rushwa ya mkupua wa kama milioni hivi, leo unamwambia akafanye biashara ya kudunduliza Bukubuku. Hawezi.

Kwa sababu, akili yake inamwambia ''unachelewa wewe, achana na hiyo takataka''
 
Tatizo kubwa ni kwamba mtoa mada hafahamu kwamba hakuna uhusiano wowote kati ya biadhara na elimu (formal). Hakuna period. Kwa hoja husika ni mufilisi.
 
Naungana na wewe pale
Wasomi Vijana, mliosoma elimu kubwa za madigrii na Masta tumekosa ubunifu hakika.
Yashangaza sana, Kijana umesoma IT, Umesoma Engeneering, Uhasibu eti unakuja Mtaani unawaza Kufunga Banda la Chips, sijui Kulima matikiti mara duka la vipodozi ni aibu kubwa.

Haiwezekani, Msomi elie elimika unashindwa kuja na mawazo mbadala ya kusaidia Jamii, kuja na mawazo mapya, kuja na Idea za kisomi, mwishoe umepata ajira unachukua mkopo alafu unawaza kufungua duka la Nguo???

Kibaya sio kufanya biashara hizo hapo nilizosema, kinachosikitisha ni kwamba unazifanya biashara hizo kama mtu ambae hajasoma, hakuna kipya wala ubunifu yani ni vuluvulu tu.

Mimi nashangaa sana, Msomi mzima unawekeza milioni 20 kwenye duka la nguo kama la Mangi ambae kaishia la saba na unaifanya biashara hiyo kama yeye?

Nimeikubali Idea ya Benjamin Fernandez, yule jamaa aliyemaliza Stanford university, kaja na Idea ambayo zilikuwepo lakini kaboresha kidogo na sasa ni mwendo wa kupiga pesa tu.

Embu tuacheni Idea za Ajabu, sijui kulima tikiti, sijui juisi ya Muwa, tuje na Idea solid ambayo asilimia kubwa inakuwa ni service business na sio manufacturing ambazo asilimia kubwa ni hasara tu.

Nakaribisha majadiliano,
Nakubaliana na wewe kuhuhu Ben Fernandez

Lakini Mkuu, naomba tusisahau uhalisia wa jamii zetu pamoja na dhana nzima ya ujasiriamali.

Kuuza chips si jambo baya as long as wanapata faida, pia huu ni mwanzo. Tuwape muda zaidi, Fernandez ni mwajiriwa wa kwanza wa kitanzania kufanya kazi na Bill&Melinda Foundation, unafikiri alikuja bongo na mtaji wa kiasi gani hadi kufanikiwa kuanzisha NALA???

Pia, sidhani kama kuna haja ya kuja na mawazo mapya kutoka sayari Mars, wakati kuna fursa nyingi tu zinazohitaji modification. Angalia Startups za wazungu, hutumia Backward Engineering method kuja na solitions zao. Hapo huangalia bidhaa zinazofanya vizuri sokoni na kuamua kutatua changamoto ndogo zilizonazo, lakini hawaji na mawazo mapya [walio wengi]

Jambo la kuwashauri ni kutobweteka na kutegemea vyanzo hivyo kwa maisha yao yote.
 
Kama umewahi kufanya biashara ungegundua kitu, ni rahisi sana kuanzisha na kuendesha biashara hz unazosema ni za aibu, ukisema uanzishe biashara kwa kutumia professional yako kwa mitaji yetu ni impossible.
 
Aisee,
Watu wana ela ila hawajui pakuziweka,
kwa mtu ambae ni mjasiriamali na anapenda kufanya hivyo,
akiwa na idea iliyosimama ela zipo mkuu,

watu wanaandika pepa, wanashindanisha idea, wanazipeleka kwa masponser na ena zinamwagaa.

hao akina Zurckeberg na bill Gates hawakuwa na ela, bali walifanya watu wakaona na wakaeka ela
Kafatilie vzr, mbele kuna Venture capitalist ambao wako tayr ku invest kn mawazo ya watu wengine. Uku bongo hamna kitu kama icho. Ata ukimfata mengi nae ana ideas kibao anataka azitekeleze.
 
Wasomi Vijana, mliosoma elimu kubwa za madigrii na Masta tumekosa ubunifu hakika.
Yashangaza sana, Kijana umesoma IT, Umesoma Engeneering, Uhasibu eti unakuja Mtaani unawaza Kufunga Banda la Chips, sijui Kulima matikiti mara duka la vipodozi ni aibu kubwa.

Haiwezekani, Msomi elie elimika unashindwa kuja na mawazo mbadala ya kusaidia Jamii, kuja na mawazo mapya, kuja na Idea za kisomi, mwishoe umepata ajira unachukua mkopo alafu unawaza kufungua duka la Nguo???

Kibaya sio kufanya biashara hizo hapo nilizosema, kinachosikitisha ni kwamba unazifanya biashara hizo kama mtu ambae hajasoma, hakuna kipya wala ubunifu yani ni vuluvulu tu.

Mimi nashangaa sana, Msomi mzima unawekeza milioni 20 kwenye duka la nguo kama la Mangi ambae kaishia la saba na unaifanya biashara hiyo kama yeye?

Nimeikubali Idea ya Benjamin Fernandez, yule jamaa aliyemaliza Stanford university, kaja na Idea ambayo zilikuwepo lakini kaboresha kidogo na sasa ni mwendo wa kupiga pesa tu.

Embu tuacheni Idea za Ajabu, sijui kulima tikiti, sijui juisi ya Muwa, tuje na Idea solid ambayo asilimia kubwa inakuwa ni service business na sio manufacturing ambazo asilimia kubwa ni hasara tu.

Nakaribisha majadiliano,

Mkuu umeongea point lkn tatizo sio amesoma akafanya shughuli izo tatizo mtaji ataupata wp ndo mana ameona aanze toka chini ili akuwe apate mtaji aweze kutumia usomi wake mbele ya safari tanzania bana kila mtu analalamika kwa sehem yake leo msomi anaonekana amna kitu kisa kujiajili kwa utaalamu wake mkuu sio mchezo kumbuka tra ukishaweka tu kioo mlangon anakuja kudai kodi awangalii ndo we umeanza umewekeza kwenye elimu aiozi acha watu watafute mtaji ameshapiga hesabu bila ivo akopesheki
 
Umenigusa. Nafanya biashara ambayo hata asiesoma anaweza kufanya. Ila jinsi ninavyoifanya mimi na hao wengine ni tofauti kabisa jambo linalofanya nipate wateja wa kudumu kirahisi sana, kwa sababu wateja wengi wa biashara yangu ni wasomi hivyo wanakuwa na amani ku-deal na mtu wanaeongea nae lugha moja.

Ni vigumu sana kufanya jambo jipya ila unaweza kufanya kitu kile kile wanachofanya wengine kwa namna tofauti na bora zaidi,utafanikiwa. Bottom line kinachotakiwa ni kipato kizuri kama biashara ni halali hamna ubaya. Mentality kama hii unayoizungumzia ndio inawagharimu wasomi wengi na kubaki walipo kwasababu wanaona watu kama wewe mtawaonaje.
Mkuu unafanya biashara gani?
 
Huyo jamaa aliyetoa mada inaonekana amekariri kwamba mtu msomi anatakiwa awe bishoo au awe mbaguzi wa aina fulani za biashara.
Maana ya kufanya kitu kisomi ni kuwa na uwezo wa kufanya prediction/forecast of the future(future plans).
So msomi hatakiwi kuangalia leo biashara gani anafanya bali tunaangalia baadae itamletea nn hyo biashara.
Kwa mfano mtu aliyesoma anaweza akaanzisha biashara ya bodaboda ukamcheka lkn badae hyo hyo biashara ya bodaboda ikamfanya badae aje kumiliki kampuni ya transportation na logistics.
Lkn mtu asiyesoma ataanza na biashara ya bodaboda hadi anazeeka na biashara hyo hyo ya bodaboda.
Yaani mtu asiyesoma hawazi kufanya modifications na kuikuza biashara yake au hata kwenda na wakati.
 
Tatizo siyo wasomi wetu, tatizo ni mfumo tuliojengewa na serikali yetu, mfumo wenyewe ni wa elimu kwa maana ya mtaala. Elimu yetu inamwandaa mhitimu kutokujua aitumie vipi elimu yake baada ya kumaliza, kwakuwa kwa asilimia kubwa elimu yake aliipata kwa njia za nadharia, na siyo vitendo.
 
Naungana na wewe pale

Nakubaliana na wewe kuhuhu Ben Fernandez

Lakini Mkuu, naomba tusisahau uhalisia wa jamii zetu pamoja na dhana nzima ya ujasiriamali.

Kuuza chips si jambo baya as long as wanapata faida, pia huu ni mwanzo. Tuwape muda zaidi, Fernandez ni mwajiriwa wa kwanza wa kitanzania kufanya kazi na Bill&Melinda Foundation, unafikiri alikuja bongo na mtaji wa kiasi gani hadi kufanikiwa kuanzisha NALA???

Pia, sidhani kama kuna haja ya kuja na mawazo mapya kutoka sayari Mars, wakati kuna fursa nyingi tu zinazohitaji modification. Angalia Startups za wazungu, hutumia Backward Engineering method kuja na solitions zao. Hapo huangalia bidhaa zinazofanya vizuri sokoni na kuamua kutatua changamoto ndogo zilizonazo, lakini hawaji na mawazo mapya [walio wengi]

Jambo la kuwashauri ni kutobweteka na kutegemea vyanzo hivyo kwa maisha yao yote.
Ben anapataje faida kwenye NALA?
 
Wasomi Vijana, mliosoma elimu kubwa za madigrii na Masta tumekosa ubunifu hakika.
Yashangaza sana, Kijana umesoma IT, Umesoma Engeneering, Uhasibu eti unakuja Mtaani unawaza Kufunga Banda la Chips, sijui Kulima matikiti mara duka la vipodozi ni aibu kubwa.

Haiwezekani, Msomi elie elimika unashindwa kuja na mawazo mbadala ya kusaidia Jamii, kuja na mawazo mapya, kuja na Idea za kisomi, mwishoe umepata ajira unachukua mkopo alafu unawaza kufungua duka la Nguo???

Kibaya sio kufanya biashara hizo hapo nilizosema, kinachosikitisha ni kwamba unazifanya biashara hizo kama mtu ambae hajasoma, hakuna kipya wala ubunifu yani ni vuluvulu tu.

Mimi nashangaa sana, Msomi mzima unawekeza milioni 20 kwenye duka la nguo kama la Mangi ambae kaishia la saba na unaifanya biashara hiyo kama yeye?

Nimeikubali Idea ya Benjamin Fernandez, yule jamaa aliyemaliza Stanford university, kaja na Idea ambayo zilikuwepo lakini kaboresha kidogo na sasa ni mwendo wa kupiga pesa tu.

Embu tuacheni Idea za Ajabu, sijui kulima tikiti, sijui juisi ya Muwa, tuje na Idea solid ambayo asilimia kubwa inakuwa ni service business na sio manufacturing ambazo asilimia kubwa ni hasara tu.

Nakaribisha majadiliano,
Maisha hayana formula maalumu, kusoma ni jambo moja kuyapatia maisha ni jambo jingine kama wewe umededicate maisha yako kuwa mgunduzi wa formula, device etc its up to you, so ukiona mtu anatumia fursa alizoziona mtaani kwake muache,

Sajwahi ona Mangi fala kama wewe
 
Kweli kaka mfundishe huyo amekariri maisha.
Hajui Kuna watu wametajirika na kutoboa maisha kwa kuuza chakula jiko la baa.
Kuna mtu amejenga nyumba 3 kwa biashara ya kuuza ndoo za plastics na mapipa used.
Yeye amekariri usomi ni kuchomekea na kuvaa tai halaf mwisho wa mwezi alipwe laki 4 au 5.
 
The issue ni una mudu vipi maisha na changamoto zake kusoma university ni level ya kuielewa dunia, jamii, pia kuwa sehemu ya utatuzi wa changamoto, sasa suala la kufanyia kazi ulicho kisoma ni utashi wa muhusika as long as kuna jambo unaeza lufanya likakupatia kipato kikubwa cha kutosha na uhakika sioni shida iko wapi, afu huyu jamaa atakua sio mchaga hakuna mchaga anaechagua hela
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] nawajua vzr wachaga.
Ukimuona kwenye biashara yake unaweza kumdharau ukafikir ni bwege ila ukionyeshwa mali anazomiliki unaweza ukazimia.
Na kuna wamama wa kichaga kule Arusha wanauza mitumba barabarani ila ukiambiwa mijengo wanayomiliki unaweza kulia kwa kupoteza muda kwenye vikazi vya kuajiriwa.
 
Mkuu,

Suluhisho nimeweka, Tuwaze kufanya vitu kwa utofauti, yani kama ni biashara ya chips basi fanya kama KFC ambayo unafanya tena kwa utofauti, sio unafungua banda la chips kama la mluguru wa pale buguruni
Wewe unachotaka ni biashara ionekane fancy sio profitable.. .hivi ni vitu viwili tofauti....mtu kama anafungua biashara bugurun, tabata,ubungo,mwenge,tandika katika location zote hizo hakosi elfu ishirin kwa siku hata kwa kuuza mihogo kwa mwez ana sh.ngap? Total utakayopata compare na salary yako kama wewe ni msomi mfanyakazi.Then utapata jibu why people do what they do.
 
cha kwanza hela mkuu,
naskia biashara ya kwanza kwanza kufanywa na Mengi alikuwa anaimport kalamu za Bic kutoka Kenya (biashara ambayo ingefanywa na mtu yoyote mwenye mtaji ) na jamaa alikuwa msomi, angeamua kufanya kazi za wasomi labda leo angekuwa nyumbani baaada ya kutumbuliwa na rais anasubii kupangiwa kazi nyingine
Hiyo biashara sio rahisi kama unavyoichukulia.pili siamini kama alikua anaimport kalamu kuja kuziuza reja reja bongo, naamini alikua anatafuta suppliers wakubwa au kutoka kiwandani moja kwa moja huko nchini kenya na kuja kuwauzia retailers bongo, biashara kama hii ni complex kiasi cha kutosha kuitwa ya kisomi,sio kuuza kalamu kwenye kingo za barabara au kutembeza kalamu chuo au kwenye kibanda.
 
Maliza chuo uje kitaa tuone ubunifu wako alafu ww mtoa Mada ni mtoto wa kishua.. Maisha huyajui maisha yako siyo Sawa na na wenzako.. na nasubiri tuone ubunifu wako
 
Kibaya sio kufanya biashara hizo hapo nilizosema, kinachosikitisha ni kwamba unazifanya biashara hizo kama mtu ambae hajasoma, hakuna kipya wala ubunifu yani ni vuluvulu tu.
Nadhani hapa ndio kuna mantiki huko pengine pote umeandika upuuzi
 
Siku hizi ukitaka pesa nzuri wewe fundisha watu jinsi ya kutengeneza pesa....! Yaani seminar hizi utatengeneza pesa nzuri easily
Bro,hapa watu walishashtuka aseee...sio ki rahc kama unavodhani mkuu...
 
Back
Top Bottom