Pre GE2025 Ni aibu na fedheha kubwa sana kwa Tundu Lissu kukimbia kujiandikisha kwenye Daftari la Mpiga Kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Ni aibu na fedheha kubwa sana kwa Lissu kukimbia kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura.ni aibu isiyo bebeka,ni aibu na fedheha ya kiwango cha juu sana.

Hivi inawezekana vipi kiongozi wa ngazi ya juu kama Lissu ambaye ni makamu mwenyekiti wa CHADEMA Taifa akimbie kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura?

Chama kitapata ushindi kutoka kwa kura ya nani? Kama yeye hataki kujiandikisha na kupiga kura, anataka nani ajiandikishe na kupigia kura wagombea wa chama chake?

CHADEMA inaweza kupata vipi ushindi ikiwa viongozi wake wenyewe hawataki kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura? Kama yeye hayupo tayari kutenga muda wake anataka nani atenge muda wake kujiandikisha na kupiga kura?

Anatoa mfano na taswira ipi kwa wanachama na wafuasi wake? Anaweza akapata wapi nguvu ya kutamka kuwa CHADEMA itashinda uchaguzi? Itashinda kwa kura ya nani wakati yeye mwenyewe hajapiga kura? Nani anakipa ushindi chama? CHADEMA kinaweza kusema vipi kinaibiwa kura? Kitasema kinaibiwa kura zipi? Kutoka kwa nani aliyekipigia kura wakati viongozi wake hawajapiga kura?

Nani mwenye akili Timamu na mwenye afya ya akili anayeweza kupoteza muda wake kuipigia kura CHADEMA .wakati yenyewe tu chini ya viongozi wake hawapo tayari kupiga kura na hawaoni umuhimu wa kupiga kura na hawaelewi nguvu ya kura yao? Watamshawishi nani kwenda kuwapigia kura wakati wao wamebaki majumbani kwao wakinywa mvinyo?

Nilishasema kuwa lissu yeye kiu yake na matamanio yake ni kutaka kuleta machafuko tu hapa Nchini.kama ambavyo amekuwa akitoa kauli zake za kichochezi kwa watanzania .ambao hata hivyo wamekuwa wakimpuuza wakati wote. Yeye anataka njia ya mkato kupata madaraka.hana uchungu na Taifa letu,hana cha kupoteza hata Taifa letu likisambaratika na kupasuka vipande vipande.

Maana watoto wake alishawachukulia Uraia wa nchi zingine za Magharibi.Familia yake yote haipo Nchini.Sasa mtu wa aina hiyo Unafikiri utakujali na kuwa na huruma na wewe mtanzania uliyepo hapa Nchini? Unafikiri atakuwa na uchungu gani Taifa likiwaka moto zaidi ya kufurahi na kufuatilia kupitia Tv akiwa sebuleni na familia yake huko Marekani au Ulaya?

Angalia hata sasa hivi akitoa lugha zake za uchochezi,ubaguzi na chuki unaona akisafiri kimya kimya na kwenda ulaya. Hiyo maana yake ni kuwa hata siku Taifa likiwaka na kuteketea kwa Moto au Watanzania wakianza kuchinjana,yeye ataondoka kimya kimya kwa ndege na kwenda kuchekea ulaya huko na wanae huku wakigongeana glasi za vinywaji vikali na laini wakishindikiza na Minofu ya nyama na kupulizwa na Feni kupunguza Joto.

Watanzania kamwe na katu tusije ingia katika mtego wa lissu wakutaka kutugawa Watanzania na kupandikiza chuki miongoni mwetu.tusikubali apandikize mbegu za ubaguzi miongoni mwetu watanzania.lissu ni mroho na mwenye uchu wa madaraka hata kwa njia ya Damu au kwenda ikulu huku akipita katika au juu ya miili ya watanzania iliyokata pumzi.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Duh, umetoa povu hilo kudadeki ni balaa!!
 
Ajiandikishe ili iweje, wakati Tanzania hakuna uchaguzi bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura?
Sasa mnashiriki uchaguzi wa nini? Mna akili kweli Ninyi? Mnajitambua kweli? Kwanini mnachukua Fomu za kuomba uteuzi wa kugombea.
 
Shida ni upeo mdogo ulionao,umeandika gazeti hata hueleweki sijui kama huwa una ubongo wa binadamu
 
Sasa mnashiriki uchaguzi wa nini? Mna akili kweli Ninyi? Mnajitambua kweli? Kwanini mnachukua Fomu za kuomba uteuzi wa kugombea.
Wapi umeona mimi nashabikia kushiriki huo upuuzi? Ama huoni ni kwa kiwango gani wananchi wamepuuza huo ushenzi uitwao uchaguzi?
 
Wapi umeona mimi nashabikia kushiriki huo upuuzi? Ama huoni ni kwa kiwango gani wananchi wamepuuza huo ushenzi uitwao uchaguzi?
Wananchi wamejitokeza kwa wingi maana wana imani kubwa sana na mfumo wa uchaguzi na uwezo wa kuheshimiwa sauti na machaguo yao.ambapo kwa kiasi kikubwa CCM ndio chaguo lao
 
Ni aibu kushinda manane ya usiku kuposti UHARO.... kama huu🤔🤔😀🤣
 
Ajiandikishe ili ahalalishe kitu gani?Umeandika kwa hamaki na chuki utadhani kichaa kimepanda.
 
Mishikaki ni huna akili au unawashwa. Kama uchaguzi ni huru na haki, basi kila MTU Ana Uhuru wa kufanya yafuatayo:-
1. Kujiandikisha
2. Kugombea
3. Kuchagua/ kuchaguliwa.
Tundu Lissu ni mweledi tofauti na MBOWE. Huu uchaguzi ni haramu, umechezewa, na umechafuliwa. Tundu Lissu hawezi kushiriki hii haramu.

CHADEMA walitakiwa kususia uchaguzi huu, lakini kwa uroho wa MBOWE wameingiza timu.

MBOWE Ana uoni hafifu wa future wa Tanganyika tuitakayo
 
..hivi kuna mtu asiyemjua Lissu Tanzania hii mpaka iwe lazima ajiandikishe kupiga kura?

..Na ukiacha hilo inajulikana kwamba Lissu alilazimika kusafiri nje ya nchi kushughulikia masuala ya kesi yake.
 
Wananchi wamejitokeza kwa wingi maana wana imani kubwa sana na mfumo wa uchaguzi na uwezo wa kuheshimiwa sauti na machaguo yao.ambapo kwa kiasi kikubwa CCM ndio chaguo lao
Hicho kizazi cha kukipa data za kupika kiko wapi? Uchaguzi wa 2015 walijioandikisha kupiga kura walikuwa 20m+, hapa ndio mfumo wa BVR ulianza rasmi, kila mtu aliona misuru ya watu kwenye vituo vya kupigia kura. Idadi hii ya kupika inasema wako 31m, lakini waliokuwa mawakala wa kuandikisha wapiga kura walikuwa wanasoma magazeti na kuchat vituoni! Na sababu hasa ya wananchi kupuuza huo uchaguzi, ni kitendo cha ccm kuchezea kura zao ilo wakae madarakani kwa shuruti.

Huu ndio ukweli uliopo na kila mtu anaujua, sasa subiri siku ya uchaguzi uone ni kwa kiwango gani wapiga kura watakuwa wachache. Wewe baki ukipiga propaganda za kizee hapa, lakini ukweli kuwa watu wameichoka ccm uko wazi peupe. Mtapika idadi ya wapiga kura sana, lakini ndio imeisha hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…