Yeah hakika kabisa, Hi-Fi system zinacheza channel mbili tu ama 2.1 ama stereo channels. Left and Right (mids & highs) pamoja Bass(Lows) ambazo ni mahususi kwa audio contents kama muziki! Home theatre zinacheza kuanzia channel 5.1 hali kadhalika 7.2 ama 9.2
Kuhusu muziki kuupigia kwenye hometheatre quality ya muziki ama vionjo utavipata vizuri tu given kwamba hometheatre husika imekuwa optimized kutenganisha channels kulingana na mahitaji yako, maana hometheatre ina combination ya channels zote, Front, Center, Rear bila kusahau bass ama low frequency channel.
Za Front ndio za Stereo ama Music pia kuna hio Center kwa ajili ya dialogues na za Rear kwa ajili ya movie effects kama bomu, radi, upepo kulingana na scenes huitwa sorround soeakers. Bass inatoa sauti ambazo ziko chini sana ya upeo wa mwanadamu kuzitambua hivyo inasikika kama ngurumo tu.
Hivyo kwa kuhitimisha ukiangalia movie kwenye Hi-Fi system hutapata manjonjo yote kama endapo ungeangalizia movie hio katika hometheatre. Sababu ni kwamba channel zitakuwa overlapped maana vyote vitalazimishwa kusikika kwenye stereo channels (Front Left & Front Right) which is less fun!
Ila kinyume chake kusikiliza nyimbo kwenye Home Theatre unaweza pata manjonjo kama ilivyokusudiwa kwa sababu vionjo vya muziki vinaandaliwa kusikika katika Stereo Channels na bass. Cha kufanya set hometheatre yako kwenye stereo sound mode itapiga speaker mbili tu kama Hi-Fi System.
Drawback ni kwamba hometheatre inaweza isiwe very loud kama Hi-Fi system.
NB: Channel ninamaanisha speakers!