Ni aina ipi ya sub woofer ni nzuri?

subwoofer langu seapiano ni HI-FI maana yake ni high fidelity sijui nyinyi mnaongea nini? high fidelity ni uwezo wa speaker kureproduce sauti katika ubora wa hali ya juu , me subwoofer langu linaipita hata subwoofer zingine za sony za bei kubwa sana , nafahamu technology kama dobly atmos au dts ambazo hutumika katika 3D sound , lakini technology hii bongo bado sana labda mpaka upate content zinazoweza kutumia hiyo technology na mara nyingi technology hizo zinapatikana kwenye movies tena sio movie za kawaida ni zile za kununua ambazo unakuta zimeandikwa 3D sound supported au dobly atmos lakini hakuna tofauti yoyote na subwoofer yenye HI-Fi kama utakuwa unapiga nyimbo za kina daimond na dogo aslay labda upate nyimbo za kwenye album ambazo zimetengenezwa special kwa technology hiyo na mziki wako uwe una support.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Man mimi ya kwangu ni LG bt kuna madogo walikuwa na sherehe nikawaazima. Tangu wamenirudishia ilianza inapiga na kukata inapiga tena inakata but now haipigi kabisa.
Inawezekana hilo ni tatizo gani?

Wema ni akiba.
 
Thanks mkuu!

Hakika umenishauri vyema,ushauri nauchukua bila shaka yoyote.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
alafu technology ya subwoofer nyingi sauti inaenda mpaka mtaa wa pili , wakati hizo za bei sauti hubaki ndani ya nyumba tu

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwani mkuu sauti unataka isibaki ndani ya nyumba we unataka ifike wapi???au ni mimi sijaelewa point yako labda?!

Kwamba uwaburudishe walio nje ya nyumba yako wakati umeme unanunua mwenyewe au sometimes uwakere sasa kuna faida gani?

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Man mimi ya kwangu ni LG bt kuna madogo walikuwa na sherehe nikawaazima. Tangu wamenirudishia ilianza inapiga na kukata inapiga tena inakata but now haipigi kabisa.
Inawezekana hilo ni tatizo gani?

Wema ni akiba.
Inakata yote au bass yake!?

Voxser empire
 
nilikua naeleza tu faida na hasara.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa kuongezea tu kwamba home theater ina mini hi-fi ndo maana kwenye setting wameweka movie na music km unasikiliza muziki unaweka music ila najua watu wengi hawalijui hilo. hata mimi nakushauri chukua home theater kuanzia watt 1000 blue ray, kama ni sony nunua kwa authorized dealer maana kuna feki nyingi.
 
Hahahaha mkuu si watu wanataka mtaa ujue kwamba wanamiliki sound za hatari. Hii ilikuwa sana enzi zile tunakua kitaa wazee wakitoka unablast mziki ili kuwanyoosha machalii zako ambao kwao redio ndogo!

Ndio alichomaanisha jamaa hiko!
 
Imeitwa Hi-Fi kwa sababu imeundwa kwa mfumo wa channel 2.1 ambayo ni Left and Right Stereo Channels with bass speaker!

Hio subwoofer yako unayosema inapita Sony kwa mziki labda kwa makelele yake ila kwa music production haiwezi kuikuta Sony hata theluthi. Nina sea piano kubwa kama lako hilo la 180,000/= lina jumla ya 150 watts za RMS. Kwa mgawanyiko Subwoofer speaker inakula 100watts RMS halafu Left and Right Channels zinachukua 25w each!

Sony ya 1000 watts yenye speaker setup ya sattelite speakers 5 na subwoofer yake yani 5.1 Channel mgawanyiko wake upo hivi. Subwoofer ni 165w RMS na kila sat. Speaker ina 165w!
Sasa do the maths 165w x 6 ni ngapi?

Kisha uniambie system yenye output ya 150w na yenye 1000w zinaanzaje kuwa sawa?
 
Una point fundi ila wacha nikuweke sawa kidogo, mie pia nilishamiliki hizo subwoofer 2 kabla sijahamia kwenye hometheatre.

Kwanza nilinunua ile kubwa yenye knob kwa mbele za kupandisha na kupunguza bass, echo na sauti. Zile ndio analog na ndio zenye mziki mzuri kuliko hizi za kidijitali. Tatizo lake tu baada ya miaka 3 ilikuja kuanza kukoroma wakati unacheza na bass sauti kama inakwangua ila ukiiset inatulia tu. Wakati unachezesha knob ndio kuna distortion flan inatokea. Sema haina shida yeyote adi sasa inadunda.

Kisha nilinunua sea piano ya kisasa ambazo ndio hizi zenye bluetooth zenyewe zinatumia saketi kama ya simu kweli waya ni chache sana na za kupachika na kuchomoa tu nadhani za speaker na za control unit/display tu. Nilikuwa na yangu iliunguwa capacitor nikaenda kuibadilisha pia fundi alinieleza hilo hilo! Ila iko poa ingawa mziki wake sio mzuri sana kama ile analog.

Jinsi ya kuzitofautisha hizi mbili ni kwamba analog zina knob kwa mbele unaseti kiwango cha sauti manually ila digital unatumia remote ama kidude cha sauti kukontrol kila kitu kupitia display. Swala hilo halihusiani na output za RCA ama AUX kama ulivyotanabaisha hapo awali!
 
Ila inakua bado iwewaka au inazima kbsa

Voxser empire
 
Mkuu mi naimba unifundishe baadhi ya ya mambo

Ningependa unifundishe jinsi ya kutengeneza amplifier kwa kutumia IC aina ya TDA2030.

Hata kwa kulipia nipo tiyari nisaidie mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…