Ni balozi wa Nchi gani alifukuzwa Tanzania kwa sababu aliwajua waliomshambulia Lissu?

We una hoja gani hapa?

Kwanini Lissu akisimulia Madhira yaliyompata mnachukia sana? Mlitaka afe?
Nipo kwenye kutafuta haki. Kwann hasiende mahakamani? That's my question to you. Naomba Majibu, usilete matusi. Kila siku anahojiwa anatoa shutuma hizo.
 
Ujinga mtupu, Lissu aliisha sema aliyempiga risasi ni Magufuli,Sasa uchunguzi wanini wakati Lissu ananjua aliyempiga risasi? Lissu haende mahakamani Maana Yeye anajifanya mwanasheria nguli hiki kichaka cha mahakama zetu hazitendi haki ni uongo, mbona Lissu haliwahi kushinda kesi nyingi kupitia hizi mahakama!.
 
Unapoteza muda wako hapa. Nenda kafanye kazi
 
Kweli lissu akili imechoka. Kila siku anataka, haojiwe lakin anaongea nonsense. Kama kuna ushahid Lissu ni mwanasheria afungue kesi mahakamani. Sasa, kila, siku porojo tu.
Inaonekana wewe ni mhitimu wa shule za kata
 
Si akafungue mashtaka kama anajua?
Kwanza hao walomshambulia nasikia walishauwawa wote
 
Unapoteza muda wako hapa. Nenda kafanye kazi
Wewe ndiye anayepoteza mda kuandika habari za kufikirika kila kukicha mnaleta habari eti mnataka uchunguzi wa kupigwa risasi Lissu wakati Yeye Lissu kwamujibu wake Yeye ananjua vizuri,tulimwona hakizunguka kwenye vyombo vya habari vya kimataifa akimtaja,Sasa uchunguzi wanini? Lissu hakwende mahakamani full stop.
 
Chadema lacks committed leadership; the top echelons are mostly all mercenaries!
In Nyerere’s parlance ni “ malaya malaya “.
 
Makonda na kipilimba
Ile damu iliyomwagika kamwe haiwezi kupotea bure!
Kama sio ninyi vizazi vyenu vitakuwa vya laana milele (rejeeni vitabu vitakatifu)
 
Dpp ni nani na kwanini awe na mamlaka ya kufuta kesi ambayo imepelekwa mahakamani
 
..kuna balozi zina majasusi hapa nchini.

..nakushauri ukasome taarifa za CIA kuhusu Tz zilizokuwa declassified utaelewa kuwa kuna watu wanatuchunguza.

Kila nchi ina majasusi Ubalozini. Hata Tanzania wanapeleka Majasusi kwenye Balozi zao ... Mfano Mdogo tu Othman alikuwa Afisa Ubalozi UK akaja kuwa Mkuu wa Usalama. Kipilimba alikuwa Mkuu wa Usalama akaenda kuwa Balozi Namibia ..... 80 % ya wafanyakazi Ubalozini ni mashushushu .....!
 
Unaambiwa hadi video ipo inasubiriwa muda tu ivujishwe.

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…