Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Zuberi, 2011 natoka Morogoro kwenda mwanzaBus gani umewah panda na ukajutia safari yako.
Nipo ndani ya basi na nishajiapiza sitapanda tena.
Linaitwa Champion
Pole sana mkuu,hyo gari inaitwa hakuna kulala,,SAIBABA,
Nilikua nasafiri kutoka dar kwenda arusha kwaajili ya interview, safari jumapili interview jumatatu,
nilikata tiketi siku mbili kabla ya safari, siku ya safari nafika stand wananiambia gari yangu imeondoka wananipa gari nyingine ya saa mbili, kumbe gari halijaondoka ila lilikua halijajaza, nimekaa kwenye gari hadi saa8 mchana ndio inatoka wakasema ata kama saa6 usiku lazima tuingie arusha siku iyoiyo,
mwendo tuliokua tunaenda njiani kama msafara wa msiba wa malkin Elizabeth
Tunafika same saa6 usiku dereva na konda wakatuacha kwenye gari wakaenda kulala wanapojua wao wanarudi saa2 asubuhi jumatatu, tunaingia arusha saa6 mchana nikafika hadi sehemu tuliyotakiwa kufanya interview nimechelewa na watu wote wameondoka ilikua chuo cha uhasibu arusha.
Iyo safari sitaisahau na SAIBABA sitalisahau.
[emoji16][emoji16]Special coach ya iringa-dar yule dereva alipiga gia tulipofika kona za iyovu mabegi yalikuwa yanapisha kwenye korido ya basi abiria wote kimya.Tulipokaribia mikumi tairi la nyuma lilipata pancha,watu wakaripuka kumlaumu dereva mwendo mkali,alinichekesha konda kwamba ule mwendo ni afadhari eti kwa siku ile alikuwa na malaria bahati nzuri ile tunasimama gari iliosimama na ya kwanza ilikuwa nayo ni special coach ya songea,tukasaidiwa spare tyre tukaendelea na safari.Injini ilikuwa ni Isuzu mv 118.
[emoji16][emoji1][emoji28]Ni mengi sana ukiyataja watasema unawaharibia biashara kumbe wao ndio wanajiharibia, unapanda gari Dar to Mbeya unafika saa nne usku gari linasimama hovyo hovyo kifupi hawaheshimu muda, lingine nilipanda kutoka Mwanza Arusha unafika saa mbili na nusu gari linaokota watu njiani kama Dalala dala.
Baadaya kugundua hayo nilijitafutia magari yangu ya kupanda. Kutoka Mwanza Arusha huwa nakamata chuma ASANTE RABI, Dar Mbeya SAUL Au NEW FORCE Arusha Mbeya hapa bado sijawasoma vizur ila KAPRICON wako vizr na kidog ARUSHA EPRESS. Mbeya To Mwanza PREMEAR wako vizuri.
[emoji38][emoji16][emoji16] alafu hiyo saibaba ni ile inayo pitaga uyole saa 4,5,6 sindioTukiwa uyole tunasubiri abiria wajae tuondoke na coaster mara saibaba ya kutoka s/wanga ikafika na kufaulisha kwenye coaster,abiria mmoja msukuma akakaa pembeni yangu huku amevaa gumboot yaani ile kishambani kabisa tulipofika makambako akaomba ajisaidie kumbe anatapika abiria mmoja akampa maji nikapata amani kidogo,walishukia msamvu na mwenzie.N.B ushamba ni kero!
Hiyo hiyo tena ni marcopolo[emoji38][emoji16][emoji16] alafu hiyo saibaba ni ile inayo pitaga uyole saa 4,5,6 sindio
Next time panda trainUpendo dar to makambako, gugari gunapiga kelele kama gutipa
Eleza kwa upana .Al saedy,nilikata tiketi kwenda stendi ikawa Hilo. Basi halipo
Nilikata tiketi 23-12-2021 ili nisafiri 25-12-2021,kama sijakosea tarehe, ilikuwa kabla sikukuu ya krismasi,nilifika kituo cha mabasi Magufuli mbezi,sikukuta basi,nikapiga simu haipokelewi, aada ndio mtu mmoja akaniambia haiendi Tabora,nikafaulishwa kwenye basi la Aifola la kwenda kigoma.Eleza kwa upana .
Aifola n zuri hope iliinjoiNilikata tiketi 23-12-2021 ili nisafiri 25-12-2021,kama sijakosea tarehe, ilikuwa kabla sikukuu ya krismasi,nilifika kituo cha mabasi Magufuli mbezi,sikukuta basi,nikapiga simu haipokelewi, aada ndio mtu mmoja akaniambia haiendi Tabora,nikafaulishwa kwenye basi la Aifola la kwenda kigoma.