Mawazo kama haya watu wanayachukulia poa lakini wenye siri ni waliothubutu kufanya biashara kama hizi
Nitakupa story kidogo,
Mwaka 2012 kuna jamaa aliniomba Tsh.40,000/= afanye kama mtaji na mambo yakiwa mazuri atanirudishia pesa yangu.
Kwasababu alikuwa ameacha mke na watoto kijijini (alikuja Dsm kwa matibabu yake) nikasema ngoja niondoe lawama tu nikampa bila kumuuliza biashara aliyotaka kufanya na sikuweka matumaini ya kurudisha ile pesa (ila sikumwambia; nilitaka abaki kwenye plan yake)
Baada ya kumpa kile kiasi, aliwatembelea fundi seremala akawa anaokota mbazo zisizo tumika akatengeneza meza ya kishikaji akaweka chini ya mwarobaini pembezoni na barabara, halafu akazama buguruni akanunua machungwa tu; sinia, kisu, ndoo ndogo na maji alichukua nyumbani
Baada ya wiki kama mbili wateja wakawa wameshamzoea, akaongeza mzigo wa matunda biashara ikachanganya na wiki ya tatu akaniletea pesa yangu
Baada ya muda ukaingia mwezi wa ramadhani, akaongeza viazi na mihogo, baadae akaanza kununua viatu vya mitumba pale Ilala Boma na kuvisafirisha kwenda kijijini hasa msimu wa mwisho wa mwaka akiwalenga wanafunzi na sikukuu za mwisho wa mwaka. Kiatu anakinunua Tsh.elfu moja, elfu moja na miatano kikifika kule kijijini kinauzwa hadi elfu ishirini!
Kumbuka chanzo ni Tsh.40,000/= Wala sio laki 3
Kumbuka.