Ni biashara gani naweza fanya kwa mtaji wa laki 3?

Ni biashara gani naweza fanya kwa mtaji wa laki 3?

Mawazo kama haya watu wanayachukulia poa lakini wenye siri ni waliothubutu kufanya biashara kama hizi

Nitakupa story kidogo,

Mwaka 2012 kuna jamaa aliniomba Tsh.40,000/= afanye kama mtaji na mambo yakiwa mazuri atanirudishia pesa yangu.

Kwasababu alikuwa ameacha mke na watoto kijijini (alikuja Dsm kwa matibabu yake) nikasema ngoja niondoe lawama tu nikampa bila kumuuliza biashara aliyotaka kufanya na sikuweka matumaini ya kurudisha ile pesa (ila sikumwambia; nilitaka abaki kwenye plan yake)

Baada ya kumpa kile kiasi, aliwatembelea fundi seremala akawa anaokota mbazo zisizo tumika akatengeneza meza ya kishikaji akaweka chini ya mwarobaini pembezoni na barabara, halafu akazama buguruni akanunua machungwa tu; sinia, kisu, ndoo ndogo na maji alichukua nyumbani

Baada ya wiki kama mbili wateja wakawa wameshamzoea, akaongeza mzigo wa matunda biashara ikachanganya na wiki ya tatu akaniletea pesa yangu

Baada ya muda ukaingia mwezi wa ramadhani, akaongeza viazi na mihogo, baadae akaanza kununua viatu vya mitumba pale Ilala Boma na kuvisafirisha kwenda kijijini hasa msimu wa mwisho wa mwaka akiwalenga wanafunzi na sikukuu za mwisho wa mwaka. Kiatu anakinunua Tsh.elfu moja, elfu moja na miatano kikifika kule kijijini kinauzwa hadi elfu ishirini!

Kumbuka chanzo ni Tsh.40,000/= Wala sio laki 3

Kumbuka.
Hii story imwnigusa sana but akili kumkichwa not everyone can start today and win tomorrow

Some win two years later while others win 10 years later
 
Hapa sio mahala pake.

Sasa laki 3 kwa miaka hii atafanyia biashara gani?

Arudi FB na insta akafanye challenge au awe content creator atapata vi mia mbili mia tatu vya kununulia mboga.
Umetoka kuuliza kuhusu zile pesa za mchango jf zimeenda wapi na usikute hujachanga

Halafu hapa unaonesha ego yako wazi wazi kabisa yaani kuhusu kijana mwenye mawazo chanys
 
Subiri mechi ya Manchester united Vs Liverpool alafu bet mpe ushindi Manutd weka hela yote , subiri kuwa Millionaire
 
Wakuu, ni biashara gani mtu anaweza kuanzisha ndani ya miezi 6 hadi mwaka, akiwa na kipato cha Shilingi laki 3 kwa mwezi, ambayo akijitahidi ina uwezekano wa 95% ya kufanikisha au kuboresha maisha yake?
Kabla ujapata ushauri tafakali unandoto gani au unamipango gani ????
 
Back
Top Bottom