Ni birthday yangu 50 years

Ni kweli umri una maana nyingi nimepitia mengi mishale, maumivu ya kuondokewa na wapendwa nk.
Kweli kabisa Mama angu kwa umri huo ni dhahiri ushakutana na mengi. Pole lakini.

M'Mungu azidi kukuweka Mama.
 
Hahahaaa. Hatujasahau ujue wengi walidanja kwa kusikia ile Kikokotoo. 😀😀😀😀

Na kama mie natamani nifikishe hizo miaka sasa mambo za 25% hapana kwa kweli. 😀😀😀😀
Ha ha ha ha acha woga muda wako ukifika wala hakutakuwa na hayo mambo
 
happy birthday big mamaaa[mama kubwaaa]....kuna mmoja pale arusha anaitwa mama kubwa kweli mama kubwaa anabonge la kalio
 
Ba mkubwa alikata kona siku nyingi alikimbia na dogodogo anasubiri watoto wapate kazi arudi analialia kama Baba Diamond, lakini hiyo hainizuii kuwa na furaha kufikisha nusu karne.

Aunti yake niwe mkweli huku kitaa wanawake wegi ni woga kuishi maisha unayoishi ww sasa hv..wanagugumia tu...samahan unaweza kuwaambia nn wanawake wa namna hyo?i mean una neno gan zuri la kuwapa moyo..au unaweza kutupa abc ulipitia changamoto gan zaidi (thou zinajulikana)..
nataman iwepo sredi ya kupeana changamoto baada ya maisha ya ndoa (kwa watalaka au watalikiwa au waloamua kutengana!ila najua itavamiwa!(watakuja na maneno mke mjinga huvunja nyumb yKe kw mikono yake mwenyewe😂😂epheww
 
Maisha ya kulea familia peke yako ni magumu madeni ni kitu hakiepukiki unakopa wee hadi ukifika mwisho wa mwezi unabaki mweupe. Jambo la kushukuru maisha yanakwenda hayagandi. Huwa nakosa majibu nikimuona baba Diamond anataka kutuzwa na kupendwa na mtoto aliemkataa. Nikikueleza maneno, kashfa, dharau za mtu niliezaa nae hutaamini kama ni binadamu wa kawaida. Kikubwa mimi binafsi nimemsamehe khs watoto nimewaeleza hawastahili kulipa kisasi kwani kisasi ni juu ya MUNGU sio wao. mioyoni mwao sijui wanawaza nini lakini kila wapoongea maneno ya chuki najaribu kuwarudisha kwenye mstari mengine nawaachia wao maana sitaishi milele wajibu wangu nimeutimiza kama mzazi. Kuhusu wanawake wanaopitia maisha kama yangu ushauri wasikate tamaa, watimize wajibu wao kadri wanavyoweza, kila kitu shida na raha vyote huwa vina mwisho wawe na furaha wajiepushe kuishi bila kufuatilia maisha ya watalaka/ EX wao watakuwa na amani kubwa.
 


Asante sana mamdg
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…