Kwa namna fulani matokeo tunayoambiwa ya uchaguzi kuwa CCM wamechukua viti vya Bunge kwa 100% mimi binafsi nimeyapokea kwa furaha sana, sio kwa kuwa naipenda CCM, la bali kwa kuwa CCM na wananchi kwa ujumla bado hawajatambua umuhimu wa kuwa na wabunge wa upinzani. Binafsi ningependa idadi ya viti sawa Bungeni kwa CCM na Upinzani, lakini mbunge yeyote wa upinzani akishinda kwenye uchaguzi huu ningependekeza ajiuzuru kuwapa CCM viti 100%.