Ni bora kutumia njia nyepesi kupambana na corona kabla hatari kuwa kubwa na kulazimika kutumia njia ngumu

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121

Janga la COVID-19 limesababisha vifo vyamaelfu kwa mamilioni ya watu nchini China naduniani kwa ujumla, na hadi sasa ugonjwa huubado unaendelea kusomba maisha ya watu katikanchi mbalimbali ambapo serikali zimeghumiwana kutojua la kufanya kutokana na kuzidiwa amakushindwa kuudhibiti kwa urahisi.

Katika kipindi cha mwanzo wakati ugonjwa huuunaibuka ambapo ilikuwa mwishoni mwaDisemba mwaka 2019, China iliathirika vibayana janga hili, lakini hatimaye ilifanikiwa kuzuiakuenea kwa muda mfupi tu.

Mafanikio haya yalipatikana kupitia hatua kali na za haraka ambazo ni pamoja na kuufunga mji, watu kujilinda, kudhibiti watu kutembea ovyo, kutenga rasilimali za kupambana na COVID-19, kutoa huduma za afya kwa njia ya kitaalamu nakusafisha maeneo mbalimbali kwa kutumiakemikali pamoja na kunawa mikono kwakutumia vitakasa mikono. Yote hayayamefanywa chini ya usimamizi wa serikaliikishirikiana kikamilifu na wananchi wake wote.

Wakati Beijing ilipokabiliwa na wimbi la pili la mlipuko wa virusi vya corona mwezi Juni 2020, baada ya miezi miwili kutoripoti kugundulikakwa mgonjwa mpya, hatua zilizochukuliwakuzuia kuenea kwa maambukizi ya COVID-19zimeonesha kuleta ufanisi mkubwa katikakupambana na mlipuko. Wahenga wanasemakinga ni bora kuliko tiba. Mwitikio wa haraka nahatua za kina na zinazofaa ndio muhimu zaidikatika kudhibiti janga hili ndani ya muda mfupi.

Hivi karibuni mikoa ya Anhui na Liaoning ilikabiliwa tena na kesi mpya za virusi vyacorona. Mara tu baada ya kugundua mtu mpyamwenye virusi hivyo, mikoa hiyo ilichukuahatua mara moja ya kuwafuatilia watuwaliowasiliana na wagonjwa wa corona nakupima watu wote ili kuzuia kwa urahisiugonjwa huo. Kwa mfano miji ya Lu'an na Hefeiyote imeanza kupima watu wa mji mzima nabaada ya siku tatu, karibu watu milioni moja wamji wa Lu'an na takriban watu 170,000 wa Hefeiwaliopimwa wote hawakupatikana na virusi vyacorona.

Lakini mbali na hapo mwamko wa wananchibaada ya kusikia kuna maambukizi mapya, ulikuwa mkubwa kwani wengi wa wale ambaobado hawajachanja walikimbilia kwenye vituovya kutoa chanjo ili kupatiwa chanjo.

Nikitupia macho nje ya China, nchi jirani yaIndia ambayo kiuchumi ina uafadhaliikilinganishwa na nchi nyingi za Afrika, yenyewe imepigika sana na ugonjwa huu, ingawa hivi sasa mwanga wa matumaini unaanzakuonekana kwa mbali baada ya grafu ya kesimpya kuonekana kutulia kiasi, tofauti nailivyokuwa wiki mbili au tatu zilizopita.

Lakini swali muhimu la kujiuliza kwa upande waserikali za nchi mbalimbali za Afrika ni kwambaje zinaitikia vipi au kuchukua hatua gani ilikupambana na ugonjwa huu thakili na kuwezakutimiza lengo la Shrika la Afya Duniani la kuutokomeza kabisa?

Kuna njia nyingi ambazo serikali zikishirikianana wananchi wake zinapaswa kuzitumiazikiwemo kuhakikisha wananchi wanachanjwa, uwepo wa mitungi ya oksojeni, dawa, mavazi yakujikinga watumishi wa afya, barakoa, mashineza kupumulia, vifaa vya kupimia ugonjwa wacorona, uwepo wa hospitali na vituo vya hudumaza afya kwaajili ya ugonjwa huu, kuwasaidiawananchi na nyinginezo.

Njia zote hizi ukizitathmini kwa kina utagunduakuwa zinahitaji gaharama kubwa sana ya fedha, lakini kwa nchi nyingi za Afrika inakuwavigumu sana kutimiza ama kufuata njia zote hizi, hasa ukizingatia kwamba hata kabla ya kujaugonjwa huu, mifumo ya afya ilikuwa dhaifu, ndio maana awali nilisema kinga ni bora kulikotiba, na pia tukumbuke kuwa mdharau mwibamguu huota tende.

Nchi ambazo zinajielewa uwezo wake kiuchumina kifedha kwamba hazimudu gharama kubwanamna hii, ni vyema zikashirikiana na wananchiwake kuchukua tahadhari na kufuata mfano ulewa China, ilipopambana na ugonjwa huu katikakipindi ambacho hakuna dawa wala chanjo, lakini ikafanikiwa kudhibiti kwa muda mfupi tu.
 
Afrika corona ilishaingia na ipo toka mwaka jana ila hadi leo mifano yetu kuhusu corona huwa tunatolea mifano nje ya Afrika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…