Ni Kweli
lakini hilo soka tamu lina watu wake sio tu kumfanya mchezaji acheze soka la aina hiyo, bali inategeama na player mwenyewe anaweza soka la aina gani..
thats alipokuja akafumua kikosi nusu chotee. na kuanza kusajili upya. Kuhusu sterling ni kweli kaongezewa makali na pep.. ila alikuwa player mzuri toka alipokuwa liver!
nae benardo alichukuliwa akiwa kwenye ubora wake na sio kwamba huko monaco alikuwa wa kawaida. nafkiri mnaikumbuk ile monaco ya kina mbappe,bakayoko,mendy,lemar. ilivyotesa kabla kina kina pep hawajaja kufumua kikosi kile..
all in all pep ni kocha!
Pep ni genius kwenye mpira kila mchezaji kabadilishwa tofauti na alivyokuwa
Hata Aguero siku hizi anahold mipira [emoji23][emoji23]
Swala kusema alibomoa kikosi huko ndo kujua kwenye sasa kwamba anauwezo wa kujenga kwanzia msingi hadi fence
Pep kabadilisha kila kitu England
England ilikuwa haitumii pesa kununua wachezaji lakini kwa sasa hata Everton inaingia sokoni ili angalau iweze kuhimili League
Pep kaifanya Man City ivutie wachezaji duniani
Zamani ilikuwa kucheza Man United ni ndoto lakini kwa sasa mchezaji kuchezea City ni ndoto kama kwenda Barcelona au Real Madrid
Pep anafanya hata uwe na njaa usahau kama unaangalia mpira wake..
Kocha Pekee ambaye Team pinzani zinajiandaa kupambana angalau kutoa sare au kufungwa goals chache
Kwa sasa ukiifunga City imekuwa moja mafanikio kwa team za EPL [emoji23][emoji23]
City ya kumtegemea Aguero imekufa kwa sasa akitoka jiwe anaingia chuma [emoji23][emoji23]
Utasikia Pep anasajili wachezaji wazuri hahahahah kwani Team zingne haziwaoni hao wazri...
Ukweli ni kwamba Pep anaujua mpira tena sio tu wa maneno ila na vitendo [emoji23][emoji23]