Uchaguzi 2020 Ni CCM kila kona, Wagombea Vyama vingine wako wapi?

Kwa Tanzania hii bado hatuna vyama vya upinzani tuna wasindikizaji tu
 
Kitu kimoja ambacho unabidi ujue ni kua wapinzani wanafaida kubwa kwenye hii nchi.
Mwisho,CCM sio chama cha Siasa labda kama ujui ilo..CCM ni idara ya dola sasa lazma ujue kua si kazi rahisi.
CCM inaongiza jeshi,tiss,polisi,mahakama,Bunge etc
 
NAthibitisha Kwamba kelele nyingi dhidi ya serikali ni kukosa hoja. Sasa wapinzani hawana wagombea, uzi kama huu umekosa kelele za aina hiyo.
CCMAGEREZA
 
Hapa unamaanisha hawa watu hawana wagombea, wanavizia watakaokatwa CCM. Maana ndicho walichofanya 2015.
 
Sio ccm, sema chama cha kijeshi. Chini ya awamu hii hakuna uchaguzi, bali kuna maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
Ha ha.. Mfa maji haachi kutapatapa
 
Kamuambie hayo maneno mwamba a.k.a DJ kama hajakulapua makofi au kukupiga na chupa ya faru John. Yaani wenzio wanapanga mikakati ya namna gani watapata ruzuku, wewe unahamasisha watu wasipige kura. Msipopiga kura atapata wapi ruzuku? Wabunge wa Viti Maalum (vipoozeo) watapatikana vp?
 

Huyo DJ atakula jeuri yake. Tukisema tunajitambua ujue tuna uhakika na tusemacho.
 
CCM kila kona kupokea na kutoa rushwa?
 
Utahangaikaje kugombea chama kingine na huku ukijua kuwa unasimamiwa na tume ya uchaguzi ya chama tawala? Utakuwa uenda wazimu kufanya hivyo. Utapoteza nguvu na pesa yako bure.
 
unategemea vipi uone wagombea wa upinzani kama kila siku wewe ni kusoma vijigazeti vya Uhuru, Tanzanite, Jamvi, nk? au kutazama TBC, Clouds, Channel 10, nk?
 
Je, ni woga wa wagombea na kulazimika kujikomba chama tawala? Au Wagombe ndani ya CCM wnaigiza upendo kwa chama kwa sababu zao binafsi?
Hizo sentesi mbili ulizoziandika ni ukweli halisi na uhalisia. Wagombea wengi lazima wajikombe kwa chama tawala ili kujilinda. Angalia mamia ya wasomi walivyojikimbiza chama tawala. Hii ni ishara kwamba hata wale tuliowatuma na kuwaamini wakatuletee maarifa wote wamelalia chama tawala na hakuna anayemfikiria mwananchi wa chini
 

Mbona hauoneshi nilipoonesha kuwalalamikia kwamba hawanipendi?
 
Hapa unamaanisha hawa watu hawana wagombea, wanavizia watakaokatwa CCM. Maana ndicho walichofanya 2015.
Ningemanisha ningesema Mimi Ila kwavile umesema wewe, Basi jua simanishi.
 
Siasa ya vyama vingi imenyongwa ili kuwanyina raia haki ya kuamua ili kukipa cha tawala na viongozi wake uwezo wa kuwamulia wananchi bila hofu. Wananchi wamegeuzwa misukule ya watawala. Ukiambiwa jumapili ni pilau na jumatatu mihogo mwananchi useme sawa kwasababu viongozi wanamaono. Ujinga wa kiwango cha lami. Haijawahi kutokea binadamu akapata maendeleo kwa staili hii kokote kule. Ukisikia udikiteta ndio huu.
 
Wagombea Wa upinzani wakijitokeza waziwazi wanatupwa ndani na mapolis..
 
Mkuu vyama vya upinzania vina struggle kutafuta wagombea.

Ushahidi, rejea Kauli ya Katibu Mkuu Mnyika aliposema "uwe uliandika barua ya kutoa nia au hukuandika wewe njoo uchukue fomu"

Sasa kulikua na haja gani ya kutia nia kwa barua Kama halikua ni sehemu ya utaratibu wa kuwatambua na kuwachambua wagombea?

CUF wanalia na meno kusagika watu hawapo, mtu akipima maji anaona eeh "maji mazito kuliko damu ya chama"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…