MFAHAMU CHIEF DODO, HII NDIO HISTORIA YAKE FUPI
Ukitaka Kuizungumzia Mbulu au Manyara kwa ujumla Huwezi kuacha Kumzungumzia mtu Mmoja Maarufu anayeitwa Amri Dodo..Mtoto wa Chiefu wa Kabila Dogo la Wagorowa ambao wana tofauti Ndogo sana na Kabila la Wairaqw..
Wagorowa Wanapatikana Wilaya ya Babati Mkoani Manyara na Kwa Kiasi Kidogo pia Wanapatikana Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma..
Kwa Majina yake ya Kuzaliwa..Anaitwa Amri Beo Dodo alizaliwa kati ya mwaka 1910..Historia inasema alizaliwa Huko Babati..
Ni Mtoto wa aliyekuwa Chief wa Kabila la Wagorowa Chief Beo Dodo, Amri Dodo alijipatia elimu yake katika shule ya sekondari Moshi (Old Moshi) Kisha Akamalizia shule ya Watoto wa Machifu ya Tabora (Tabora Boys). Ambapo alimaliza Mwaka 1936
Katika ujana wake Amri Dodo alikuwa kijana Muhimu Mno kwa Ukoo wake Akitokea Ukoo unaitwa Harnaa (Ukoo wa Kigorowa).
Baada ya kumaliza masomo yake Amri alifanya kazi kama Karani akiwa chini ya Baba yake, kazi hii alifanya kwa miaka saba, alitokea kuwa Kijana Muhimu sana!
Baada ya kazi ya ukarani Amri akateuliwa tena kuwa Chiefu mkuu katika Boma la Mbulu na kazi hii pia aliifanya kwa Miaka saba!
Kutokana na uzoefu wake katika shughuli za Kiuongozi Amri Dodo aliteuliwa Kuwa Chief Msaidizi mwaka 1950 yaani Msaidizi wa Baba Yake..
Ilipofika Mwaka 1952 Baba yake Amri alifariki Dunia kitu kilichopelekea Amri kuwa Chief Halali wa Kabila la Wagorowa.
Pia ikumbukwe Amri Dodo Pamoja na Kuongoza Kabila la Wagorowa aliweza Kuongoza Mpaka Upande wa Mbulu.
Mwaka 1955 Bwana Robert Gray alifanya Mazungumzo na Amri Dodo, Katika mazungumzo hayo Amri alimwambia kuwa Baba yake pia aliwahi Kutawala Kabila la Wambugwe.
Bwana Robert anamuona Amri Dodo na Gari lake Jipya aina ya Peugot station Wagon, na Amri alikuwa akiishi katika Jumba kubwa tu (Hapa Nacheka Kidogo).
Japo alikuwa Akiongoza Kabila la Wapagani.. Amri Dodo alikuzwa Katika Imani za KiMohamedan (Yaani waumini wa Mtume Muhammad)..Kwa Maana hiyo alikuwa na uwezo mkubwa wa kuona haraka sana mwezi mtukufu wa Ramadhan.. Pia kutokana na Imani yake ya Kiislamu Amri alikuwa na wake zake Halali wanne na hakuwa Akinywa Pombe.
Amri alikuwa Kibaraka wa wazungu yaani wakoloni kwa wakati ule walikuwa Waingereza.. yaani aliwasaidia katika kukuza himaya na kuimarisha tawala zao wakitumia Machifu Miongoni Mwao alikuwa Amri Dodo..Kitu kilichopelekea kuteuliwa na D.C wa Kiingereza wa Wakati huo Mr C.I Meek, kuwa Miongoni mwa Machifu watano watakaoenda Uingereza..
Mwaka 1954 (Septemba na Agosti) Amri akateuliwa Rasmi kwenda Uingereza na alikuwa kiongozi wa wale Machifu Wengine Wanne na kuteuliwa kuwa Mzungumzaji Mkuu Mara Wafikapo Uingereza..
Machifu Hao walikuwa
Sylvanus Kaaya wa Kabila la Wameru
Sefania Sumlei wa Kabila la Waarusha
Sabu bin Sabu wa Morogoro
Paul Norbert wa Mtama Lindi
Ila kabla ya Kuondoka Babati ilionekana Amri Hajui Chochote Hasa katika ustaarabu wa Mlo wa Kizungu ikabidi D.O wa babati ampe kozi ya siku kadhaa kuhusu ustaraabu wa kula.
Ikumbukwe Pia Amri Dodo alikuwa anazungumza Kiingereza Kizuri sana Japo Pia alikuwa akikijua Kiswahili vizuri Zaidi kutokana na kukitumia mara kwa mara katika shughuli zake hasa zile alizokuwa akizifanyia Mbulu
KISA CHA CHIEF DODO NA CHIEF SARWATT
Kwa Wale Wataalamu wa Historia mtakumbuka kulifanyika Uchaguzi Mkuu Mwaka 1961, Wakati Huo Mwl Nyerere alikuwa Waziri Mkuu, akiwa na chama chake cha TANU kwa sasa (CCM) mwl Nyerere na wanaTANU wenzake walimteua Chief Amri Dodo Kuwa Mgombea Ubunge Kupitia Jimbo la Mbulu (Wakati huo Jimbo la Mbulu iliunganisha Babati, Karatu na Hanang na Mbulu Yenyewe)..
Mara Ghafla akajitokeza Kijana Mdogo anayeitwa Herman Elias Sarwatt (Mwairaqw) (Kwa sasa Maarufu Kama Chief Sarwatt).. Akiwa MwanaTANU pia.. aliwapinga sana wanaTANU kwa kwa uteuzi wao ule.. Sarwatt aliwaambia.. Alaa! Hiki chama changu hakina akili hata kidogo. Hawa viongozi wangu hawana, akili! Hawa machifu ndio zamani wakitaka kutufunga wakati tukigombana na mkoloni. Leo wanamchukua Chief Dodo aliyetaka kutufunga sisi ndiye awe mbunge wetu katika jimbo la Mbulu?..
Kwa kitendo kile Wairaqw Wakatokea saana Kumpenda Sarwatt..Hapo Herman Sarwatt akajisimamisha Rasmi Kama Mgombea Binafsi yaani Hakugmbea kwa ilani ya Chama Chochote..na alikubalika Sanaa..
kitu kilichopelekea Nyerere Kusafiri Toka Mbeya Hadi Mbulu Kumpigia Debe Chief Dodo, Kwa bahati Mbaya sana Jitihada za Mwalimu Hazikuzaa Matunda..
Pia inasemekana Kwamba baada ya Mkanganyiko kati ya Chief Dodo na Sarwatt Mwl Nyerere aliwaambia Herman Sarrwat na mgombe mwenzake (Chief Dodo) kutoka TANU kwamba atakayewahi kufika Dodoma ndie atakuwa mbunge wa Mbulu Halafu baadaye Mwl Nyerere akampa mgombea wa TANU (Chief Dodo) Gari aina ya Land Rover ili awahi kufika Dodoma. Kitendo Hichi Kiliwachukiza sana Wairaqw ..Wairaqw wakachangishana na kuuza ngombe wakamkodia Sarwatt ndege ya Mzungu.
Mwl Nyerere alipomkuta Sarwatt asubuhi mlango wa ikulu ndogo ya Dodoma hakuamini.
Basi ikabidi Mwalimu akubali ya kuwa Sarwatt Ndiye mbunge Halali wa Jimbo la Mbulu na Mwl Nyerere hakuwahi kukanyaga mMulu tena.
Hatua hii ya Herman Sarwatt Kushinda Kama Mgombea Binafsi ndio Kitendo Kilichopelekea Kupingwa au Kupitishwa Kwa Sheria inayokataza Mgombea Binafsi.
Hiyo Ndio Historia Fupi inayomhuhusu Amri Dodo Al-Maarufu Chief Dodo, Pia Kukiwa na Shule Moja Mjini Babati ikiwa na Jina la Chief Dodo..Kwa Heshima ya Huyu Bwana..
NOTE: Historia hii nimeandika kwa Kadri ya Ufahamu wangu Kuhusu Chief Amri Dodo..Ukiwa na Nyongeza Yoyote tafadhali usisite kutufahamisha sisi wengine kupitia kitufe cha kutolea Maoni (Comments)..
Kwa Hapa Chini Nimeunganisha na Picha zao..
Picha yenye Rangi ni Chief Dodo Akiwa na Binti yake Mdogo aliyekuwa Akisoma Shule ya Msingi wakati Huo..
Picha Nyigine inamuonesha Mwl Nyerere akiwa na chief Dodo (Aliyevaa Miwani)..Wakati Huo Mwl Alikwenda Mbulu Kumpigia Kampeni Amri Dodo..
Picha Nyingine ni Mwl akiwa na Kijana Mdogo wakati Huo Herman Sarwatt Mjini Dodoma..
Kupata Makala kama hizi na nyinginezo kwa haraka zaidi Follow Ukurasa wangu wa Instagram kupitia hiki kiunganishi
Instagram.com/AlfredDPatrick
Mimi Tena
Patrick Alfred
Call/Sms/WhatsApp: 0787887745